Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Pascal alichofanya ni akili ya juu mno katika kujaribu kuasa wapiga kura.

Jee wapiga kura watakuwa hawajitambui na kuona kuwa katika mitikisiko ya kukiua chama hakikufa? Nani alipambana kisife wakati huo hadi sasa?

Na jee huyu mgeni ndani ya chama wa chini ya miaka 4 iweje aje na kufikiria kuwa yeye anauwezo wa kukamata nafasi ya juu kabisa ili kukiponya chama chake kipya dhidi ya chama chske cha zamani ambacho majuzi mwenyekiti wake amesema Mwambe anakipenda sana na alifanyiwa mizengwe tuu akaondoka?

Ni sawa na unataka kuoa mke aliyemuacha mumewe sio kwa vile hampendi bali gubu la mawifi ndio limemuondoa huko. Akikutana na mumewe wa zamani chocho basi ni mahaba "kama yote"

Andiko kuna walio lipokea tofauti kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu la maswali yako ni fupi sana. Watanzania tuna tatizo kubwa juu ya namna tunavyofikiri na tunavyoji 'behave'. CHADEMA' ni sehemu ya watanzania, kwa hiyo watakuwa na tatizo hilo kwa vyovyote vile.

Nini cha kufanya, watokee watu ambao interest yao sio vyeo bali kutengeneza misingi ya mabadiliko ya kijamii ya kimtizamo na kitabia, swali ni ikiwa watu hao tunao na wana uthubutu wa kufanya hivyo? Zaidi ya hapo haya mengine ushabiki tu usio na faida yoyote

Mkuu hao watu watatokea wapi, wakati hao wabovu ndio wako madarakani na ndio wanaoongoza vyama vya siasa, na wanafanya uhayawani wowote kuhakikisha wanabaki madarakani? Mkuu hebu anzisha chama chako chenye huo usahihi kisha uanze kupata uungwaji mkono uone kama utatoboa. Hayo natamani yako labda upindue nchi kisha uweke huo utaratibu kibabe, lakini sio kwa box la kura ambazo vyombo vya dola ni sehemu ya hujuma hizo.
 
CDM wanachotaka ni ruzuku tu ndo maana wapo tayari kushirikiana na yeyote anayewahakikishia hilo refer alichowaahidi Mamvi.

Nguvu sasa ni kupambana kubaki chama kikuu Cha upinzani kuelekea 2020 na Mbowe ana uzoefu na hilo he deserves.
Kuwa chama kikuu ni lazima uwe na wabunge wa kutosha

Nakuhakikishia 2020 Chadema haipati mbunge hata mmoja........ACT watapata kadhaa kule Pemba lakini siyo bara!
 
Mkuu usiwandanye!....kwa hali ya kisiasa Chadema imepitia kwa kipindi hiki...mtu sahihi ni mbowe....mbowe bado anahitajika sana Chadema hata kwa miaka kumi ijayo...siasa za sasa zinahitaji mtu mwenye roho ngumu na jasiri....na mtu huyo ni mbowe....kwa kifupi ukitaka kuua Chadema kwa kipindi hiki Muondoe Mbowe.
 
Pasco umefeli.

Unaleta kampeni huku jf, hawa mods kama wana akili huu uzi wataufuta, ila kama nao hawajitambui kama wewe watauacha!. Najua humpendi Mbowe toka jamaa yako wa kigoma alipofukuzwa uanachama. Huwezi kusema CDM hawajitambui kwa kuwa tu hawamuweki mtu unaemtaka wewe, wajumbe ni watu wazima wenye akili zao usiwafundishe cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakupongeza kwa justification uliyoitoa juu ya uhalali wa mwanachi asiyekuwa mwanachadema kukizungumzia chama hicho. Hata hivyo nimeshindwa kuelewa kwanini umeshindwa kujastifai umadhubuti wa Mwambe dhidi ya Udhaifu/mapungufu ya Mbowe katika kukiongoza chama hicho.
 
Mkuu, Paschal. Unaheshimiwa hapa jamvini. Hebu wakati wote uwe mkweli kwako kwanza, na kwa wasomaji hapa pili. Nasema kwako kwanza kwa sababu ukijitendea haki kwanza, kuna nafasi ya kuwatendea wengine pia. Tenda haki sasa na ukiri kuwa wewe ni mwanaCCM (hata kama kiitikadi). Kiri hilo moyoni mwako na tusonge mbele.

