Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Yaani huwa natamani ningekuwa na maisha ambayo naweza kusimulia.

Kuna watu maisha yao ni shule nzuri sana.
Ni rahisi sana kutamani lakini ni maisha magumu na ya mateso sana mkuuu...

Mshukuru Mungu hujapitia aina hiyo maana si raha wala fahari kupitia aina hiyo ya maisha.

Kuna ambavyo hawezi viweka na visimulia vigumu na vinaumiza..Acha kabisa mkuuu Mwombe Mungu akuepushie.
 
Umechemka haswaaaa DUH!!!!
kumbe nawe wale wale wanaopenda kupinga ya watu.. tena huyu ni story yake mwenyewe anasumulia. muonekana mnayajua sana kila kitu humu.. kumbe pwaaa.. eeeeeh.. huwa nawapita ila hii ya true story imebidi nikuambie uwe unatulia shaaaa..

Makubwa.. nauli aliyopewa ilibidi ujiongeze.
Mazoea mazoea mimi naweza msaidia mtu 10 elfu nikijua anenda kupanda basi safari moja.. zilizobaki ni atajiju nazo. Ungekuwa wa hivyo usingejichemsha aiseeee duh!!!
safi sana.

nawachukiaga watu wanaojua angalia kasoro...mbona huko madarasani walikua wanafanya Mitihani hadi mwisho mpk mwalimu anakuja anawambia swali la 10 lina makosa,ila yeye alishafanya na jibu akapata.

mijitu ya namna hii naipitaga na inaniboaga natamani niitwishe mitusi sema kila tusi naona sio jipya ni yale yale.

Asante kwa kunsaidia mchana.
 
Ni rahisi sana kutamani lakini ni maisha magumu na ya mateso sana mkuuu...

Mshukuru Mungu hujapitia aina hiyo maana si raha wala fahari kupitia aina hiyo ya maisha.

Kuna ambavyo hawezi viweka na visimulia vigumu na vinaumiza..Acha kabisa mkuuu Mwombe Mungu akuepushie.

Mkuu sijapita kwenye raha kiivyo, nina issue ambayo siku nikipata upako ninaweza kuiweka hapa.

Ila nadhani bado sijafikia maamuzi.
 
Sehemu ya 5:

.... Hakuna kitu kigumu kama kumngojea mtu ambae hujui yuko wapi au anafanya nini. Kwa wakati ule nilishindwa nifanye nini maana sikuwa na plan B. Ikabidi niendelee kuzuga tu mjini pale. Uzuri wa mikoani sehemu za kujiachia ni chache, nakumbuka ilikuwa ni siku ya nane nane, karibia mji wote wa Songea kuna sehemu huwa wanakutana. Kwavile sikuwa na mishe, ikabidi na mimi nijisogeze kwenye viwanja vya nane nane, sina ili wala lile pia sina plan maalum. Nikazungukia karibu vibanda vyote vya maonesho. Mpaka leo hii naamini kama unaishi Songea alafu kuna mtu unamdai ila anakukwepa au umepoteana na mtu kitambo, we kuwa mvumilivu alafu tegea siku ya nane nane utampata tu. Maana hiyo siku ile natoka tu getini, ghafla namuona yule jamaa wa harakati za migodi. Nilifurahi kichizi, japo mwanzo hakunikumbuka ila baadae kumbukumbu ilirudi tukaanza kuyajenga.

Jamaa ananipa story amekutana na majanga kibao kule, mara ya mwisho kwenda walifanikiwa kupata kajiwe kadogo kadhahabu akiwa na mwenzake Mbongo pamoja na Mzimbabwe. Ila utaratibu wao kule ni kwamba mkiwa katika eneo wote mnatafuta, atakayebahatika kupata, basi mnagawana wote kwavile wote mmehangaika. Sasa kisa chake ni kwamba yule Mzimbabwe ndio aliyepata mali, ila kutokana na tamaa hakutaka kugawana na wengine. Kwa hustling za machimboni zilivyo, ni vigumu sana mtu kufanya kazi mfano masaa mawili alaf akaondoka labda upate mali, ukifanya hivyo wengine wengine watahisi umepata tu. Sasa yule Mzimbabwe ili wengine wasimhisi, ikabidi ampe msala yule Mbongo mwingine. Alipayuka tu "We umemeza nini?" . Naskia ile kauli ilishtua wengi pale, maana njia yao kubwa ya kuficha ni kumeza. Yule mbongo akapaniki, ila mzimbabwe akakaza. Raia wengine wakamtaitisha yule mbongo ili aseme kameza nini. Huyu mshikaji wangu kujaribu kutetea, nae akawekwa kati. Wakabebwa wote. Yule mbongo wa kwanza naskia akalishwa madawa fulani ya asili ambayo yanasababisha kuharisha. Aliharisha sana ikafika hatua akawa analia.

