Najiuliza wakati shetani anaasi mbinguni, alishawishiwa na nani? Maana hakukuwa na shetani muda huo. Binadamu tunashawishiwa na shetani dhambini

Najiuliza wakati shetani anaasi mbinguni, alishawishiwa na nani? Maana hakukuwa na shetani muda huo. Binadamu tunashawishiwa na shetani dhambini

Hili swali huwa najiuliza sana

Ni nani alimshawishi shetani kumuasi Mungu?

Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuasi ?
Mungu mwenyewe ndio Shetani, yaan hapo ni kupiga hesabu ngumu sana ndio upate jibu hizo calculation sio ndogo ila mwisho jibu linakuja kwa mujibu wa maandiko Mungu mwenyewe ndio Shetani, km unapingana na Mimi basi ungana na Mimi nikuthibitishie hilo kwamba ni kweli Mungu na Shetani ni kitu kimoja
 
Kwenye Qur'an, imeelezwa sababu ya shetani kuasi...

Kosa lake lilikuwa kutokumsujudia Adam , sijda ya heshima na kutambua utukufu na daraja aliyopewa juu ya viumbe wengine.

Kwanini aliasi..... Ni kwasababu ya husda alokuwa nayo kwa baba yetu Adamu, aliapa kwamba yeye angefanywa Bora angemuangamiza na Adamu akifanywa Bora angemuangamiza pia.

Kwanini aliachwa akaasi..... Binadamu na majini wanauhuru wakuchagua njia wanayotaka kupita, Wana nguvu ndani ya maamuzi ya kuwa wema au waovu, kwahyo njia utakayoichagua itakuwa ni jukumu lako na utapelekwa huko huko unapokutaka.

Shetani tangu alivyoasi mpka Leo Bado anaendeleza kazi yake, lakini pamoja na uwepo wa shetani watu wema wapo na waovu wapo, ingekuwa shetani anaushawishi wa Moja kwa moja kwa watu, wema wasingekuwepo hata mmoja.

Shetani ana nguvu baada ya wewe mwenyewe kuamua kufata njia isiyosahihi na yeye anakushawishi zaidi Uende huko huko ulipokuchagua.

Mfano: Wewe una rafiki yako muhuni, mvuta bangi lakini hajawahi kukwambia hata siku Moja njoo tuvute, mkikutana ni story basi. Siku Moja ukaamua mwenyewe tu hebu nami nijaribu kuvuta, mshkaji akakupa bangi ukavuta, mshkaji akaanza

" nikivutaga hii Huwa najiskia vizuri sanaa, inanipa mzuka".

Kuanzia siku hiyo mshkaji akaanza kukuvuta zaidi kwenye uvutaji , akikuona

" Leo mshkaji wangu Nina Ile ya Arusha kbsaa, ya Leo Leo".

Usinambie katika hali hii rafiki yako ndo kakuingiza kwenye uvutaji, Bali ni wewe mwenyewe ndo umeingia.

Ndomna baada ya shetani kuasi kukaja miongozo, na mitume ili kumuweka mtu katika lengo lake husika na asifate nyayo za shetani aliyeasi. Kwahy ukiiacha hiyo miongozo basi wewe na shetani hamna tofauti wote waasi na shetani atakuwa na nguvu juu Yako kwakua umemfanya rafiki.

Lakini ukiifata miongozo uliyopewa shetani hawezi kuwa na nguvu juu Yako.
Mungu ni upande wa pili wa Shetani yote yaliyotokea ni mipango yake alipanga iwe hivyo yeye mwenyewe ni sawa na wewe uchonge draft uweke kete kisha ucheze mwenyewe both side huku una attack huku una defend ndio ilivyo kwa Mungu na Shetani, ni ngumu sana kuelezea na ngumu pia kumshawishi mtu aelewe hasahasa aliepandikizwa elimu fulan kisha akagoma kujiuliza maswali au kuuliza maswali kabaki tu km Zombie fulani
 
naunga mkono hoja.
ELIMU YA FALAKI inasema shetani alijisemea Moyoni mwake alinuia ndani ya moyo wake mambo mawili 1)ashawishi malaika 2/3 wamuasi Mungu wawe upande wake alijua kwa vilw alikuwa na ushawishi mkubwa Mbinguni mana alikuwa ni malaika mkuu wa sifa LUCIFER ingekuwa rahisi kuwashawishi asilimia kubwa ya malaika anaowaongoza waungane naye wangemsikiliza kutokana na nafasi yake aliyokuwa nayo na shughuli aliyokuwa anaifanya mbinguni.

2)nitatengeneza enzi yangu na kiti changu cha enzi /utawala wake/ufalme wake juu ya mbingu iliyopo ,new mbingu nyingine mpya juu zaidi yabiliyopo,malaika wa Mungu wachache watakaobaki 1/3 ambao watakuwa loyal kwa Mungu hata wakifanya vita juu yake hawatamshinda kwa vike aliamini yeye atakuwa na jeshi kubwa la sehemu kubwa ya malaika upande wake yani 2/3
(Haya alikuwa anawaza moyoni mwake)..MOYONI NDANI YA MOYO WAKE.
Kabisa mkuu na ushaidi mwingine ni kwamba mpaka dhambi inaingia duniani akukua na shetani shetani alikua Bado kwenye majukumu yake mbinguni
 
Back
Top Bottom