Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Endelea mkuu, naamini unaelekea kwenye kutoboa, kama sio ushatoboa kabisa
Tuendelee sasa..


.....Maana yule Mzee aliporudi, kabla hata sijamsalimia aliniuliza namdai kiasi gani? Tukapigiana hesabu akanipa changu alaf akaniambia "Fanya haraka utoke nataka kufunga geti tulale"

Sikujifikiria sana, kama niliweza kuondoka kwetu sembuse hapa? Nikabeba vyangu nikatoka. Hapo ilikuwa majira kama ya saa tatu usiku. Nikajichanganya mtaani. Niwe muwazi, pamoja na kukaa sana Dar ila watu wake sijawahi kuwaelewa. Kila mtu ni mjanja mjanja na anajua kila kitu,hakuna siku niliyotoka nje usiku nikakuta watu wamelala,mda wote wanapirika pirika tu. Pia hata mtu usiyemdhania anaweza akakuibia au kukudhurumu. Nasema hivi kwasababu ya kilichonikuta nilivyorudi mtaani. Nilikuwa natembea mdogo mdogo lengo ikiwa nielekee sehemu inaitwa Kariakoo maana niliambiwa huko kuna kila kitu japo sikuwahi fika. Kutokana na kubana bajeti sikutaka kupanda gari maana hela yenyewe ya ngama.

Kuna sehemu kule Dar panaitwa kwa Mnyamani. Maeneo yale nilikutana na watu kama wa 5 wakiwa wameshika fimbo, wanajiita sungusungu. Walinisimamisha na kuanza kunihoji, muda ule. Nikajaribu kutoa maelezo yangu, ila hawakutaka kunielewa. Watu wa Dar wanaongea haraka haraka sana hadi wakaanza kunichanganya. Naongea neno moja, wao washao gea 10.

Sijawahi kuona sungusungu anamsachi mtu, wala kumpiga mtu. Wakachukua hela zangu, bahati nzuri sikuziweka zote pamoja, nikabaki na kiasi kidogo. Waliponiacha, nikatembea hadi sokoni buguruni, nilipoona watu wengi wengi, nikaweka kambi pale kwa mzee aliyekuwa anauza kahawa. Kulipokucha nikapata kibarua cha kushusha matikiti. Hapo kidogo nikapata vijihela. Sikwenda tena kariakoo, nikaweka kambi hapo. Mida ya mchana, kazi hakuna ikabidi nitulie kwenye kijimgahawa cha mama mmoja hivi huku nakunywa soda maana hawaruhusu kukaa bure. Wakati nainywa soda yangu taratibu ili isiishe, kwenye tv kulikuwa na kipindi cha maswala ya shule (nishakisahau jina) ila channel ni Star Tv. Yani kile kipindi cha siku hiyo kama kilinilenga mimi, maana somo lilikuwa Kiswahili, maswala ya sentensi sentensi. Yule ticha alikuwa anafundisha maswala ya kutunga sentensi za "...nge..." Mara nikamsikia ametoa mfano "Ningejua, nisingeondoka" . Ile sentensi ikanishtua sana. Nikamwambia yule mama mwenye mgahawa abadili channel "Maliza soda uende" ilo ndio jibu alilonipa

Kimoyo moyo nikafikiria " Ningeenda kidato cha tano, nisingekuwa hapa" Nikajikuta napakumbuka nyumbani kwa wazee. Ikanipelekea kulikumbuka tukio moja ambalo lilitaka kuwagombanisha mama na baba. Ilikuwa ni kama wiki mmoja baada ya kudondosha kibox cha kondom darasani, kwavile nilipewa suspension ya wiki 3. Nilivyorudi nyumbani mzee alisema kwa wiki 3 zote itakuwa zamu yako kuchunga mbuzi.

