Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Dalili za mapungufu yaani ukitoka chadema ukasifia an kumtukana Mbowe utapewa uwaziri wakati huohuo Hawa wanapigiana simu na Mbowe na kucheka. Mnafikiria mtu kaamka tu na fikra za CCM!
 
Dooohh kwahiyo V8 Kilimo kwanza,nyumba ya bure,mafuta ya bure,perdiem na marupurupu ya uwziri ndio yamekata!!
 
Masikini alishindwa kuimba mapambio kama Mwigulu

Kumbe usiku ni mkubwa, ndio najua haya hapa JF baada ya kukosa usingizi
 
Ukiwa na "layman" kwenye masuala nyeti harafu mbishi, mjeuri na mwenye ego kubwa kuliko kichwa chake, ni tatizo.

Dr. Ndungulile alipinga huo ujinga wa kupropagate the so called nyungu bila facts (miti ipi, kiasi gani, ujifukize dakika ngapi etc). Pia alipinga mambo ya barakoa za kushona. Kiufupi alikuwa anampa shule Jiwe na kwa Jiwe hilo ni kosa kubwa
Aliyethibitisha hiyo miti ina impact ya ku compromise viral activity ni nani na kama inafanya kazi iwe extracted zipatikane vaccine....na hili swala la nyungu walitakiwa watumie watu gani yani mtu tayari ni victim ana dyspnoea afu ajifukize wakati tayari ana respiratory depression....medicine ni ngumu sana ila basi tuheshimu tu maamuzi ya mzee wetu.. Nimefikiria kwa sauti kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah nimekumbuka enzi za ugomvi wa Bashite vs Gwajima kila J2 asubuhi watu wametega sikio ufufuo na uzima.
 
Hivi bado yuko mafichoni? au amerudi Dar/DDM. Zito alisema "anasikia tetesi" yuko njiani kurejea
 
Ndungulile alitaka sayansi itawale na sio ujinga wa nyungu sijui kujifukiza ambako hakuna ushahidi wa kisayansi kama kunatibu ugonjwa. Hii iko kinyume na matakwa ya boss anaetaka ujinga ndio utumike kama tiba ya corona...
Mheshimiwa Raisi Dr John Pombe Magufuli hajakosea kabisa kutengua uteuzi wa Mheshimiwa Faustine Ndugulile kwa sababu

-Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mamlaka ya kuteua na kutengua

-Faustine Ndugulile hana uwezo na Sifa za kuendelea kuwa katika nafasi hiyo.

-Faustine Ndugulile ni mtu mwenye mawazo finyu yasiyoweza kutatua matatizo makubwa kama hili linaloikumba dunia.

_Anaonekana ni mtu ambaye hawezi kuelewa jambo kwa haraka labda mpaka apewe muda mrefu wa kufikiri.

-Ni mtu aliyekosa busara ya kawaida sana (common Wisdom).

-Ni mtu ambaye kama angeishi kabla ndege haijagunduliwa asingeweza kuamini kwamba mwanadamu angeweza kutengeneza chombo kinachoruka.

-Anaonekana ni mtu ambaye hatambui kabisa kuwa uzoefu yaani "experience" ndiyo mamlaka ya mwisho ambayo haiwezi kupingwa na utafiti wala malaika au ufunuo wa aina yoyote.

-Anaonekana wazi kuwa amekosa nguvu 12 ambazo mwanadamu hasa anaetaka kuwa kiungozi anatakiwa kuwa nazo: Hapa ninamaanisha kwamba:- Ni mtu aliyekosa vitu vifuatavyo:

1-Hana imani Kabisa

2-Hana maono

3-Hana uwezo wa kujieleza na uelimisha umma

4-Hana Busara

5-Hana uwezo wa kufikiri kwa ufasaha

6-Hana ari ya kazi

7-Anaonekana ni mtu ambaye anatumia muda mwingi kufikiri mambo yaliyopita na mambo yajayo kuliko mambo yaliyopo na hivyo muda mwingi kuwa katika mkanganyiko wa mawazo.
 
Ndungulile anasema nyungu zina madhara lakini anasahau kwamba hata hizo dawa anazoziamini yeye toka nchi zilizoendelea zina madhara pia. Kwangu mimi hakua na faida yoyote kwani ameshindwa kuboresha tulichonacho anabaki kusubiri kuletewa dawa na nchi zilizoendelea ambazo hata wenyewe wana hali mbaya kwa hili.
Akakae kando kidogo ajifunze

..Dr.Ndugulile ni shujaa.

..kiapo chake cha Udaktari kinamtaka asipotoshe wagonjwa.

..Nyungu zinaweza kusaidia ktk changamoto tofauti, lakini hazifai kwa wagonjwa wa covid19.

..madai kwamba nyungu zinatibu covid19 ni UZUSHI, na Dr.Ndugulile yuko sahihi kukataa kueneza uzushi utakaokwenda kuwadhuru wananchi.
 
Back
Top Bottom