Organisation ndani ya Chadema imepungua, Mbowe yuko jela, Lema na Lissu wakiwa kama viongozi ndani ya chama nao hawapo nchini, sasa amebaki KM peke yake mzigo wote unamuelemea, ndio maana ameanza kuonekana hatoshi.
Lazima itafutwe namna hawa watu waliokimbia nchi warudi, ama sivyo, wajipange upya;
- Lissu adui yake mkubwa alikuwa ni Magufuli, na ndio alisema alikuwa anatoa maelekezo afanyiwe unyama, now Magufuli is gone, bahati mbaya Samia nae haaminiki, ushauri wa wasaidizi wake anauchukua kama ulivyo.
- Lema alikimbia kesi ya kubambikiwa, Samia akasema hataki watu waonewe tena, baada ya muda mfupi tunamuona Mbowe anabambikiwa kesi, hapa napo Samia haaminiki.
Lissu na Lema wanaweza kuendelea kuwepo nje ya nchi kwa muda mrefu zaidi, Chadema lazima wajipange upya kukabiliana na hali hii inayowakuta.
Kikao cha Samia na upinzani (Chadema ikiwepo) kingemaliza hii hali mapema sana, but Mbowe kuwa gerezani maana yake hicho kikao sidhani kama kitakuwepo tena, na yale majibu ya Samia kwenye interview ya BBC ndio yanakatisha tamaa kabisa.
Chadema sasa watafute njia za kujipanga, video conferencing inaweza kutumika, sio kushinda twitter day and night; wajue namna mpya ya kukabiliana na CCM inayobebwa mgongoni na jeshi la polisi ili kuendana na hali ya kisiasa nchini inayowakuta kwa sasa.
Kwenda makanisani na uniform za chama hiyo strategy sijaipenda, nyumba za ibada ziheshimiwe, CCM wakikosea Chadema wasirudie kosa la CCM, watachafuliwa na tope la CCM mwishowe wafanane na CCM halafu wananchi wakose namna ya kuwatofautisha iwe faida kwa CCM, Chadema wanatakiwa kwenda three steps ahead of CCM kama walivyokuwa wakifanya.
I repeat, organisation is needed ndani ya Chadema, they have to re-group to find new ways and means, Chadema haifi, lakini wasipokuwa makini itadumaa.