Naishauri Serikali isiwatumie ambao sio watumishi kwenye sensa, maeneo mengi wameharibu kazi na hakuna njia ya kuwajibisha

Naishauri serikali isiwatumie watu ambao sio watumishi wa umma Kwenye zoezi la sensa na sababu ni hizi.
1. Wengi wanaomba maeneo ambayo hawayajui hivyo wanalipua ili wawahi kuondoka mfano mtu anakaa dar es salaam anaomba kazi ya sensa matombo hapa atalipuwa ili amalize haraka aondoke.
2. Watumishi wenu wa umma wao wanafungwa na kanuni za kiutumishi kuwa watiifu hata akiharibu ipo namna ya kumwajibisha.
3. Watumishi wengi wako Kwenye maeneo yao ya kazi (within localities) hivyo kuongeza tija ya kazi ubora na ufanisi.
4. Kuna maeneo sensa ya makazi wameharibu kwasababu wamepewa kazi kwa kujuana na mabosi wa halmashauri walipoharibu wakatumwa walimu warudie tena bila malipo yoyote msipowafikiria hawa kazi ikiharibika tena itatafsirika mnaihujumu serikali makusudi.
Kazi kubwa maslah madogo hukaribisha tamaa.Hata hao watumishi wa serikali wapo wasiyowaaminifu.Kwani ufisadi unaotokea serikalini unaletwa na hawa wasiyoajiriwa na serikali?
 
Wanatetea eti wanawapa ajira. Wanatest kwenye professional career Ili kazi ziharibike, hili unaweza ukaliona kwenye chaguzi... Wanaofanyia mpaka jeshi letu lihangaike kulinda raia ambaye hana hofu na kujali ubora wa kazi.
 
Naishauri serikali isiwatumie watu ambao sio watumishi wa umma Kwenye zoezi la sensa na sababu ni hizi.
1. Wengi wanaomba maeneo ambayo hawayajui hivyo wanalipua ili wawahi kuondoka mfano mtu anakaa dar es salaam anaomba kazi ya sensa matombo hapa atalipuwa ili amalize haraka aondoke.
2. Watumishi wenu wa umma wao wanafungwa na kanuni za kiutumishi kuwa watiifu hata akiharibu ipo namna ya kumwajibisha.
3. Watumishi wengi wako Kwenye maeneo yao ya kazi (within localities) hivyo kuongeza tija ya kazi ubora na ufanisi.
4. Kuna maeneo sensa ya makazi wameharibu kwasababu wamepewa kazi kwa kujuana na mabosi wa halmashauri walipoharibu wakatumwa walimu warudie tena bila malipo yoyote msipowafikiria hawa kazi ikiharibika tena itatafsirika mnaihujumu serikali makusudi.
Naunga mkono hoja..na mtumishi lazima awe na digrii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkishabahatika kupata ajira Serikalini mnajikuta sanaa mnasahau kila kitu.
 
Kutoka dakawa mpaka Morogoro mjini ni kama km 30 akishahesabu amechoka anawaza kupanda hiace arudi morogoro mjini akale kuku kwa hela ya sensa huku kazi ameharibu acheni utani na mambo ya msingi.
Kwani we unadhani wanahesabu watu kama nyanya sokoni!?? Ndio maana kuna semina elekezi kabla hawajakabidhiwa majukumu yao.
 
WAALIMU WANA HALI NGUMU SANA.

HADI KUSIMAMIA MITIHANI NA KUSAHIHISHA HUWA MNAROGANA.
Jf bwana, unaweza kukuta Huyu ni mtoto WA kufikia WA mwalimu na anaishi Kwa hisani ya mwalimu mpaka bando anapata kutoka Kwa huyo baba'ake mwalimu. Na siajabu mama yake alitumia muda na nguvu kweli kumuwinda huyo mwalimu ili apate hifadhi na huyu mtoto wake. Leo, akijua hajulikani humu, anamtukana Baba yake muhifadhi. Laana Sana hii!
 
Tunazungumzia uzoefu wa wadau kwenye sensa ya makazi
Lini mtaa haukujazwa? Na nyumba zilijazwa sijui, sijui sijui maana yake Nini? Kwani sensa imeshafanyika? Mbona una wasiwasi? Sensa inafanyika mwezi was nane au nadangaya ndugu zangu?
 
Jamani jamani watumishi chonde chonde juzi tu mmeongezewa mshahara, na za sensa mnazitaka mweee!!.. unatakwimu za kutosha kuwa hao watumishi Huwa hawaaribu kazi??... Hao watu wa takwimu si wameweka utaratibu wao wa namna ya kusimamia kazi, maana yake wanaokuwa wameharibu kazi ni watu wa takwimu
 
Inaonyesha wengi mnaotetea ujinger ni applicants wa aina hiyo lakini naamini wakifwata ushauri wengi watashuhudia mengi.
 
Kwanza kumbuka hizi kazi unakuwa mdhamini anayeaminika na unapokuwa kwenye majukumu pia unakuwa na viongozi wa NBS sasa kama hawatahakikisha umetimiza kile ulichopangiwa basi wao NBS ndio watakuwa wazembe.

Watumishi mngebaki tuu na majukumu ya siku zote kwani baadhi yenu hata hamuwajibiki ipasavyo hivyo msitafute sababu ya kuja kuharibu zaidi uwajibikaji wenu katika kipindi cha zoezi hili la sensa.
 
Weee Ndio unaongea ujinga, hao walimu huo ufanisi umeuona kwenye shule za serikali? Au unatetea tumbo?? Kwani hivyo taasisi ya takwimu haiwezi kuweka Sheria za kuwabana na wakasimamia vizuri nini kinashindikana? Eti wakiharibu kazi namna ya kuwawajibisha ni ngumu, ugumu unatoka wapi, wamejaza taarifa zao unashindwaje kuwadaka na Sheria kuchukua mkondo wake? Ukiona kuna uharibifu uzembe umeanzia huko huko juu
 
Acha kuwafundisha kazi NBS, we jamaa, kwanza umesomea kozi gani wewe. Tangazo lipo wazi, limesema linataka watu wa statistics, Economics na Kz. Sasa wewe unaweka kigezo cha utumishi. Akili zako zichunguze vizuri.
 
Kwanza kumbuka hizi kazi unakuwa mdhamini anayeaminika na unapokuwa kwenye majukumu pia unakuwa na viongozi wa NBS sasa kama hawatahakikisha umetimiza kile ulichopangiwa basi wao NBS ndio watakuwa wazembe.

Watumishi mngebaki tuu na majukumu ya siku zote kwani baadhi yenu hata hamuwajibiki ipasavyo hivyo msitafute sababu ya kuja kuharibu zaidi uwajibikaji wenu katika kipindi cha zoezi hili la sensa.
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom