Naishauri serikali Kesho isije Ikatumia mabavu, iache CHADEMA wafanye maandamano yao kwa Amani

Naishauri serikali Kesho isije Ikatumia mabavu, iache CHADEMA wafanye maandamano yao kwa Amani

Sitaki watu waumie hasa wanyonge
Tupo pamoja sana katika hilo; lakini inawezekana tukawa tofauti kwenye 'details' za namna hao "wanyonge" wanavyoweza kuondokana na hali ya "maumivu" inayo wakabili.

Wakati mwingini "maumivu" hayaepukiki wakati njia za kuyaondoa zikitumika. Sawa na mambo mengineyo, kama kutibu magonjwa, n.k., n.k..
 
Changamoto ni kuwa huenda wananchi wengi wamechagua kutawaliwa na serikali isiyojali maisha na uhai wa watu wake(wachache)
Ndio maana nikasema hali kama hii huweza kupelekea nchi kupasuka vipande vipande
 
Hapana.
Hii ni dhana tusiyoweza kukubaliana hata kidogo.
Hakuna nchi yoyote duniani ambayo wananchi wake wengi "wanachagua kutawaliwa na serikali isiyo jali maisha na uhai wa watu wake". Maneno haya sijui kwa nini umeyatumia.

Linalo julikana bila wasiwasi wowote, duniani kote na katika nchi zote, ni watu "wachache" wanao jitokeza mbele na kukataa yanayofanywa na watawala. Hao wengi huwa wanafuata tu matokeo ya mampambano ya hao wachache.

Usitegemee hata mara moja kukuta waTanzania asili mia 70 wakishiriki kwa pamoja kutafuta mageuzi ndani ya nchi yao.
Acha hawa wachache watimize wajibu wao.
 
Tukienda kwenye sanduku la Kura Watanzania wengi huchagua CCM

Mwaka 2020 nilijitahidi kuzunguka mikoa mitatu ndani ya siku moja nikajionea jinsi CCM inavyopewa nafasi hasa kwenye nafasi ya Urais.

Sizungumzii kupendelea chama chochote
 
Mkuu, ni vizuri kusoma maandiko yako; lakini wakati mwingine yana chekesha kidogo hata kama ni kuhusu mambo yasiyo hitaji kucheka.

Simama upande wa hao hao unao wasema humu, na jaribu kujua msukumo unao wafanya wafanye haya. Ni dhahiri kuna mambo wanayaogopa na wanajaribu kuzuia kwa kila njia yasitokee.

Hawa siku nyingi wame faidika na njia hizo hizo za mabavu. Nafasi wanazo shikilia sasa hivi ni matokeo ya mabavu hayo hayo wanayo jaribu kuyatumia, bila ya kujali kama safari hii yataendelea kuwa hakikishia mafanikio yale yale.

Njia hizo zimefanikiwa, hadi sasa, lakini kumeanza kuonekana usugu kwa hao wanao tishiwa; kwamba liwalo na liwe na wawo hawatarudi nyuma. Hali ndiyo hiyo sasa
'Who is going to blink'?
Wewe Baba yako au Mtoto wako ndio
angekuwa ameuawa au kutekwa na hajulikani
alipo usingeandamana?
Yaani assume hao watoto wako ambao wako
salama au huyo Babaako unayempenda
aliyesalama angetokea mtu akamuua kwa
kifo cha kikatili au akatekwa
usingeandamana?
Au fikiria wewe ndio umeuawa, au umetekwa
uko matekani kwa watesi wako. Alafu
ukasikia watoto na watu wanaandamana
kwaajili yako ungejisikiaje? Ungewachukuliaje
Wananchi wenzako?
Ungeionaje nchi yako?

Umesema vyema. Haya jibu hayo maswali.
 
Tukienda kwenye sanduku la Kura Watanzania wengi huchagua CCM

Mwaka 2020 nilijitahidi kuzunguka mikoa mitatu ndani ya siku moja nikajionea jinsi CCM inavyopewa nafasi hasa kwenye nafasi ya Urais.

Sizungumzii kupendelea chama chochote
Huko kuzunguka kwako siyo sampuli sahihi ya Kisayansi katika maswala hayo; kwa hiyo hilo ninakuomba uliweke pembeni, kwa sababu linaku egemeza kwenye nguzo ya kishabiki hata bila kutambua unafanya hivyo.

Unapozungumzia kwenda kwenye sanduku la kura 2020 (pamoja na kutokubaliana nawe katika hitimisho ulilo fanya); hiyo ni miaka takribani mitano iliyo pita, tena katika mazingira tofauti sana na yaliyopo sasa. Utapata wapi ujasiri wa kusema CCM inakubalika leo kama waTanzania walivyo kubali pengine kazi za kiongozi mmoja wa wakati huo; halafu ulete picha hiyo hiyo katika mazingira ya leo, wakati huko CCM kwenyewe kumebadilika sana chini ya kiongozi mwingine?

Haya unayo yaona leo ya vitisho vingi kiasi hiki, hayakupi picha ya kujua hofu ya viongozi hawa inatokea wapi?
 