Ni kweli Chadema ni public organization, sawa na CCM na vyama vingine (kwa mujibu wa katiba). Pamoja na hilo, ni tu unapokuwa mwanachama wa chama husika ndipo unapata haki ulizotaja. Mfano mdogo, huwezi kugombea uongozi, kupiga au kupigiwa kura ndani ya chama cha siasa kama wewe si mwanachama wa chama hicho. Hii si sawa na kuhoji mambo ya serikali, kitu ambacho uraia tu wa jamhuri yetu unaweza kukupa haki hiyo hata kama si mwanachama wa chama cha siasa. Swala la kutaka kuhoji mambo ya Chadema kwa msingi wa "public entity" sio sahihi!! Hii sio governmental organization!

Ungependa kuona Cecil Mwambe anakuwa kiongozi wa Chadema. Kuna wengine wanapenda kuona Mbowe anakuwa kiongozi tena. Ni wewe huyu ni shabiki wa watu "kuunga juhudi za Magufuli". Ni wewe huyu unayesema Chadema inaelekea kufa. Ni wewe huyu uzungumzia viongozi waliojiuzulu kwa sababu wanaona hali ya kisiasa ya mbele imeegemea CCM na kwamba wako sahihi. Ni wewe huyu unaona vyama vya upinzani vimekosa mwelekeo na vitapotea. Katika yote hayo unayonesha, huwezi kuwa pia unatamani mabadiliko yaliyo chanya kwa Chadema. Unafahamu moyoni kuwa mabadiliko hasi ndiyo yatakayoupendeza moyo wako.

Naweza kuwa sifahamu kwa hakika Chadema wanataka nini lakini ninajua wamefahamu kiasi cha kutosha aina ya viongozi waliowahi kupitia Chadema na mambo yaliyotokea. Juliana Shonza, Sumaye, Amani Kaborou, Mwita, Lowassa, wabunge, viongozi na madiwani wengi waliowahi kuwa wanaCCM. Wengi wao walirejea CCM tena kwa mbwembwe nyingi za "narudi nyumbani". Je umejiuliza swali moja hapa? "Italeta picha gani mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani akiondoka na kurejea CCM?" Cecil Mwambe alikuwa CCM, ana doa linaloleta wasiwasi usioweza kuthibitishwa. Anaathiriwa na historia ya wenzake. Kama mgombea wa urais kupitia chama chao "anarejea", swali linakuja "ni nani mwingine hig-profile atafanya hivo?". Wasiwasi huu kwa wanachedema uko justified!!

Bora zimwi likujualo!! Na kama watafanya kosa tena, ni bora likafayika tena.
 
Pascal kwa nyuzi hizi siku chache zijazo tutakuona ukishika Biblia Takatifu mkono wako wa kuume ukitoa kiapo cha uaminifu mbele ya jiwe.
 
Umimaanisha wakimchagua Mwambe wamechagua maisha na wakimchagua Mbowe wamechagua kifo?

Hatuhitaji pandikizi tutamchagua tena huyohuyo mnaempiga vita.

Kwanini kila anaelaumu na kukosoa ni mpinzani wa chadema yameanzia lini mkaipenda chadema kwa kuwachagulia viongozi mnaotaka nyinyi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ulikiri hapa kuwa Baba yako na Mama yako walikuwa(ni) usalama wa taifa na kwamba wewe una mizizi ya uTISS.
Kwa hali ya sasa, kwa wenye kumbukumbu, ushauri wako ni kinyume. Mbowe anawakilisha uhai na Mwambe kifo cha chama.
 
Wewe ulikiri hapa kuwa Baba yako na Mama yako walikuwa(ni) usalama wa taifa na kwamba wewe una mizizi ya uTISS.
Kwa hali ya sasa, kwa wenye kumbukumbu, ushauri wako ni kinyume. Mbowe anawakilisha uhai na Mwambe kifo cha chama.
 
Kuwa chama kikuu ni lazima uwe na wabunge wa kutosha

Nakuhakikishia 2020 Chadema haipati mbunge hata mmoja........ACT watapata kadhaa kule Pemba lakini siyo bara!

Hawapati sio kwasababu hawana watu wa kuwapa kura za kutosha, ila ni kwakuwa rais hapa nchini ni Mungu na anaweza kuamua nani atangazwe mshindi. Kwa hiyo hapo huna la kujisifia kama ccm, bali sifia katiba mbovu inayoruhusu rais kufanya utashi wake kuwa ndio matakwa ya umma.
 
Back
Top Bottom