Ndungulile alitaka sayansi itawale na sio ujinga wa nyungu sijui kujifukiza ambako hakuna ushahidi wa kisayansi kama kunatibu ugonjwa. Hii iko kinyume na matakwa ya boss anaetaka ujinga ndio utumike kama tiba ya corona...
Mheshimiwa Raisi Dr John Pombe Magufuli hajakosea kabisa kutengua uteuzi wa Mheshimiwa Faustine Ndugulile kwa sababu
-Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mamlaka ya kuteua na kutengua
-Faustine Ndugulile hana uwezo na Sifa za kuendelea kuwa katika nafasi hiyo.
-Faustine Ndugulile ni mtu mwenye mawazo finyu yasiyoweza kutatua matatizo makubwa kama hili linaloikumba dunia.
_Anaonekana ni mtu ambaye hawezi kuelewa jambo kwa haraka labda mpaka apewe muda mrefu wa kufikiri.
-Ni mtu aliyekosa busara ya kawaida sana (common Wisdom).
-Ni mtu ambaye kama angeishi kabla ndege haijagunduliwa asingeweza kuamini kwamba mwanadamu angeweza kutengeneza chombo kinachoruka.
-Anaonekana ni mtu ambaye hatambui kabisa kuwa uzoefu yaani "experience" ndiyo mamlaka ya mwisho ambayo haiwezi kupingwa na utafiti wala malaika au ufunuo wa aina yoyote.
-Anaonekana wazi kuwa amekosa nguvu 12 ambazo mwanadamu hasa anaetaka kuwa kiungozi anatakiwa kuwa nazo: Hapa ninamaanisha kwamba:- Ni mtu aliyekosa vitu vifuatavyo:
1-Hana imani Kabisa
2-Hana maono
3-Hana uwezo wa kujieleza na uelimisha umma
4-Hana Busara
5-Hana uwezo wa kufikiri kwa ufasaha
6-Hana ari ya kazi
7-Anaonekana ni mtu ambaye anatumia muda mwingi kufikiri mambo yaliyopita na mambo yajayo kuliko mambo yaliyopo na hivyo muda mwingi kuwa katika mkanganyiko wa mawazo.