Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Kojoa ukalale. Njaa mbaya. Ndio maana unaitwa Mayala
 
Kwan undhan hajui alitendalo?huyu yawezekana.kuna mawili mosi sababu ya kabla lake pendwa au din yake.pendwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ya chadema ndiyo tatizo la serikali ya Tz.........Chadema bado haijatengenezwa kama taasisi imara ambayo hata asipokuwepo fulani inaweza kujiendesha bila shida,Ni kama tunavyo msikia Jpm akisema haya ninayofanya nikiondoka yatafanyika kweli.

Shida ya Chadema haijajengwa kama taasisi
 
I'm learning something here and try to compare notes.

Thanks.
P
 
Tangu awamu hii iingie madarakani tumeshuhudia jinsi CDM in particular, inavyoandamwa, viongozi karibu wote wana kesi za ajabu ajabu mahakamani, wamewekwa rumande na kunyimwa dhamana kwa sababu ambazo hata mahakama ilishangaa, mikutano imezuiliwa, wengine wamenusurika kuuawa na wengine kuuliwa kabisa. Katika hali kama hii ingekuwa maajabu kama CDM au upinzani kwa ujumla wasingetikisika. Nashaanga Paskali kushangaa CDM kuonekana kuyumba huku ukijua tatizo liko wapi. CDM wanaweza kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu, lakini umakini mkubwa unahitajika.
 


Mbowe angesimamishwa na LEMA AU LISSU

Mwambe ni garasa tu

lengo wampe Mbowe

Pia mwambe hajaoa kwa mtei.period
 

Paskali,
Ukweli ni kwamba ulichoongea hapa ni pumba.uongo,unafiki na uzandiki ambao hauna tija yoyote kwa CHADEMA na Wanachadema kwa ujumla wao.
Let me say this to you: Paskali wewe ni mnafiki na hujawahi kuwa mpenzi wala mwanachama wa CHADEMA. Kama kuna siku utajiunga na CHADEMA basi wewe utakuwa ni PANDIKIZI sawa na kina Lowassa,Sumaye au Kitila Mkumbo.
Kauli zako, misemo na mabandiko yako hapa Jeiefu yana dhihirisha uongo na unafiki wako kuhusu CHADEMA.

Kwa bandiko lako hili kuelekea Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA wewe unaonekana kabisa unataka Mhe. Mbowe asichaguliwe tena...!!!Hivi kwa akili yako unafikiri Cecil Mwambe anaweza kuiongoza CHADEMA kwa udhaifu alionao?Katika kipindi hiki ambacho kuna Utawala wa Rais Magufuli ambaye kwa kila dalili anaonekana ana chuki na Wapinzani na hasa CHADEMA mtu kama Mwambe hawezi kukabiliana na Magufuli...!!!

Mhe. Mbowe amedhihirisha kuwa ni kiongozi wa mfano na ana uwezo wa kuimudu mikiki mikiki ya Magufuli na ndiyo maana juzi kwenye Sherehe za Uhuru/Jamhuri kamwambia Magufuli point black kuwa umefika wakti sasa ni lazima Magufuli akubali kukaa meza moja na Upinzani ili kuleta mwafaka na mustakabali wa Taifa letu...!!!

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anaona nini kinachoendelea kuhusu Uchaguzi wa Viongozi wa Juu wa CDM. Mbowe anapigwa vita kutokea CCM na mapandikizi yaliyoko ndani. Mbowe amedhihirisha kuwa ni Kiongozi Makini, Mweledi, Mwerevu na bora sana kwa nyakati zote za Siasa za Upinzani. Mbowe ndiye Kiongozi tishio kwa Utawala wa JPM na CCM.
Kila mbinu zinafanywa kuhakikisha Mbowe hachaguliwi tena kuiongoza CDM.....!!!Hilo ni kosa kubwa sana CCM na wachukia CDM wanalofanya....!!!

Hivi Mbowe akiendelea kuiongoza CHADEMA hata kwa miongo 2 au 3 kuna shida gani? Mbona CCM kuna Viongozi wakubwa kabisa wanataka MAGUFULI AONGEZEWE MIAKA MINGINE 5,10 au AWE WA MAISHA moja kwa moja?
Lakini wana CDM wakisema wanataka Mbowe aendelee kelele zinakuwa nyingi sana.....???Tatizo nini? Mbona CCM mmeendelea kutawala kwa miaka yote hii 25 tangu tuanze mfumo wa vyama vingi(1995-2020)? Kama ni swala la kung'ang'ania madaraka mbona CCM hamlioni upande wenu?

Pasi-kali acha DEMOKRASIA itamalaki ndani ya CHADEMA. Usitake kuwalisha wana CDM matango pori kwa kutaka Cecil Mwambe awe Kiongozi wa CDM mtu ambaye nina hakika ataishia kuji-MWAMBEFY tu!!
 
Mtoa mada ungelifanyia hili jukwaa haki kama ungewashauri hao ccm wenu wajifunze kuheshimu demokrasia na kuacha kujificha kwenye mgongo wa polisi na wasiojulikana kukandamiza vyama vingine.

Kama ni kushauri, basi ushauri wako ulipashwa uuelekeze huko ccm make ndicho chama kilichobaki kutegemea dola ili iendelee kuwepo. Bure kabisa.
 

Wewe kuku mgeni?

Mbona anasema hayo kila siku?

Mswahili wewe!!!!
 


Mimi kwa mawazo yangu sasa naona Chadema wanajua kabisa wanataka nini. Ukiangalia vizuri Mbowe hana zile sifa za viongozi kuwa wasomi sana lakini ana vitu viwili vikubwa ambavyo Chadema ndiyo wanahitaji na ndiyo maana CCM itachukuwa muda sana kuelewa hili. Lissu pekee ndiye ameonekama yuko kama Mbowe kwa hayo hapo

1. Mbowe ni jasiri sana: Nitafutie kiongozi wa CCM ambaye amekaa jela hata week end moja na angalia makesi ya kusingiziwa ya mbowe yalivyo mengi.
2. Mbowe ana amini anachokisema. Hata kama anakosema Watanzania wanaheshimu watu wanaojiamini. Magu naye anajiamini hivyo watu wanajua hasemi au kufanya kwa siasa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…