OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Baadhi ya mambo ambayo yakizidi sana huwa nayaona ushamba na ulimbukeni. Haya mambo mimi yamenipita mbali kabisa.
1. Kujipost WhatsApp status
Hata kama nitafanya jambo gani, hata kama nimepata nini cha mafanikio huwezi kukikuta status. Mwaka jana nimegraduate taaluma mbili tofauti lakini huwezi kukuta status. Acha status hata graduation sikuhudhuria(Japo sio ushamba)
Sijui nimenunua gari kali najisikia aibu sana kujipost. Hata picha tu ya gari sina, na zile zilizotumiwa na Mjapani nilishazifuta.
Kuna mdogo wangu alikuwa anapenda kupiga picha na gari anajipost. Nikamkataza.
Yule baby alikuwa anapenda kujiselfie na mimi halafu anajipost. Nikamkata kistaarabu tu baby don't do that. Hata kesho nikifanya harusi nadhani hakutakuwa na status.
Naona wenzangu wanapost matokeo ya watoto wao yaliyotoka jana. Mimi A tupu za wakwangu siwezi kuzipost, naona ulimbukeni. Ahadi ya zawadi niliyompa akipata A zote nitampatia, nitamtia moyo aongeze bidii na kumpeleka vacation ya kisima.
2. Kutumia elimu na kazi yangu kujiona bora
Nina mavyeti mengi tu lakini sio bora kuliko wengine. Sio bora kuliko mlinzi na mfagizi pale ofisini. Wakati wengine wakipita bila hata kumsalimia mlinzi na kusaini daftari getini. Mimi lazima nimjulie hali nijitambulishe. Hata akisema basi nenda tu, namwambia hapana nitasaini hapa na kule kwa Mkurugenzi nitasaini. Maana ndio utaratibu.
Tukiwa shamba mimi sio bora kuliko kibarua. Kwa hiyo msosi wa shamba utakula wote.