Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Weka picha hata ya mkono tuone, online dr's wanaweza shauri kitu kwa kuona tatizo husika, magonjwa ya ngozi ni mengi
 
Mimi ulinikataa ww kwann uangaike dawa wakati unapendwa jinsi ulivyo
 
Kun kipindi miaka ya 2004 - 2006 KCMC walikuwa vizuri sana kwa magonjwa ya ngozi. Sina uhakika kwa sasa...ila najua bado wana clinic ya ngozi nzuri tu. Jaribu kufika huko....KCMC, Moshi.
 
Tatizo lako sio ngozi wala makovu, tatizo lako ni kujichukia. Unahitaji msaada katika hilo kwanza. Ukifanikiwa kumaliza hiyo shida, utakuwa na amani hata issue ya kupata mchumba itamalizika.

Jifunze kujikubali, kujipenda na kuwa positive. Kila Mtu ana challenges za aina fulani mwilini, ngozi ikiwa mojawapo. Kuna Mwenye chunusi kama kijana, kuna Mwenye oily skin akinawa tu uso kama kitumbua kilichopikwa Na moto mdogo, kuna anaebabuka. Yaani Dotnata na Yule twin wake wanapata wachumba wewe unakosaje? Kuna Mwenye matege, Mwenye miguu mikubwa kama nje, kuna Mwenye kifua cha kususiwa, kuna Sony flat wega, kuna Mwenye nywele kama za paka. Mwisho wa matatizo kuna Mwenye akili za kupulizia, moja haikai, mbili haisimami! Yaani wewe ngozi yako ndio unaona mwisho wa dunia?

Nimalize kwa kusema hebu Nenda hospitali kwa ajili ya ngozi. Halafu soma kuhusu eczema. Mwisho anza kujipaka olive oil ama mafuta ya nazi tu, Na usitegemee matokeo kabla ya kumaliza Mwaka. Lakini anza kujifunza kuwa positive Na mwonekano wako huku ukihesabu Yale ambayo yako vizuri kabisa kwako. Kila la kheri.
 
Nenda hospitali kacheki full blood picture pia tafuta special list doctor wa ngozi muelezee matatizo yako anaweza kukupa dawa na ukapona
 
Barikiwa mtumishi kwa ushauri huu! Injili ya Kristu na isonge mbele!
 
nitaachaje kujichukia akati vyote ulivotaja vinanihusu,post yangu ya nyuma nimeeleza jinsi nilivyo
 
Nenda hospitali kacheki full blood picture pia tafuta special list doctor wa ngozi muelezee matatizo yako anaweza kukupa dawa na ukapona
sawa najipanga kufanya hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…