Sasa siku hiyo tuko machungoni na na watoto wengine, tukaokota kiberiti cha gesi. Kule machungoni tukawa tunawasha majani alafu tunazima kwa kukanyaga. Sasa kuna muda tukawasha, ile tunazima, kukanyaga jani likapeperushwa na upepo, moto ukawaka na kwingine. Kila tukijitahidi kuzima, moto unapepea. Moto ukatanda kote, mbuzi zikaanza kukimbia ovyo. Kuona vile na sisi tukakimbia kuzifata mbuzi huku tunarudi nyumbani. Wanakijiji wakaitana, wakaushambulia moto na kufanikiwa kuuzima japo ulishaunguza eneo kubwa kiasi. Mzee mzima nikarudi nyumbani, moja kwa moja chumbani nikazuga kulala. Kumbe wakati tunakimbia na mbuzi kuna bibi mmoja alikuwa anaokota kuni alituona. Kwenye mkutano wa kijiji akatutaja tuliosababisha moto. Siku hiyo mzee alinipiga fimbo sio za nchi hii. Baadae namsikia anamuuliza mama " Hivi mama nanii, huyu ni mwanangu kweli??" Bi mkubwa nae akawaka "Nitolee wehu wako hapa, angalia lipua la mwanao alaf nenda kajiangalie kwenye kioo kama hujawahi kujiangalia" faza akawa mpole, maana kama ni pua tu, kweli tunazo.

Pia wakati nasubiria majibu ya kidato cha nne, kuna demu nilikuwaga nae ila akaja kunipiga chini baada ya kumpata mwenye hela. Miezi kadhaa akadaka mimba, ila yule jamaa akaikana. Kijiji chote kilikuwa kinanionaga na yule dem, habari zikasambaa mimba yangu. Demu nae akashikiria pale pale kuwa mimba yangu. Nilijitahidi sana kukataa , ila watu akiwemo faza hawakunielewa. Japo baadae sana ilikuja kugundulika kuwa mimba haikuwa yangu.

Hayo matukio yote nilikuwa nayakumbuka wakati nipo kwenye ule mgahawa pale buguruni. Nikamalizia soda nikatoka.

**** **** ***** ***** *****

Nilikomaa sana pale buguruni kwa muda mrefu, nafanya kazi pale na kujiegesha mule mule. Nakumbuka siku moja nilikuwa nimekaa na wabeba mizigo wenzangu tunapiga story. Akatokea jamaa akawa anatupa story za migodini, kuwa unafanya kazi kwa tabu ila ukitusua unasahau msoto. Jamaa alikuwa anafanyia kwenye migodi za Msumbiji, kuna eneo linaitwa Mtipweshi (kama sijakosea kulitamka). Story yake ilinivutia, nikajisemea, sibebi mizigo tena hapa, naenda Msumbiji


...............
 
Hiyo sehemu ya kwanza umesema hela uliibiwa mpaka mzee kesho alikusaidia hela ya chai na nauli!

Halafu mwishoni unamalizia kama baada ya kufika ubungo ulinunua vocha umpigie huyo ndugu yako! Hela ulitoa wapi mkuu?

Umechemka haswaaaa DUH!!!!
kumbe nawe wale wale wanaopenda kupinga ya watu.. tena huyu ni story yake mwenyewe anasumulia. muonekana mnayajua sana kila kitu humu.. kumbe pwaaa.. eeeeeh.. huwa nawapita ila hii ya true story imebidi nikuambie uwe unatulia shaaaa..

Makubwa.. nauli aliyopewa ilibidi ujiongeze.
Mazoea mazoea mimi naweza msaidia mtu 10 elfu nikijua anenda kupanda basi safari moja.. zilizobaki ni atajiju nazo. Ungekuwa wa hivyo usingejichemsha aiseeee duh!!!
 
