Najiona maisha Yangu yakikosa nuru kabisa na kuelekea ukingoni

Najiona maisha Yangu yakikosa nuru kabisa na kuelekea ukingoni

Pole saa man nafahamu maumivu uliyonayo,mimi nililala na mwenye ngoma 2018 bahati nzuri asubuhi kabla ya kusepa ndo ananiambia kua ana ngoma mwaka wa 4 na yupo kwenye dawa. Akanitolea kadi na vidobge dah alinivuruga vibaya sana na ukizingatia nilipiga peku usiku kucha,niliacha kila kitu nikaenda hospital kupata PEP nilitumia mwezi mzima ila pamoja na kuwahi kupata PEP nilikonda vibaya na nilikua mtu wa mawazo muda wote.

Wahuni,ndugu na bi mkubwa alikua amenishtukia alinibembeleza mno nimweleze kinachonisibu maana nilipukutika ghafla na nilikua mtu wa huzuni sana muda wote na nilikua nakaa pekee yangu staki kukaa na watu,masomo hayaendi. Baada ya kupima zaidi ya mara 50(nilimaliza boksi mbili kila mara nilikua nikijipima gheto) ndani ya miezi miwili nikajikuta sina ngoma. Hapo ndo nikapona na kila kitu kiliisha.
 
Pole umeyataka mwenyewe. Angalia sasa umepata maradhi na umeharibu urafiki wenu ambao huenda ungekuwa wa faida kwa hapo baadae.

Vijana tujitahidi kudhibiti tamaa zetu za kimwili, vinginevyo tutafute mpenzi mmoja muaminifu wa kuweka naye malengo.

Tukumbuke kesho yetu ni matokeo ya mawazo na matendo tunayoyafanya leo.
 
Pole sana FORTUNE JR huo ndio uamamume sasa!...

Halafu, kuwa na ngoma sio MWISHO wa maisha... Wenye ngoma wanaishi maisha mazuri mno kuliko wenye sukari...

Cha muhimu ikifika wa kati wa kutumia zire karanga ... Zingatia.

Mwenye ngoma anakula takataka zote nzuri za anasa... Na anaendelea kudunda...

Ila kisukari, kansa, BP... Kuliko uugue hayo magonjwa... Ni mara mia upate Ngoma!
Acha kumpa matumaini ya kusema bora...ukimwi ni ukimwi tuu bana..shida ya ukimwi ni kukosa tumaini...haya mengine ya kina kisukari unakua na matumaini..
 
Back
Top Bottom