Pre GE2025 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aandika barua ya kujiuzulu Ubunge

Pre GE2025 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aandika barua ya kujiuzulu Ubunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mzee wa DP World nchi iko pazuri sana, haihitaji mabadiliko yoyote yake. Binafsi nashauri Raisi Samia auze mbuga zote tu kama alivyofanya kwenye bandari, maana hata zikibaki sisi hatuwezi kuziendeleza. Hata hivyo, waarabu wana uzoefu na akili nyingi kuliko sisi.​
Mkuu umepiga panapo uma. Ila kwakuwa akili ya huyo imepigwa ganzi na warabu wa dp hawezi sikia maumivu ya kipigo chako
 
Mbunge kateuliwa na Rais, inakuaje aombe kujiuzulu kwa Spika, pamoja na kwamba Spika ni bosi wa wabunge (mwenye kuelewa katiba hii imekaaje?)
IPO sawa kabisa, jambo la msingi ,hii lazima ,imeanzia kwa Rais mwenyewe, kwanza Rais ndie alimteua kuwa Mbunge,pili Rais ndie alimteua kuwa Naibu waziri, kwahiyo kabla ya maamuzi lazima alimshirikisha Rais.


Kinacho shangaza , ni kwamba ,huu sio utaduni wa nchi hii, labda kama kalazimishwa na Rais kujiuzulu! Hatujazoea kuona binadamu Mtanzania anaachia kazi ya Unaibu waziri kwa sababu nyingine yoyote , halafu ameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi mbili ambazo ni hot cake kwa Mtanzania (ubunge na unaibu waziri) ngoja tusubiri ila kwa hili sio bure! Kuna jambo
 
Tiss sina uhakika maana wanateuliwa hao lazima wafuate ya rais. Ila kwa jeshi nimeshangaa sana kuona jeshi linaloabudu wanasiasa badala ya kuhakikisha linalinda katiba.
Wapi katiba imekanyagwa

USSR
 
Back
Top Bottom