Na hiii nayo kalii eeeheee ikaweje mkuu
Duh umenikumbusha kipindi flani nilisala nyumbani nikasepa hovyo ili kuwatikisa wazee. Wiki yakwanza ikapita sioni hata wakunitafuta, wiki yapili ikapita holahola nikaona msinichezee nyie..
Nikaandika meseji inayosomeka hivi:-

Wewe ndio mzazi waflulanga mtoto wako amefariki Dunia, natumechukua namba yako baada yakuona kwenye simu yake amesave Jina mama ndio tumeona tukutafute kukupa hii taarifa
 
Nilizaliwa miaka kadhaa iliyopita. Katika familia ya watoto 7,mimi nilikuwa wa 6.

Kama watoto walivyo, nilikuwa mtundu kiasi ila sio mtukutu. Nakumbuka nikiwa darasa la 5,niliitwa mbele na ticha nikafanye swali la hesabu. Nikafanya swali kwa mbwembwe, nilikuwa nasumbuliwa na mafua, kabla sijaondoka pale mbele nikatoa leso ili nijifute. Wakati naitoa, kibox cha condom kikaanguka, darasa zima full kicheko. Ticha wa mathe ndio ticha wa nidhamu..nikaambiwa nitangulie ofisini.

Nikala bakora zangu za kutosha, kisha ndio nikaombwa maelezo, kila nikijitetea hawanielewi. Ukweli sio kwamba nilikuwa na dem au nilishaanza mapenzi, ni ile tu utoto utoto, unaokota kibox cha condom alaf unakaa nacho uangaliage zile picha. Kesi iliisha baada ya mzazi kuitwa.

Miaka ikakata, siku zikaenda. Darasa la saba mwishoni, wakati natoka kujisomea nikiwa na wenzangu wawili, ghafla tukasikia miguno kwenye darasa moja, kuchungulia tunakuta mlinzi wa shule yupo na muuza ubuyu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]. Jamaa akatukimbiza maana ndio alikuwa
anajiandaa kupiga show alaf tumemtibulia.

Kitoto toto, tunakimbia huku tunacheka, nikaenda kuliparamia lori la mchanga wakati navuka barabara. Nikapelekwa hospital na kushonwa nyuzi 18,maana nilipasuka kichwani na usoni. Nikauguza majeraha, baada ya miezi kadhaa nikapona.

Baada ya kumaliza la saba, wazee wakaona nisisome shule za day, wakaamua kunipeleka seminari huko mkoani Iringa, mbali kabisa na mkoa wangu. Sijawahi ona shule ambazo wako strict kama seminari. Sema siku zikakata pia, wakati nipo kidato cha 3,hata mawazo sijui yalitokea wapi, me na rafiki yangu Shedy tukapanga tuuze nguruwe wa kanisa. Nakumbuka tulivibana vizuri ili visitoe sauti (vitoto viwili),kumbe wakati tunaishia, kuna sister akatuona (aliutambua mzura wangu). Wala hatukupigwa, tuliambiwa tutaje tulipowapeleka ili tusamehewe. Tukataja, wakafatwa. Tukashangaa wik end wazazi wetu wamefika, wakakabidhiwa barua zetu za kufukuzwa shule, tukaambiwa tusepe.

Mshua aliongea sana siku hiyo, njia nzima hadi tunafika home. Kwanza hakuninunulia chochote cha kula njiani, maji nilikunywa kwavile yanatolewa ndani ya bus. Kufika home,ilifanywa mipango nikajiunga na shule fulani ya private ili nimalizie O level. Nikiwa kidato cha 4,me na mdogo wangu ndio tukafanya ule msala wa kumfungia dingi kwa nje,alaf tukala ndizi zote..

Kufupisha,fatisha hii link kusoma kilichotokea maana nilishawahi kuandika hiki kisa:



Nikamaliza form 4,majibu yakatoka. Nakumbuka nilipata 3 ya mwisho mwisho huko. Nilikuwa napenda sana hesabu,ila cha ajabu nilipataga D. Na post zilivyotoka nikapangiwa HKL. Afadhali History,sikuwahi kulipenda somo la Kiswahili wala English,leo hii nikasome vishazi na ngeli shurutia ambazo nilivutwa sana masikio lakini sikuzielewa? Nikampanga faza anipeleke private Advance, akagoma. Msimamo wangu ukabaki me HKL siwezina sitaki. Faza akakausha. Baada ya wiki akaniita, akaniambia kati ya vitu viwili kimoja lazima nikiweze "KUSOMA HKL AU KUJITEGEMEA". Kikao kikaishoa hapo, nikaambiwa nikafikirie.

