Naishi na Mwanaume, tatizo nikimgusia suala la ndoa anadai nisubiri hayuko tayari kwa sasa

Mimi nakuombea sana ninachofikiria mimi kiwe wrong.
Maana kwa mdada kutumika miaka minne plus kama mke halafu usiolewe nae, ni maumivu makubwa sana. I hope i am wrong, na nakuombea all the best, upate hitaji la moyo wako!
 

Inawezekana ikawa ni kweli pia


Lakini tusemeni ukweli kwa dunia ya sasa kuna mwanaume tu anaweza kumjengea mtu asiyemuhitaji? Akamfungulia biashara tena kubwa haswa na usafiri juu na vyote Viña majina yangu peke yangu bado kamfungulia kijacho wetu junior acc hela ananipa mwenyewe nikaweke

Kuanzia kiwanja nilitafuta mwenyewe yeye alinipa hela tu 16m na engineer nilitafuta mwenyewe kuanzia ramani hadi ujenzi nafatilia mwenyewe yeye anauliza tu imefikia wapi mafundi vipi na imemtoka more than 20m hadi sasa kwenye huo ujenzi na bado haijaisha, vyote hivyo alisema mwenyewe mke wangu Tafuta kiwanja unakokupenda nakununulia ee jamani tusiwe waongo wapo kweli?? Kama ya kutolea tu wanalilia

Bado nikiumwa hata ukucha iwe usiku wa manane atahakikisha nakua Sawa, nimetoka hosp nilivyojifunga vyote alikua ananifanyia mwenyewe kuanzia kunikanda maji kujua nakula nini kunicomfort sababu tulipoteza mtoto

Nimeshakua na watu kadhaa wazo tu la kimaendeleo hawakua nayo zaidi ya kuonana kunjunjana basii nimepata huyo ananiridhisha [emoji817] bado ananipa furaha tele

Tulizika mtoto akaomba likizo ya 1month tunakawa tunashinda wote tu hadi likizo imeisha

Hayo ni mema yake machache tu ambayo huko nyuma sikuwahi kuyapata

Mpaka namwambiaga Mbona unanifanyia mambo mengi hivi tena mazuri nitakulipa nini?? Anachonijibu ni ananipenda kweli na cha kumlipa ni kutokumsaliti na kuwa muanifu kwake basi, zaidi zaidi anatamani sana mtoto na Mimi sanaaa
 
Mimi nakuombea sana ninachofikiria mimi kiwe wrong.
Maana kwa mdada kutumika miaka minne plus kama mke halafu usiolewe nae, ni maumivu makubwa sana. I hope i am wrong, na nakuombea all the best, upate hitaji la moyo wako!
Ujue bana mabinti wakiambiwa kuhusu kujihamishia kwa mwanaume bila ndoa, watakuona mshamba au unajifanya mtakatifu; kumbe ni kwa faida yao binafsi. Ukiamua kujipeleka kwa mwanaume, make sure haupo desperate kwa ndoa, ukifika huko kaa kwa kutulia maana hajakwambia kuwa njoo ili nikuoe.

Mwanaume anaweza akakaa na wewe for years, ila moyoni mwake, wala hana hata wazo la kukuoa, as long as anapata mbususu na kupata huduma muhimu basi yeye anaenjoy tu. Au akakaa mpaka siku atakayojisikia mwenyewe ndiyo akaamua kukuoa, usimlazimishe na maswali ya "utanioa lini"

Wakati wanawake tukifika tu kwa mwanaume, tunachowaza next ni kuanzisha familia; watoto, ndoa n.k. Sasa unashangaa miaka inakata, watoto mmeshazaa na bwana hajawahi hata kuota ndoa, wala hata kujitambulisha kwenu hana mpango. Unaanza kuishi na wasiwasi na kisirani kwamba kwa nini hataki kunioa, what if akiniacha humu ndani na akaenda kuoa mwingine? So kisirani kinaanza ndani, na ndiyo ugomvi unaanza humo ndani, hamnywi maji hamkogi ni ndoa ndoa.

Ukiangalia miaka uliyopoteza na huyo mwanaume, unaona daah ngoja tu nivumilie, kwenda kuanza upya jeuri hiyo huna. So either utaendelea kuishi na kisirani chako au unabakia kujitia moyo kuwa "mbona ananipenda tu na tunaishi kwa amani"; kama uliyajua hayo mbona unalalamika?

Mtu unaishi naye ndani, mnazaa watoto anakwambia hawezi kukuoa ana malengo yake kwanza; kwamba mkifunga tu ndoa hayo malengo ndiyo yanakufa au? Bora mkiwa mnaishi tofauti afu akwambie usubiri ndiyo tutaelewa, sio mnaishi wote, mnazaa na watoto afu eti akwambie sijui sitaki wewe na watoto mpate tabu; hiyo tabu kwa watoto ndiyo italetwa na kufunga ndoa?
 
Ana

Sasa kwanini hakupi furaha ya ndoa na anajitahidi kukupa furaha kila engo. Amekubali kukuona ukihuzunika na kuumia na kukosa furaha kwa kukosa ndoa.Inafikirisha? Pole sana.
Jitahidi kumuomba mungu akufungulie hilo fumbo najua unajiuliza maswali mengi kila siku.
 
Kama mnaishi vizuri dada kula vitu hiyo ndoa itajawakuta mbele ya safari huenda unavyomlazimisha ndoa ndoa kuna kitu anajiuliza .
Sory nje ya mada vipi ushamzalia??
Na kama bado hilo nalo shida huenda ana waswas na uzima wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Yeye anavyosema tusifanye kwavile flani na flani wamefanya tusubiri muda utafika lakini kwa vitu anavyonifanyia ni Kama ananiweka kifungoni hivi kuwa hata nikimuacha moyoni nitaona sijamfanyia kitu sahihi

Kitu ambacho kinaweza kumnyima furaha siku nzima nikisema ndoa tu sasa nina kama miezi miwili sijalizungumzia hilo lakini anajua sipendi

Hopeful M/mungu ataleta kheri kama ndiye basi itakua kama siye wote tutakua na watu wetu tuliopangiwa nao
 

Amiin [emoji1431]

Nimeshamwambia ndoa sio sherehe ni kuhalalisha kwa M/mungu tu iwe ya halali anasema nivumilie kila kitu kitakua Sawa
 

Wa kwanza alifariki, huyu wa pili tunamsubiria[emoji2972]
 
Nacheka huku naogopa..hivi mtu anasemaje kuna vitu naweka sawa ndipo tufunge ndoa na wakati huo huo mnaishi pamoja jamani..tena na watoto juu.

Like seriously, ni afadhali kila mtu akawa kwao/kwake ukisema nna vitu naweka sawa inaeleweka..ila mpo humo ndani pamoja. Au anaogopa kugawana mali so anatengeneza zake kabisa afu ndo aoe muanze sasa kutafuta vya pamoja [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama yote anakufanyia kwa nini ukai kwa kutulia usubiri mpaka amue mwenyewe mfunge ndoa kipi kimepelekea ulete mada Jf zingatia sio kila anayechangia kinyume na fikra zako ukadhani anataka utoke kwenye mahusiano yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…