Naibu Waziri wa Habari aagiza washindi wa Shaaban Robert watunge wimbo kumsifu Magufuli kwa gharama za Serikali

Naibu Waziri wa Habari aagiza washindi wa Shaaban Robert watunge wimbo kumsifu Magufuli kwa gharama za Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Naibu Waziri wa Habari amewaagiza vijana walioshinda tuzo za kiswahili za Shaaban Robert watunge wimbo kumsifu Rais Magufuli kwa anayoyafanya kisha wimbo huo utarekodiwa katika Studio za TBC kwa gharama za serikali.

Ameyasema hayo alipokuwa anapokea tuzo ya juu ya Kiswahili ya Shaaban Robert ambayo ametunukiwa Rais Magufuli.
 
Kuwepo na wananchi wenzetu ambao ataona hapana tatizo lolote juu ya maagizo haya ndio sababu kuu Tanzania daima itakuwa nyuma kimaendeleo na tutashindwa kuamka kimawazo na kuwa na uwezo wa kufikiri nje ya boksi.
 
Enyi viumbe wa dunia hii msifuni na kumtukuza Mola peke yake,kumtukuza binadamu ni makufuru kwa Mola wetu.
Wapi waziri au mleta mada kasema kumtukuza Magufuli?

Kasema kumsifu na kusifiwa binadamu akifanya vizuri ni kawaida hajasaema kumtukuza kuwa mwelewa usilete geuzageuza yenu ya maneno.
 
Napita kwa mbali kabisa, huku nakimbia.
🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu
Usijifanye wewe hapa duniani humtgemei binadamu, yaani uko kivyako Kama nyumbu.

Biblia imesema alaaniwe amtegemeaye mwanadamu HUKU AMEMSAHAU MUNGU.

Usikatishe vifungu vya biblia ili upate maana ya kishetani utalaaniwa.
 
Yani anamuona Magufuli ni bora kuliko hata Mungu. Vijana waache kumsifu Mungu wamsifu mwadanamu. Huu nao ni utumwa.
 
Back
Top Bottom