Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Nadhani tungeruhusu wataalamu wa afya,

what if matone yakadondokea kwenye barakoa na vitundu vyake vinapitisha kirusi?
inakuwa imekusaidia nini?
 
Na kigamboni ilivyo na wasukuma wengi vile,, atapita asubuhi tu,,
 
Bashite kwanini anaachwa apoteze raia na elimu yake ya fafafafafafafafa div zero? Yaani anatamka kabisa watu wafunge vitambaa vya jasho kufunika pua na mdomo kujikinga na corona?? Jackma kagawa barakoa bure,matajiri wamechangia bil 6 kwanini wasinunue "santaiza na max" na kuwapa wananchi bure?
 
Makonda yuko sahihi.
Ni bora kuvaa barakoa ya kitambaa.
Lesso ikikunjwa vizuri inazuia Corona kusambaa .
Na pia kitambaa ni rahisi kukifua kwa sabuni na maji ya moto na kukipiga pasi kwa wale wasio na Sh.3000 /- za Maski ya kitabibu inayonunuliwa kila siku na kuibadili kila baada ya masaa manne.

Huyo waziri atakua na mafamasi mengi na amelenga kufanya biashara.
Ubinafsi wa mwanadam ndio ulioleta Corona kwa manufaa ya kiuchumi zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa anahitajika mganga mkuu wa serikali kutoa msimamo wa kitaifa juu ya Barakoa tunazopaswa kutumia na namna ya matumizi yake.

Ndiposa namuomba mganga mkuu wa serikali atoe ufafanuzi wa kitaifa utakaojikita kwenye sayansi na uchumi.

Naomba kuwasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
Naunga mkono hoja
P
 
Haha kwahiyo Gavana anakwenda kupambana na Dr??
 
Wakuu huku mtaani kuna trend ya watu kuvaa mask zenye material ambayo yanaonesha wazi kua ni sidilia na hakuna mwenye habari wala kutilia shaka.

Sasa unakuta hizo sidilia zenyewe zimechukuliwa kwenye mabelo ya mitumba huna uhakika wa usalama wake. Hujui mvaaji wa mwanzo alikua anamatatizo ya aina gani, pengine alikua na kansa ya titi lakini kwasababu ya maslahi ya muuzaji na unafuu wa bei kwa mnunuzi watu hilo hawalijali.

Tangu kauli ya mkuu wa mkoa kusema vaeni hata kanga kama mbadala wa mask, huku mtaani imekua ni extreme sasa

Wizara ya afya itoe kauli ya moja kwa moja ijulikane ni aina ipi ya mask zenye uwezo wa kutukinga. Mkiacha watu wajiongeze ilimradi wafuniko midomo na pua, mtasababisha mlipuko wa maambukizi mengi ambapo watu watakua wahaogopi kukaribiana huku wakiamini mask walizovaa zitazuia virus vya corona kutokana na kauli iliyotolewa kua vaeni chochote.
 
Hapa anahitajika mganga mkuu wa serikali kutoa msimamo wa kitaifa juu ya Barakoa tunazopaswa kutumia na namna ya matumizi yake.

Tumeshalisikia agizo la RC Makonda kwamba tuvae barakoa hata za Leso na vitambaa vingine na tumemsikia pi Naibu waziri wa afya Daktari Ndugulili kwamba kitambaa hakizuii virusi wala bakteria kumdhuru mtu. Wote tunawashimu na mawazo yao pia.

Ndiposa namuomba mganga mkuu wa serikali atoe ufafanuzi wa kitaifa utakaojikita kwenye sayansi na uchumi.

Naomba kuwasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
Matokeo yake ni haya.
F5F6C644-696A-4333-925C-5F596ECB990A.jpeg

CA56C132-4B01-4447-B6D6-FE0268CADB16.jpeg

86B47B97-FE06-452E-9036-1D2AA74201FC.jpeg

DE69136D-BD7C-496A-8B89-C97F015C07EA.jpeg
 
Kwahiyo hili la kuvaa sidilia puani nalo linahitaji wizara ya afya itoe kauli?

Nitailaum sana wizara kama itatoa tamko eti tusivae sidiria puani ni aibu sana hatujawa wajinga kiasi hicho wanaovaa acha wavae kwa utashi wao
 
Back
Top Bottom