Nikiwa peke yangu chumbani, nikawa natafakari mavitabu, tamthilia, riwaya, ushairi ntakayoenda kusoma Advance, nikaona ngoma nzito ikiwa Mabala the Farmer kilikuwa kinanitoa jasho. Wiki moja baadae mshua akaniita tena, akanipigia hesabu zote za gharama zinazohitajika kuanzia nitakapoenda shule, alaf akanikabidhi cash pamoja na joining instructions ya shule. Akasema

"Vitu vyote utakavyohitaji kununua vimeandikwa humo na hela hii hapa, shule inafunguliwa tarehe 21,itakapofika siku hiyo nisikuone hapa kwangu, either uende shule au hiyo hela iwe mtaji wako wa kuanzia maisha"

Kikao kikaishia hapo. Ndani naona hapakaliki, nikaenda uwanjani kuangalia mpira ili kupoteza mawazo. Siku kama mbili mbele nikiwa nimekaa na washkaji, zikaanza story kuhus Dar es salaam. Kwamba ukijituma, na kuwa mjanja mjanja unafanikiwa. NIKAPATA WAZO LA KWENDA DAR.

Tarehe 15 /05 nikapanda bus kwenda Dar. Kabla sijatoka toka, Maza aliniuliza kama naenda shule, nikamwambia hapana, nachukua uelekeo mwingine.


Nakumbuka Dar es salaam tuliingia mida ya saa tano usiku. Bus ilisimama nikaona watu wanawahi kushuka, na mimi nikabeba vitu vyangu nikashuka. Kufika chini nauliza hapa ndio ubungo? ( Ndio sehem pekee niliyokuwa naijua) . Jamaa akanijibu "Hapa Mbezi dogo". Nikapaniki. Ikabidi nitafute sehemu nikae chini nitafakari vizuri. Kuna gari ilikuwa imepaki, nikakaa kwa chini, nikijiuliza nafanyaje.

Nilikuja kugundua badae chini ya lile gari kumbe kuna watu ndio sehemu yao ya kulala, na niligundua baada ya kile kifurushi changu nilichoweka chini kutoweka "NILIDATA"

•••••••• •••••••••• •••••••• •••••

Kwenye kile kifurushi ndio kulikuwa na nguo zangu pamoja na hela. Nikajaribu kuulizia, hakuna aliyenijali, naishia kutukanwa tu kuwa nawarushia stimu.

Mpaka kuna kucha, sikuupata mzigo wangu. Kuna Mzee mmoja ndio alinionea huruma akaninunilia chai na kunipa nauli ya kunifikisha ubungo, maana jamaa aliyetarajia kunipokea ilibidi nikutane nae ubungo. Kwavile namba zake nilikuwa nazo kwenye karatasi, niliongea nae kwanza kupitia simu ya yule mzee na kumuelezea kwa ufupi yaliyotokea.

Nikapanda daladala hadi ubungo. Kufika, nikaingia hadi ndani mule, nikaazima simu ya mtu, nikampigia tena jamaa yangu kumwambia kuwa nimefika. Wakati namsubiria, nikajiegesha sehemu.

Nikiwa pale, nilishuhudia tukio ambalo siwezi kuja kulisahau. Mbele yangu kulikuwa na Mwanaume wa makamo, kwa mavazi yake ni kama mchunganji, alikuwa anaongea na simu. Akatokea mtu mwingine kwa nyuma yake amebeba makaratasi kibao,ameyabana kwapani huku akiwa anakunywa maji ya uhai, yalipobaki nusu akaenda na kuyamwaga nyuma ya yule mchungaji, kisha akasubiri. Mchungali alipomaliza kuongea na simu, lile jamaa likamuuliza "Nani aliyekuruhusu kukojoa eneo ili?"

Mchungaji akashangaa, nahisi akumuelewa jamaa, ila alipotaka kuondoka, wakaongezeka wengine. Kuna mmoja akampiga kofi, yule aliyemwaga maji akamuuliza " Yani unakojoa eneo la wazi alafu unakuwa mkali?, Twende nae ofisini" Mchungaji akapaniki, wakamwambia atoe faini au akalale ndani. Mchungaji kujisachi, hela hana, atoe simu ili ampigie ndugu yake, simu hakuna. Mchungaji akalia. Ikabidi waazime simu, akampigia ndugu yake ili aje na hela ya faini.

Japo mchungaji alidata, ila mimi nilidata mara 100 zaidi yake. Ikabidi niweke vocha kwenye simu ya mtu tena, piga sana namba ya mwenyeji wangu ila haipokelewi, mwisho wa siku ikawa haipatikani tena. Kucheki muda,saa moja kasoro usiku. Nikazidi kudata.....



***** ***** ******* ******* ******

Imeendelea post #27

Imeendelea tena post #68

Imeendelea tena post #137
Nimesubiri sioni muendelezo..
..ngoja nikafanye kazi za watu, nisijekutana na yaliyomkuta ndugu Analyse kwenye ile kazi ya kulisha mifugo ya yule bwana.. au kwa lile bomba la Don.
Nitarudi jioni kufuata muendelezo.
.
.
.
 
Umenikumbusha hiyo ya kuangalia picha kwenye box la condom mie na wenzangu enzi tuko wadogo tumezifanya sana..
Ilikuwaga "salama condom", inaonesha hatua za uvaaji condom, kunjunjana na namna ya kuivua na kui-dump baada ya tendo.
Kwenye kunjunjana jamaa na bibie wamejifunika na ka-shuka nusu mgongo.. [emoji3][emoji16]
Nyingine ilikuwaga condom tunaijaza maji au tunaifanya puto/ pulizo. Afu yalikuwaga magumu kupasuka tofauti na zile puto nyingine za kawaida..
Basi ilikuwa tunazirusha hewani then tunafurahi. Msala wake mkutwe sasa.. Apo ndo ilikuwa ishu...
Nway hongera kwa ku-hustle..
We are waiting for muendelezo
Kumbe miaka ya 2003 ivi ndiyo umezaliwa ?
Maana condom zimekuja juzi juzi tu
 
Na hiii nayo kalii eeeheee ikaweje mkuu
Bmkubwa alizimia.... Kuna mdogo wangu wakike alilia hatari, simu yangu ikaanza kupigwa kwafujo zote manamba mageni ndio usiseme nikawa nawachora2 sikupokea. Baada yamda nikamtafuta msela nikampanga akawa kapiga namba yamdingilili akamueleza kuwa walikuta nimejinyonga nawakanichukua kunipeleka hsptl, nilipofikishwa hsptl wakagundua sijafa ila nilikuwa nimezimia. Ndo sasa nikaanza kuwaendesha navyotaka mimi mtoto nikageuka kuwa mkubwa nawenyewe wakageuka watoto
 
Bmkubwa alizimia.... Kuna mdogo wangu wakike alilia hatari, simu yangu ikaanza kupigwa kwafujo zote manamba mageni ndio usiseme nikawa nawachora2 sikupokea. Baada yamda nikamtafuta msela nikampanga akawa kapiga namba yamdingilili akamueleza kuwa walikuta nimejinyonga nawakanichukua kunipeleka hsptl, nilipofikishwa hsptl wakagundua sijafa ila nilikuwa nimezimia. Ndo sasa nikaanza kuwaendesha navyotaka mimi mtoto nikageuka kuwa mkubwa nawenyewe wakageuka watoto

Mkuu utakuwa unalaana wewe
 
Back
Top Bottom