Naiona failure ya CHADEMA kwa Mbaali japo ni wabishi

Naiona failure ya CHADEMA kwa Mbaali japo ni wabishi

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wewe dada huwa una mikwara sana!

Hii mikwara yako si uwe unaenda nayo pale Central?
Kasikutishe hako bwana tunajua hiyo ni kawaida yao kutaka kutuaminisha kwamba wanajua kila kitu
 
pesa haishindwi mbowe anakesi ya kufadhiri ugaidi moja ya ugaidi ni huo kufadhiri walinzi wasiwepo eneo la kazi ili watu wa mbowe wafanye yao wa lissu
Utaonyesha busara zaidi kama utapeleka ushahidi na vielelezo vyako kwenye vyombo vya dola ili kuwasaidia Polisi wapate nguvu ya kulimaliza swala hilo. Sasa huna tofauti na mjukuu wa shetani wa kule kwenu.
 
Organisation ndani ya Chadema imepungua, Mbowe yuko jela, Lema na Lissu wakiwa kama viongozi ndani ya chama nao hawapo nchini, sasa amebaki KM peke yake mzigo wote unamuelemea, ndio maana ameanza kuonekana hatoshi.

Lazima itafutwe namna hawa watu waliokimbia nchi warudi, ama sivyo, wajipange upya;

- Lissu adui yake mkubwa alikuwa ni Magufuli, na ndio alisema alikuwa anatoa maelekezo afanyiwe unyama, now Magufuli is gone, bahati mbaya Samia nae haaminiki, ushauri wa wasaidizi wake anauchukua kama ulivyo.

- Lema alikimbia kesi ya kubambikiwa, Samia akasema hataki watu waonewe tena, baada ya muda mfupi tunamuona Mbowe anabambikiwa kesi, hapa napo Samia haaminiki.

Lissu na Lema wanaweza kuendelea kuwepo nje ya nchi kwa muda mrefu zaidi, Chadema lazima wajipange upya kukabiliana na hali hii inayowakuta.

Kikao cha Samia na upinzani (Chadema ikiwepo) kingemaliza hii hali mapema sana, but Mbowe kuwa gerezani maana yake hicho kikao sidhani kama kitakuwepo tena, na yale majibu ya Samia kwenye interview ya BBC ndio yanakatisha tamaa kabisa.

Chadema sasa watafute njia za kujipanga, video conferencing inaweza kutumika, sio kushinda twitter day and night; wajue namna mpya ya kukabiliana na CCM inayobebwa mgongoni na jeshi la polisi ili kuendana na hali ya kisiasa nchini inayowakuta kwa sasa.

Kwenda makanisani na uniform za chama hiyo strategy sijaipenda, nyumba za ibada ziheshimiwe, CCM wakikosea Chadema wasirudie kosa la CCM, watachafuliwa na tope la CCM mwishowe wafanane na CCM halafu wananchi wakose namna ya kuwatofautisha iwe faida kwa CCM, Chadema wanatakiwa kwenda three steps ahead of CCM kama walivyokuwa wakifanya.

I repeat, organisation is needed ndani ya Chadema, they have to re-group to find new ways and means, Chadema haifi, lakini wasipokuwa makini itadumaa.
Tatizo ninyi mwafahamu kila kitu mkishauriwa hata kwa nia njema mnajibu tu bila kutafakari kwanza.

Mimi pia nimewashauri humu mtafute strategists wawasaidie hilo pia linawashinda.
 
Utaonyesha busara zaidi kama utapeleka ushahidi na vielelezo vyako kwenye vyombo vya dola ili kuwasaidia Polisi wapate nguvu ya kulimaliza swala hilo. Sasa huna tofauti na mjukuu wa shetani wa kule kwenu.
KILA kitu kinajulikana subirini kesi ianze mtaficha wapi sijui sura zenu
 
Ni siku zaidi ya 20 ambayo Mwenyekiti wa CHADEMA yupo jela bila kuonesha actions za maana

1. Nimeshangaa sana Godbless Lema anamlaumu Bob Wine wa Uganda kutolaumu serikali ya Samia kwa sakata la Mbowe nimejiuliza maswali mengi sana are we serious?

2. Press ya awali ya Mnyika ilinipa picha kwamba hakuna matumaini yeyote juu ya mipango wanayosema

3. Sasa hivi ndani ya Chama wamegawanyika sana!

4. Lissu anogopa Kwenda Tanzania kuhamasisha mabadiliko on ground anaishia kumtuma bwana Godfrey Rwehumbiza wa Bangkok amuombee msamaha kwa Samia na kufutiwa mashtaka Yaan anajinasua mwenyewe tu!! Huyu Rwehumbiza Ana act kama Balozi wa Tanzania nchini Thailand anakaa Soi 7 Sukhumvit road Thonglou. Japo Tanzania tunapata Visa za Thailand kupitia Kenya ila Rwehumbiza ndio anafanya uwakilishi wa mambo kadhaaa

3. Vijana wa CHADEMA hawana kinachoendelea zaidi ya BAWACHA ndio wanafanya kazi kubwa!!! Wao wenyewe wanazungukana! Walikubaliana woote waliokamatwa Mwanza wasikubali dhamana ila John Pambalu baada ya kutishiwa na mtuhumiwa pale Central kwa kutoa uume wake na kumtisha kwamba njoo tulale akapiga kelele asubuhi Anaomba dhamana !

4. LISSU anabeza sana mawazo ya wengine aliona kwamba yeye mawazo yake ndio alpha na Omega Kuna matatizo

Britanicca
Britanicca, umenisikitisha sana maana sikutegemea uandike vitu kama hivi. Unadhani kuna mtu anapenda kuwa njee ya nch yake? Lisu is right kutetea maisha yake. Haya ya Pambalu uliyashuhudia? Nimeanza ku doubt credibility yako. Hii ni nchi ya ki dicteita, sidhani kama ni busara kuwa dead hero. Wapigania uhuru mara nyingi wanakimbia nchi maisha yao yanapokuwa hatarini. I was in Uganda during Idd Amin era, people were dying like hell! Waganda ni jeuri sana, lkn kwa mauaji yale wengi walikimbia. Hivyo lazima kutetea maisha kwanza kabla ya kujitoa mhanga
 
Kuna jinga moja lilinifanya niende jela ya hapa jf

Alafu kuna mods humu wana vimihemuko balaa, ukitoa coment inayochoma moyo wake wa kisiasa unashangaa anabonyeza kitufe cha ban
[emoji23][emoji23][emoji23]
🤣🤣 Kuna ma-dikteta chipukizi vimejificha kwenye kichaka cha u-mod
 
Kuanzia awamu ya 5, CCM/dola imeshachukua hatua zote kuhakikisha CHADEMA hawatafanya kazi tena kama chama cha siasa. Kiuhalisia, CHADEMA inachukuliwa kama kikundi cha ugaidi. Ajenda kuu ya TISS, polisi, n.k. ni kufuatilia nyendo zote za viongozi na makada muhimu wa CHADEMA na kuwavurugia iwe kisheria au hata nje ya sheria. Wanaoweza kununuliwa wanachomolewa. Wanaoweza kupotezwa (neutralised) wanapotezwa.

Leo hii mtu “cool” kama Mbowe anafunguliwa kesi ya ugaidi? Tena enzi za SSH? Halafu bado wapo wanaofikiri uimara wa CHADEMA utategemea kuja na “mikakati bora” ya kuendesha chama! Kwa kifupi, hakuna mkakati wa kioganaizesheni, kisiasa, kiuchumi, n.k. unaoweza kuisadia CHADEMA kuimarika zaidi ya ilipofikia. Ukisoma comments za wapambe wa CCM/serikali hapa JF ndipo utaliona jibu sahihi.

Wanawacheka CHADEMA kwa kutoitikia wito wa Lissu wa kuandamana au wito wa kuendelea na mikutano ya katiba licha ya polisi kuzuia. Wanawacheka kwa “kutolianzisha” ili kumtoa mwenyekiti wao jela badala ya kulialia tu kwenye mitandao.

Nionavyo, ni mpaka siku ajenda/hoja za CHADEMA zitakapoeleweka kwa wananchi wengi hadi kuamua “kulianzisha kiroho mbaya” ndipo CCM/dola itakapolazimika kuacha ujinga na kustaarabika. Hizi mada za mikakati ya CHADEMA zinaanzishwa na wanapropaganda wa CCM/dola ili kukebehi na kubeza chama hicho na kuwachanganya wanachama na mashabiki wake.
Ukisema hakuna mikakati mipya ya kuinyanyua Chadema kwasababu CCM na polisi wanatumia kila aina ya mbinu kuwakandamiza maana yake unakubali Chadema ife au idumae, haya mawazo yako ni sumu kwa maendeleo ya chama.

Leo nimeona Pambalu anasema makongamano ya Katiba Mpya yanaendelea mkoa wa Mara licha ya Mbowe kuwa gerezani, hii ndio mojawapo ya mbinu mpya, never look back, kama CCM walidhani kumkamata Mbowe ndio wamemaliza mchezo wamefeli.

Ukisubiri ajenda za Chadema zieleweke kwa wananchi ili wananchi "walianzishe" nayo ni maneno ya kujifariji tu, utasubiri mpaka lini? upo tayari kulianzisha?Chadema ina miaka zaidi ya ishirini tangu ianzishwe, kama mpaka leo haijaeleweka kwa wananchi, utasubiri miaka mingine mingapi?
 
Wengi waliosema Chadema itakufa wamekufa, akiwemo jiwe aliyekuwa anakulipa na ukifanya mchezo tutaweka hadharani akaunti ya NMB uliyokuwa unaingiziwa pesa wewe na mamluki wenzio kabla hujatemwa.
Du!!! Kumbe alikua ana ingiziwa
 
Nmejifunza hapa jf ukiwa na siasa za misimamo mikali kama alshabab utapigwa ban kila siku

[emoji23][emoji23][emoji23]

Sio kweli, bendera fuata upepo huo sio msimamo. Labda unaongelea kitu kingine lakini sio msimamo.
 
