Former Israel Prime Minister Ehud Barak lands in Tanzania’s northern tourist circuit
WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TAIFA LA ISRAEL,EHUD BARAK ATEMBELEA SERENGETI NA NGORONGORO.
Na Dixon Busagaga,Arusha.
WAZIRI mkuu mstaafu wa Taifa la Israel, Ehud Barak amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo huku akieleza kuwa eneo la bonde la Olduvai Gorege ni muhimu kama makutano baina ya kizazi cha binadamu wa kwanza na binadamu wa sasa.
Barak aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo la kumbukumbu ya Binadamu lililopo katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro akielekea Hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa ziara ya utalii.
Akiwa ameongozana familia yake na ujumbe wa watalii zaidi ya 100 kutoka nchini Israel kiongozi huyo wa zamani wa taifa la Israel ameoneshwa kuridhishwa na namna Tanzania inavyo toa kipaumbele katika kuhifadhi rasilimali zake za kitalii.
Ehud Barak pia amepata nafasi ya kuweka saini katika kitabu cha wageni kabla ya kuanza kutembelea eneo la makumbusho huku Mhandisi Ramo Makani akionesha matumaini ya kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka nchini Israel.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete ametoa mwito kwa watanzania kujenga Uzalendo wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.
Ehud Barack amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Israel kati ta mwaka 1999 na 2001 na baadae Waziri wa Ulinzi wa Isael kati ya mwaka 2007 na 2013 kabla ya kustaafu.
View attachment 496505 View attachment 496506 View attachment 496507