Naingiza milion 22 kwa mwezi kwa biashara ya kuuza Mapapai shambani

Nakufatilia kwa karibu kiongozi,. Tupe darasa kutokana na uhalisia
Hiyo bei jumla ukifikisha sokoni tena mbegu ya kisasa papai kubwa sana na siyo msimu wa papai nyingi za kienyeji.
Kiangazi kikuu ukitoa papai kubwa Sana utauza 1500 hadi 2000 bei ya jumla ukifika sokoni kwa dalali.
Hapo bado dalali hajakusokota, pia kuna ushuru, usafiri na ulinzi.
 
Kitu kingine gharama za umwagiliaji siyo ndogo, Mbolea ya samadi yakutosha muhimu.
Ukiweza vitu hivyo viwili utavuna papai la pesa utafurahia kilimo.
 
Oukay,. Nimekupata kiongozi
Shukrani🙏
 
Soko mtaani ndo linakupa MILLION 22 ....Nipe location afandee
 
Kilimo cha mitandaoni hicho.
Kilimo halisi huwezi kuuza papai likiwa shambani kwa 1500/- labda shamba lako lipo pale Sokoni Kisutu au Ilala au Kariakoo au Mabibo.
Mimi nilipanda mipapai miche 700 mbegu ya kisasa Malikia F1. Naongea nikiwa na uzoefu.
tupe update mkuu
 
Muda WA wewe kuwa na hela umefika ndio maana kilichokutoa unahisi pekee kiko sahihi Ila nikikwambia kuna watu wamepoteza pesa zao Kwa haya haya mapapai unaweza shangaa! All in all hongera Kwa ushuhuda mzuri
 
Ni
Nina mipapai20 hapa Dodoma nitapata sh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…