Wewe Baba yako au Mtoto wako ndio
angekuwa ameuawa au kutekwa na hajulikani
alipo usingeandamana?
Yaani assume hao watoto wako ambao wako
salama au huyo Babaako unayempenda
aliyesalama angetokea mtu akamuua kwa
kifo cha kikatili au akatekwa
usingeandamana?
Au fikiria wewe ndio umeuawa, au umetekwa
uko matekani kwa watesi wako. Alafu
ukasikia watoto na watu wanaandamana
kwaajili yako ungejisikiaje? Ungewachukuliaje
Wananchi wenzako?
Ungeionaje nchi yako?

Umesema vyema. Haya jibu hayo maswali.
Nimeshindwa kuchagua kati ya alama ya mshangao au kusikitika.
 
Ndio maana Mimi sijayapinga na nimeishauro serikali nini chakufanya, kutoa HAKI

Ila Maandamano yanayohamasisha kuangushwa kwa serikali hayo napinga kwa sababu hayapo kisheria. Yaani sidhani kama kuna sheria inaruhusu serikali kuangushwa kwa maandamano.

Kama Samia hafai Mwakani sio mbali, wapige Kura. Kama atashindwa sawa. Kama atashinda sawa. Kama ataiba kura hiyo tutaipinga. Kama mpinzani atashinda kwa kuiba kura tutaipinga

..hata " Samia Must Go " haina tatizo.

..tujiulize ni sheria gani inayokataza kusema hivyo.

..mara nyingi Chadema wamesikika wakisema wanataka kuitoa Ccm madarakani. Mbona kauli hiyo haijawahi kuleta shida yoyote?

..ilimradi Chadema hawajasema watatumia njia haramu kumuondoa Samia madarakani hakuna makosa ktk kauli mbiu yao.
 
Waachwe wafanye maandamano ya "Samia must go"? Hakuna anayeshabikia maandamano ya vurugu
 
..hata " Samia Must Go " haina tatizo.

..tujiulize ni sheria gani inayokataza kusema hivyo.

..mara nyingi Chadema wamesikika wakisema wanataka kuitoa Ccm madarakani. Mbona kauli hiyo haijawahi kuleta shida yoyote?

..ilimradi Chadema hawajasema watatumia njia haramu kumuondoa Samia madarakani hakuna makosa ktk kauli mbiu yao.

Kikawaida Maandamano ni njia ambayo inatumika baada ya mazungumzo ya kawaida kushindikana.

Samia Must Go ingekuwa wakati wa uchaguzi yaani Mwakani ingekuwa na Mantiki kwa sababu ni wakati sahihi ambapo chama chochote hata CCM yenyewe inaweza kuitumia hiyo Kauli mbiu ya Samia Must Goo kama hawajamkubali Mwenyekiti wao. Lakini kwa Sasa Kauli hiyo sio sahihi kabisa.

Ni kutaka kuiangusha serikali ya Samia ambayo tunajua kuwa mpaka dakika hii ni serikali Halali hata kama ingekuwa inafanya mambo haramu
 
Huko kuzunguka kwako siyo sampuli sahihi ya Kisayansi katika maswala hayo; kwa hiyo hilo ninakuomba uliweke pembeni, kwa sababu linaku egemeza kwenye nguzo ya kishabiki hata bila kutambua unafanya hivyo.

Unapozungumzia kwenda kwenye sanduku la kura 2020 (pamoja na kutokubaliana nawe katika hitimisho ulilo fanya); hiyo ni miaka takribani mitano iliyo pita, tena katika mazingira tofauti sana na yaliyopo sasa. Utapata wapi ujasiri wa kusema CCM inakubalika leo kama waTanzania walivyo kubali pengine kazi za kiongozi mmoja wa wakati huo; halafu ulete picha hiyo hiyo katika mazingira ya leo, wakati huko CCM kwenyewe kumebadilika sana chini ya kiongozi mwingine?

Haya unayo yaona leo ya vitisho vingi kiasi hiki, hayakupi picha ya kujua hofu ya viongozi hawa inatokea wapi?

Mkuu serikali ya CCM kikawaida ni serikali ya vitisho. Ajabu ni kuwa Watanzania wengi ndio wanapenda serikali za namna hiyo.

Ushahidi wa hili tuliona kwenye serikali ya Magufuli, Moja ya mambo yaliyofanya Jpm apendwe ni aina ya siasa zake za vitisho mbali na uchapakazi wake.

Watanzania wengi ni watu wa aina ya ajabu sana. Usipotumia vitisho wao huamini kuwa huwezi kuongoza.

Embu Muangalie Makonda, siasa za Makonda zinapendwa na Watanzania wengi ukichunguza kwa undani utagundua sababu ni kufanya siasa za vitisho na Ubabe.

Watanzania wengi ni kama wanyama yaani hawana utashi wenye afya. Sio ajabu hupenda Kuona siasa za vitisho au pengine ni athari za kisaikolojia walizozipata.

Juzi tuu hapa Rais Samia alitoa hotuba ambayo kwa sisi wengine tuliona ametoa Boko kwa sababu hotuba Ile iliandikwa na kusomwa kwa hisia Kali huku akili iliyotulia ikitumika kidogo.
Lakini Mimi nilifuatilia mitandaoni nikaona Watanzania wakijaribu kumpongeza Ati kuwa ameanza kuwa kama JPM. Na wakaonyesha tumaini la kumkubali
 
Back
Top Bottom