Wadau wengine kila wakichambua kinyesi hawaoni kitu, wanaambizana bado hajanya mali huyu tumpe dawa nyingine, mchizi analia tu. Huyu jamaa yangu nae wakambana aseme mali iko wapi. Akijitetea, hawaelewi. Akatokea Mzambia mmoja na sululu, akafyeka vidole vya jamaa. Hapo na mm ndio nikagundua kumbe mshikaji mkono wa kushoto umebaki na kidole gumba pamoja na cha shahada (viwili tu),muda wote ananisimulia sikumtilia maanani nilikuwa napawaza mgodini tu.

Mshikaji anasema mpaka wale wadau walipokuja kushtuka kuwa yule Mzimbabwe hayupo, ndio wakaelewa atakuwa amewapoteza maboya tu. Jamaa yangu anamalizia kunisimulia kwa kusema alivyofanikiwa kutoka kule hajarudi tena hadi leo na hana mpango wa kurudi. NIKASIZI KIDOGO.

* * * * * * ***

Tulibadilishana namba za simu, tukaachana. Nikarudi ghetto, maana nilikuwa nishabahatika kupata sehem ya kujiegesha eneo fulani wanaliita moonlight, nyumba ya bibi mmoja hivi imechoka kichizi, ila hakuna jinsi, maana hela hakuna.

Ikabidi niwe najichanganya na raia wengine, mara leo nimekata nyasi za fensi vizuri, kesho nimesaidia mafundi ilimradi niingize hela. Napambana ili akiba yangu iongezeke. Nikasogea mashambani na kuanza kulima kama kibarua, fanya sana palizi, mwagilia sana bustani za watu mpaka siku moja nilipokutana na jamaa kutokea Namtumbo,sehemu inaitwa Nambecha, aliyenipa fursa nyingine.

Huyu jamaa akaja na story fulani kuhusu hazina iliyoachwa na Mjerumani miaka hiyo. Jamaa alipa ufafanuzi wa kina kiasi kwamba nikamuelewa, mm nikiwa kama baharia wa nchi kavu napigania kupata ushindi, na ushindi wangu ni mkwanja. Nikasema dili ndio ili. Kwa maelezo ya mshikaji, kati ya mali ambazo zina hela moja wapo ni rupia, mekyuri na pasi. Akasema nikifanikiwa mfano kupata pasi, basi maisha ya msoto yanaisha, kiufupi nasahau shida kabisa. Na kulingana na taarifa alizo nazo, kuna babu mmoja yupo Nyasa, huyo ndio mwenye pasi, tukifanikiwa kumpata huyo na kufanikiwa kuipata hiyo pasi ya mjerumani, tunakuwa na uwezo hata wa kununua nchi.

Nikaona miaka yote nilikuwa wapi? Fursa si ndio hii, ngoja nikaisake pasi ya mjerumani. Kilichonikuta, NILIJUTA.


.......
 
Hao wajuaji sana achana nao, wataishia kukukera tu
safi sana.

nawachukiaga watu wanaojua angalia kasoro...mbona huko madarasani walikua wanafanya Mitihani hadi mwisho mpk mwalimu anakuja anawambia swali la 10 lina makosa,ila yeye alishafanya na jibu akapata.

mijitu ya namna hii naipitaga na inaniboaga natamani niitwishe mitusi sema kila tusi naona sio jipya ni yale yale.

Asante kwa kunsaidia mchana.
 
Back
Top Bottom