Najiuliza wakati shetani anaasi mbinguni, alishawishiwa na nani? Maana hakukuwa na shetani muda huo. Binadamu tunashawishiwa na shetani dhambini

Najiuliza wakati shetani anaasi mbinguni, alishawishiwa na nani? Maana hakukuwa na shetani muda huo. Binadamu tunashawishiwa na shetani dhambini

Binadamu wa sasa tena wa jf wanaomhasi Mungu kwa kumkana hadharani kwani wanashawishiwa na nani mkuu?

Imani za ki dini zinafundisha kwamba Binadamu wanashawishiwa na shetani kufanya maovu.

Muovu ni mfuasi wa shetani.

Je shetani wakati anaasi alishawishiwa na nani enzi hizo ? Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuhasi ?
 
Mungu Baba aliwaacha viumbe wake huru sana hapo awali.Ulifika muda wakawa wanataka kugusa hadi nyaya za umeme.Sikuelekezi usome sehemu gani ya bible.Anzia mwanzo.
Yes, swali lake ni zuri sana tu, sababu kumbuka bibilia inasema kwenye mbingu mpya na nchi mpya dhambi haita kuwemo... Sasa je kivipi wakati hata mbinguni hakukuwa na dhambi lakini shetani alipata wazo la dhambi?
Kama binadamu tatukuwa huru kama kipindi hicho na sasa, hawatafikiria uovu kama sasa hata kwa nyakati moja?
je, Mungu atatupa uwezo wa ziada wa kuepuka dhambi ambao hakuwapa watu wa mwanzo?
Dhambi ni uvunjifu wa sheria sasa je inasemaje dhambi haita kuwepo wakati sheria zitakuwepo?
 
Swali zuri sana

Hawa CHAWA wa Kwenye siasa Chanzo chake ndio nyakati hizo

Shetani ni Lucifer ambaye alipenda sana Sifa na kwa kujua hilo Malaika wenzake wakawa wanampa Sifa za Uwongo Kwamba Yeye ni kama Mungu

Naye akaamini na kujipa Utukufu

Kilichomkuta kila Malaika anakijua hasa Mikael, Gabriel na Raphael

Ulale Unono 😀😀
 
Mungu Baba aliwaacha viumbe wake huru sana hapo awali.Ulifika muda wakawa wanataka kugusa hadi nyaya za umeme.Sikuelekezi usome sehemu gani ya bible.Anzia mwanzo.
Yes, swali lake ni zuri sana tu, sababu kumbuka bibilia inasema kwenye mbingu mpya na nchi mpya dhambi haita kuwemo... Sasa je kivipi wakati hata mbinguni hakukuwa na dhambi lakini shetani alipata wazo la dhambi?
Kama binadamu tatukuwa huru kama kipindi hicho na sasa, hawatafikiria uovu kama sasa hata kwa nyakati moja
je, Mungu atatupa uwezo wa ziada wa kuepuka dhambi ambao hakuwapa watu wa mwanzo?
Dhambi ni uvunjifu wa sheria sasa je inasemaje dhambi haita kuwepo wakati sheria zitakuwepo?
 
Chanzo cha uovu kwa mujibu wa dini sio shetani.

Hata wale ambao wanadhani kuwa peponi itakuwa ni sehemu ya raha tu na hakuna dhambi wanapaswa kutafakari upya kupitia mfano huu.

Kuna uwezekano mkubwa jinsi unavyoishi hapa duniani kwa kuepuka dhambi ndivyo utatakiwa kuishi hivyo hivyo huko peponi kwasababu nako dhambi inawezekana kutendeka.

So yatakuwa maisha ya leo upo peponi ukamtamani mke wa mwenzio hapo hapo utajikuta upo chumba cha pili unaota moto

Kwasababu stori inaanza kwa kuitaja mbingu kuwa ni sehemu tukufu ambayo mema tu ndio yanatendeka.

Lakini in the middle of story mambo ya kusalitiana (uovu) yanaibuka.

Na sio tu kusalitiana bali ni Shetani kupata kundi kubwa la uungwaji mkono ambao walikuwa Malaika.

Hao malaika wanaotajwa kuwa upande wa Shetani sio wawili au watatu, ni zaidi ya theluthi.

Can you imagine hilo kundi la malaika liliweza kuona shetani ana haki?

Je wewe unamjua zaidi Mungu na kumfahamu kuliko hao Malaika waliokuwa wakiishi naye karibu?

Huwenda tukio kama hili lingefanyika katika mazingira yetu haya ambayo njaa inaweza kununua hadi utu wa mtu, pengine tungeweza kuwapuuza hao waasi kwa kauli rahisi tu kuwa wamehongwa kwasababu ya njaa. Na still inge-sound very logically.

Lakini kumbuka huko ni mbinguni hakuna njaa, na pesa haina thamani yeyote ya kuweza kuifirikia kuwa ndio sababu ya hao malaika kushawishika.
 
Back
Top Bottom