Najihisi nimekuwa mraibu, Wangapi mmeweza kutumia smartphone / laptop siku nzima bila kutumia internet ?

Najihisi nimekuwa mraibu, Wangapi mmeweza kutumia smartphone / laptop siku nzima bila kutumia internet ?

Imefikia hatua siku hizi hata familia na wanandoa hawanaa ukaribu, kuzungumza na upendo umepungua kwa sababu kila mtu akirudi nyumbani yuko busy na smartphone yake. Kitu mbaya sana kwa afya ya ndoa
 
Sidhani kama kuna siku nishawahi kua offline [emoji2][emoji2][emoji2356][emoji2356], labda nipoteze simu napo hazitazidi siku mbili lazima nirudi tena
We kiboko, I can't you. Mi kukaa bila bando week ni mara nyingi tu. Hua nahisi mtu akinicheck wasap akiona kimya atanipigia tu kama ni muhimu.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Umetusema kabisa yani, ndivyo ndoa nyingi zilivyo nowadays.
Inasikitisha sana mkuu

Nimejifunza kwa familia ya rafiki yangu ya wamejitia nidhamu kuna muda ukifika wanaweka simu pembeni wanapiga story na mke wake na kucheza cheza na watoto wao wadogo.

Nimeona upendo na furaha vimeongezeka.

Nikamuuliza jamaa yangu amefauluje akasema mwanzo mgumu lakini sasa hivi imekuwa kama sehemu ya maisha yao
 
Tangu mwaka huu uanze sikumbuki siku ambayo nilikuwa offline, Nina biashara zangu na kazi sio kwamba nipo idle.

Yani uwe na smartphone halafu ukose data waweza kuhisi unakosa mahitaji ya msingi, ukifika hii stage jijue ushaanza kuwa mraibu.

Matumizi ya data napenda kuingia Youtube kufatilia habari za Millard Ayo na channels nyingine zinazojielewa, Napenda kuiingia whatsapp kuangalia status, Twitter kufatilia habari za kimataifa, kuperuzi jamiiforums, usiku napenda kucheki tamthilia ama documentary, n.k.

TIKTOK niliitoa, ukitaka kujua maana ya kupoteza muda bila faida tumia hii app.

Wangapi mmeweza kupiga kavu siku nzima bila net
Huyu ni mimi kabisa
 
Back
Top Bottom