Naibu Waziri wa Nishati: Mgawo wa umeme nchini utaisha mwezi wa tatu

Naibu Waziri wa Nishati: Mgawo wa umeme nchini utaisha mwezi wa tatu

Moja ya hasara za Ukiritimba katika service delivery ni hii. Poor service
 
Mradi wa umeme wa Julius Nyerere ni moja ya mradi unaotekelezeka kwa weledi mkubwa sana, sote tunajua mwezi wa sita mwaka huu ndiyo tulitegemea kuwasha mtambio namba 9 kwa mara ya kwanza lakini kwa jitihada za serikali na wakandarasi tuliweza kusogeza ratiba za kuwasha mtambo huu hadi mwezi wa pili, jana tumefanikiwa kufanya majaribio kwa ukamilifu kwenye mtambo namba 9 na tumeutembeza kwenye uwezo wake wa mwisho wa megawati 235," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

"Tuliahidi mwezi huu tuna ratiba ya kuzindua mtambo huu na ratiba hii iko palepale, tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuvumilia, matumizi ya umeme yanategemeana tukizalisha mwezi huu mgao utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunazalisha megawati 235 na mwezi wa tatu tutazalisha megawati 235 hivyo zitakuwa megawati 470 uhakika ni kwamba kufikia mwezi wa tatu mgao wa umeme utaisha nchini," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

Pia soma
- Februari 16 Serikali ilisema umeme mwisho kukatika. Ulipo umeme upo?
Tupo vizur, tunaendelea vizur, tunaelekea pazuri na kwakweli tutafika pazuri sana muda usokua mrefu,

Na wananchi wote wa Tanzania watafurahia matunda ya mikakati na mipango madhubuti ya serikali ya awamu ya6 chini ya Dr Samia Suluhu Hassan kwenye umeme na huduma nyingine muhimu za kijamii humu nchini...

Ile muhimu zaidi, ni wananchi kuendelea kuwa wastahimilivu na wenye subra wakati jitihada za kukamilisha miradi hii ya kimkakati ikiendelea kutekelezwa kwa bidii, kasi na viwango tajika usiku na mchana 🐒

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Pamoja na haya yote bado wakati wa uchaguzi kuna watu watasahau watakichagua tena hiki chama kinachounda hii serikali iliyoshindwa hivi
 
Tanga nchi imepata uhuru, mgao wa umeme haujawahi kuisha na hautokwisha
 
Huyu kama ndio aliyesema mgao utaisha February 16, 2024, hakupaswa kusogeza tena tarehe mbele, alitakiwa awe ameshajipima na kujiuzulu.

Viongozi wa kiafrika ni kama matapeli vile, hawawezi na hawapendi kuwajibika kwa kauli zao. Ikifika March atasogeza tena tarehe, subirini muone.
Hawa bora wanyamaze tu
Waendeleee tu na mgawo na kuzima
Umeme wakijisikia kurudisha waarudishe

Ova
 
Huyu kama ndio aliyesema mgao utaisha February 16, 2024, hakupaswa kusogeza tena tarehe mbele, alitakiwa awe ameshajipima na kujiuzulu.

Viongozi wa kiafrika ni kama matapeli vile, hawawezi na hawapendi kuwajibika kwa kauli zao. Ikifika March atasogeza tena tarehe, subirini muone.
Mmh ngumu kumeza
 
Mimi namuomba sana Mwenyezi Mungu awaadhibu hawa viongozi wa Serikali kwa kwa yale yote ambayo Mungu anajua SIO YA HAKI kwasisi wananchi. Kimsingi wameshagundua unyonge wetu. Mwenyezi Mungu awahukumu wao na watoto wao ili nao waikose furaha.

Imagine kila kukicha ni kuahidi tarehe na wanapoona tarehe zimekaribia wanajitokeza na kuahidi tarehe zingine. Wao wana uwezo wa kutumia solar na majenereta.
Kwa mfumo ulipo Tanzania sio rahisi wananchi kuwawajibisha viongozi. Viongozi wana nguvu kubwa sana dhidi ya wananchi. NDIO MAANA NAMUOMBA HURUMA YA MUNGU KWETU WANANCHI NA AWAADHIBU HAO VIONGOZI

Mhe Spika tambua kuna Mungu aliyekuweka hapo
 
Kisingizio kingine kitakuwa kukosekana mvua za masika, na hapo hapo mvua zikinyesha maji hayaingii kwenye bwawa la kuzalisha umeme ila kwenye mabwawa ya pemebeni yapo full......tupeni na ratiba ya kuisha kwa mgao wa sukari, bila kusahau kuanza kwa safari za SGR.
 
Mradi wa umeme wa Julius Nyerere ni moja ya mradi unaotekelezeka kwa weledi mkubwa sana, sote tunajua mwezi wa sita mwaka huu ndiyo tulitegemea kuwasha mtambio namba 9 kwa mara ya kwanza lakini kwa jitihada za serikali na wakandarasi tuliweza kusogeza ratiba za kuwasha mtambo huu hadi mwezi wa pili, jana tumefanikiwa kufanya majaribio kwa ukamilifu kwenye mtambo namba 9 na tumeutembeza kwenye uwezo wake wa mwisho wa megawati 235," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

"Tuliahidi mwezi huu tuna ratiba ya kuzindua mtambo huu na ratiba hii iko palepale, tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuvumilia, matumizi ya umeme yanategemeana tukizalisha mwezi huu mgao utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunazalisha megawati 235 na mwezi wa tatu tutazalisha megawati 235 hivyo zitakuwa megawati 470 uhakika ni kwamba kufikia mwezi wa tatu mgao wa umeme utaisha nchini," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

Pia soma

Huu uongo na usanii unamsaidia nani? Tutaenda kwenye uchaguzi tukiwa gizani, kwa dizaini ya watu wa aina hii. Hawamaanishi.
Wanaona sawa kutudanganya maana hawawezi kufanywa chochote...aibu sana

Ngoja nimsikilize Karubandika...ananikumbusha enzi zangu wakati nacheza chipukizi. Na kweli chama kilishika hatamu 😂 😂 😂 😂 😂 😂

View: https://www.youtube.com/watch?v=6T9GzLGswG0
 
Mimi namuomba sana Mwenyezi Mungu awaadhibu hawa viongozi wa Serikali kwa kwa yale yote ambayo Mungu anajua SIO YA HAKI kwasisi wananchi...
Viongozi wa hii nchi wanawadharau sana wananchi, wanaona kama wanawamudu sana. Lakini pia kingine, wanaamini kabisa sanduku la kura ni geresha tu (rejea alichosema Prof. Tibaijuka kuhusu Lowassa) kilochotokea 2020 na wananchi tukaufyata kimezidi kuwapa kiburi zaidi CCM.
 
Back
Top Bottom