Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Mungu atakuponya mdada usijar,semah fanya kwenda kuchekiwa hospital nasio kutumia kila dawa unayoshauriwa,pengine izo dawa zinaongeza kasi ya tatizo lako.
 
Umewahi kwenda hospital kuwaona wataalam wa magonjwa ya ngozi?
 
Dada kama ujawahi kupima damu/ afya basi kesho nenda jibu utakalolipata ndo mwanzo kupata dawa. kuna MTU namjua yeye akiumwa na mbu au kujikuna basi hilo kovu halitoki milele, baada ya kupima tulipata jibu na amekubali hali hiyo anajistili kwa nguo ndefu.

na mbaya zaidi ni mweupe yaan magonjwa haya sikia kwa MTU. makovu ni madogo madogo mwili mzima yaan hayatoki. kuna kipindi aliishi dar akaanza kutumia cream na asali na lile joto cream ikamkubali kweli yalipungua kwa 90 % aliporudi mkoan yakarudi upya. hilo shape sasa alilo nalo wenye genye zao hawachoki kutuma maombi na hayajibiwi, kweli mungu hakupi vyote.
 
Nenda kawaome madaktari wa ngozi. Nna rafiki alikua hivyo sijui walifanyaje!
 
just focus on how to live alone for now and work hard on ur carrier.. jaribu kua smart sana na pia nenda kamwone dermatologist.. hta kama una makovu kiac gan naamin ukipata wa kukupnda hatajali sana instead atakua bega kwa bega na wew ktka kutafuta ufumbuzi...
 
Fanya water therapy, jaribu inaweza kukusaidia
 
Kuna professor Massawe,yuko posta,Ana clinic ya Ngozi..ni Dr mzuri sana sana..Ila ndo ujipange gharama zake,clinic yake iko mtaa wa samora,
 

Jaribu kutumia Miss white full package
 
Dada hilo ni tatizo dogo sana kwa MUNGU WA ELIYA (1 Falme 18:21-40), sasa ili upone hakikisha kila unapotoka kuoga jipake mafuta ya mzeituni siku zote na utaiona ngozi yako ikipona na kuwa nzuri kipita hata mwanzo au ulivyozaliwa.
Hayo mafuta usichanganye na kitu chochote.( Kutoka 30:26-31).
Kama una swali karibu!
 


Wokovu siyo dini mbona unamshauri aende TAG au EAGT, unajua anakosali leo? mbona hujamshauri aende kwa mch lusekelo? maana na yeye ameokoka na anahubiri wokovu, na kuponya watu kwa maombezi, ni kweli yesu anaponya akimukiri na kujitenga na uovu na kumtegemea yeye kwa kila jambo atapata faraja na huo uponyaji anaoutaka, yesu ni mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…