Naishi kwenye Nyumba ya kupanga mwenye nyumba alifariki ghafla na ndugu hawaijui hii nyumba

Naishi kwenye Nyumba ya kupanga mwenye nyumba alifariki ghafla na ndugu hawaijui hii nyumba

Daah tatizo mkuu hapa mjini shida kuwatambua ndugu wanaweza kujitokeza matapeli sababu jamaa tulikutana nae bar akasema anajenga akimaliza Mimi nihamie kama mpangaji wake Nikalipia miezi 6 ndio mwezi wa 4 akafariki

Kama una namba ya simu ya jamaa, ukitumia hiyo namba tu, utapata mpaka anapoishi na mtaa, kama una nia hiyo. Na hata ndugu zake utawapata. Tafuta familia yake wape nyumba na kiwanja chao, fanya ujanja ujanja ulaaniwe wewe na kizazi chako. Nyumba haiokotwi.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb

Sasa mzee Mimi kwani ndio nimeua mpaka useme nipate laana
 
Sasa mzee Mimi kwani ndio nimeua mpaka useme nipate laana
Hujaua, lakini unapotaka kujimilikisha kitu ambacho una jua kabisa sio haki yako, una tofauti gani na mwizi au jambazi?
Unajuaje labda hiyo kodi alikuwa anasomesha watoto wake na sasa hawaendi shule kwa muda wote huu ambao wewe hulipi, unakaa tu? Je kama ana wagonjwa alikuwa ana hudumia na wamepoteza maisha kwa ajili ya kukosa huduma? huoni kuwa wewe tayari ni muuaji? nimekupa mifano tu ya madhara ya wewe kukalia haki na stahiki ya mtu.
 
Wakuu naishi kwenye nyumba ya kupanga na familia yangu yenye vyumba vinne na Kila kitu quality kuanzia aluminum mpaka tiles nyumba ni nzuri sana mwenye nyumba alifariki ghafla mwezi wa 4 mpaka Leo mwezi wa 12 nakaa bure naona kama hii ni bahati kutoka Kwa mungu nyumba ya bure sababu nilisikia fununu ndugu wameshagawana Mali zake ila hii hawaijui hii nyumba alikua anafanya Siri sababu ni mpya imezinduliwa mwaka huu naomba muongozo jinsi ya kupata hati miliki ya hii nyumba wakuu
Kwa hiyo umeokota nyumba?Hauwajui ndugu zake?
 
Sasa ndugu siwajui na yeye alikua anasema ni Siri anataka awafanyie suprise
Hauwajui, lakini unasikia amefariki tena ghafla. Na kusikia ni mpaka usikie kwa mtu anaongea. Anayeongea anamjua mtu aliongea ama alishuhudia.

Unaonaje ukianza na yule uliyemsikia ukawapata ndugu na wewe kuendelea kulipa kodi.

Lakini hapo umeshaingiwa na nia ovu.

Halaf vipi namba ya simu mliyokuwa mkiwasiliana, haijachukuliwa hata na mke anaitumia? Mjulishe wewe ni mpangaji wa nyumba yake
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Wanaokoteza stori za Instagram uko wanatufanya sisi watoto wadogo 😃

Kwani mtu anapata faida gani kuwa muongo ???
Mwenge Dar ilikuwepo moja madalali walitaka kuiuza baada ya mwenye nyumba kufariki na familia hawaijui. Mpangaji aliondoka.

Majirani waliokoa jahazi wakafuatilia mpaka kuipata familia
 
Wakuu naishi kwenye nyumba ya kupanga na familia yangu yenye vyumba vinne na Kila kitu quality kuanzia aluminum mpaka tiles nyumba ni nzuri sana mwenye nyumba alifariki ghafla mwezi wa 4 mpaka Leo mwezi wa 12 nakaa bure naona kama hii ni bahati kutoka Kwa mungu nyumba ya bure sababu nilisikia fununu ndugu wameshagawana Mali zake ila hii hawaijui hii nyumba alikua anafanya Siri sababu ni mpya imezinduliwa mwaka huu naomba muongozo jinsi ya kupata hati miliki ya hii nyumba wakuu
Kuna jamaa yangu zamani kidogo alikuwa ndo kaachiwa kukusanya kodi na kumpelekea mwenye nyumba. Sasa jamaa akakaa miaka 2 hapati mwenye nyumba, àkamtafuta kumbe akilishafariki na wenyewe hawajui kuhusu hiyo nyumba. Jàmaa aliambulia kodi tuu wenyewe wakàja wakauza nyumba hadi leo anajuta.
Kuna watu wana hela hazina kazi wewe bahati yako hakuna mtu anafuatilia mambo ya nyumba wala hati.
 
Sasa ndugu siwajui na yeye alikua anasema ni Siri anataka awafanyie suprise
Ndugu huwajui wapi bwana sema tu ukweli roho imeshakuingia tamaa unaona umeshapata nyumba bure.

Main post umesema umesikia fununu ndugu wameshagawana mali ungekuwa na nia kweli ya kutodhulumu hiyo nyumba si ungewaambia hao waliokupa fununu wakawaambie bado nyumba moja hawajaigawana?
 
Nenda kwa hao maboss wenzake waliokupa taarifa za kufariki kwake hakosekan hata mmoja wa kupajua alipokuwa anaishi au familia yake
Usitafute namna ya kumiliki hiyo nyumba itakutokea puani
Haipatikani
 
hiyo kazi ,anaijua sana wamakonde usije THUBUTU kumpa nyumba au kiwanja alinde!
 
Ishu kama hii zipo sana ughaibuni, Ukikuta nyumba haina wakazi, na ukakaa kwa miaka mi3 bila kusumbuliwa inakuwa yako.
 
[emoji706]View attachment 3174399
Screenshot_20241211-134334_1.jpg
 
Ndugu huwajui wapi bwana sema tu ukweli roho imeshakuingia tamaa unaona umeshapata nyumba bure.

Main post umesema umesikia fununu ndugu wameshagawana mali ungekuwa na nia kweli ya kutodhulumu hiyo nyumba si ungewaambia hao waliokupa fununu wakawaambie bado nyumba moja hawajaigawana?
Huyo alioniambia nae anasema alisikika jujuuu bar jamaa wanazungumza na yeye ndugu hawajui na pia unaweza kukurupuka kumbe matapeli wa mjini sio ndugu zake
 
Back
Top Bottom