Ungesema tu lengo la post yako ni kumchafua Lissu. Umetumwa na yule Lissu alimuita MJINGA? Maana naskia kajiapiza "kummaliza Lissu" (clue: he won't and can't).
Wewe ni tapeli wa kimataifa ukirudi bongo kabla wajomba awajakudaka lazima tukupakate ukalie rungu
 
nimejiuliza maswali mengi sana are we serious?
Sasa hivi ndani ya Chama wamegawanyika sana!.
LISSU anabeza sana mawazo ya wengine aliona kwamba yeye mawazo yake ndio alpha na Omega Kuna matatizo

Britanicca
Mkuu britanicca, haya wewe ndio unayaona leo?!. These people have never been serious hata kidogo!. Wangekuwa serious saa hizi siku nyingi wangekuwa Ikulu!. Angalia hapa niliwashauri nini na lini, wangeufuata ushauri huu, saa hizi wangekuwa Ikulu!.
P
 
Mkuu britanicca, haya wewe ndio unayaona leo?!. These people have never been serious hata kidogo!. Wangekuwa serious saa hizi siku nyingi wangekuwa Ikulu!. Angalia hapa niliwashauri nini na lini, wangeufuata ushauri huu, saa hizi wangekuwa Ikulu!.
P

Kawe ulipata kura moja,jishauri kwanza wewe mwenyewe ilikuwaje.
 
Chadema hawana Sera inayogusa watanzania wote zaidi ya mambo yao ya kupata madaraka tu.

Kuna wanaharakati huru waliojitolea kujenga uelewa kwa watanzania na kujua madhaifu na maovu ya serikali jambo lililopelekea watanzania wengi kuanza kujielewa.
Mfano Kigogo wa kwenye Twitter.
Mange Kimambi.
Maria Sarungi.
Shangazi Fatma Karume.
Tobias Marandu n.k.
Paskali Mayalla na wengine.

Chadema kwa sababu ya siasa zisizo na ulekea wakadhani kuwa wanaporwa umaarufu wao na kuanza kuruka ruka na agenda za wanaharakati.

Ni kosa kubwa sana kurukia kila agenda na kujibu kwa kukurupuka ushauri au tamko la wanaharakati.
Wanaharakati ni watu wenye kipaji hicho hivyo inapaswa kuwaheshimu na kuwapa nafasi yao ya kushauri au kukosoa sio kuwachukulia kama wanasiasa wanaosaka madaraka.

Kigogo Leo anaonekana ni adui mkubwa na kujaribu hata kumtaja jina . Ni jambo baya sana. Je, hao Chadema wakiingia Ikulu watawachukuliaje hao wanaharakati kama wanashindwa kuwaelewa leo.?
Siasa na harakati zinafanywa kwa tahadhari kubwa sana sio kama Chadema wanavyodandia dandia .


Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kawe ulipata kura moja,jishauri kwanza wewe mwenyewe ilikuwaje.
Mkuu Ngongo , kwanza ni kweli, niligombea kuteuliwa Kawe kupitia CCM, na nilipata kura moja, na baada ya uchaguzi ule, sio tuu nilijishauri, bali pia nilitoa ombi maalum humu jf kwa wana jf wenzangu,

Hivyo huku kila siku kurudia rudia ulipata kura moja, ni kama kunisimanga!.
Please!. Japo nilipata kura moja, lakini ugombea ule umeisaidia sana jf, mimi Pasco Mayalla as a verified member wa jf, mimi ndie member wa kwanza wa jf, to be officially recognized by JF kama kada wa kwanza wa CCM kuwa jf member. This is good to jf, kama kada wa CCM anaweza kuwa member wa jf, hii inaamisha jf ni mtandao safi wa watu wote, vyama vyote na hata wasio na vyama. Kabla ya ule utambulisho wangu mpya wa "Pasco Mayalla ni kada wa CCM", kuna members humu wa chama fulani, walitamalaki humu kupita kiasi na kuufanya huu mtandao wa jf, kuonekana kama ni mtandao wao, hivyo sasa nime neutralize, JF ni mtandao wa wote. Isn't this good?
P
 
Chademaa hawajawahi kuwa serious, watu wao walipopoteza ubunge ndio wakaanza visa kwasababu wamekosa "ulaji".

Wanakosa ajenda na mipango ya kimkakati, wakae watambue kuitoa CCM kunahitaji mikakati ya kweli.
 
Chademaa hawajawahi kuwa serious, watu wao walipopoteza ubunge ndio wakaanza visa kwasababu wamekosa "ulaji".

Wanakosa ajenda na mipango ya kimkakati, wakae watambue kuitoa CCM kunahitaji mikakati ya kweli.
Kama Ile ya kwenye chafuzi za wanakijani sio?
 
Back
Top Bottom