Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Aminia sana, huo ndo uanaume sasa siyo kila siku mastatus WhatsApp kama shanga halafu yote picha za mtu
 
Baadhi ya mambo ambayo yakizidi sana huwa nayaona ushamba na ulimbukeni. Haya mambo mimi yamenipita mbali kabisa.

1. Kujipost WhatsApp status
Hata kama nitafanya jambo gani, hata kama nimepata nini cha mafanikio huwezi kukikuta status. Mwaka jana nimegraduate taaluma mbili tofauti lakini huwezi kukuta status. Acha status hata graduation sikuhudhuria(Japo sio ushamba)
Sijui nimenunua gari kali najisikia aibu sana kujipost. Hata picha tu ya gari sina, na zile zilizotumiwa na Mjapani nilishazifuta.

Kuna mdogo wangu alikuwa anapenda kupiga picha na gari anajipost. Nikamkataza.

Yule baby alikuwa anapenda kujiselfie na mimi halafu anajipost. Nikamkata kistaarabu tu baby don't do that. Hata kesho nikifanya harusi nadhani hakutakuwa na status.

Naona wenzangu wanapost matokeo ya watoto wao yaliyotoka jana. Mimi A tupu za wakwangu siwezi kuzipost, naona ulimbukeni. Ahadi ya zawadi niliyompa akipata A zote nitampatia, nitamtia moyo aongeze bidii na kumpeleka vacation ya kisima.

2. Kutumia elimu na kazi yangu kujiona bora
Nina mavyeti mengi tu lakini sio bora kuliko wengine. Sio bora kuliko mlinzi na mfagizi pale ofisini. Wakati wengine wakipita bila hata kumsalimia mlinzi na kusaini daftari getini. Mimi lazima nimjulie hali nijitambulishe. Hata akisema basi nenda tu, namwambia hapana nitasaini hapa na kule kwa Mkurugenzi nitasaini. Maana ndio utaratibu.

Tukiwa shamba mimi sio bora kuliko kibarua. Kwa hiyo msosi wa shamba utakula wote.
Ni kweli ujiposti status WhatsApp lakini bado una ego hata, hiki ulicho kileta kinaonesha wewe ni mjivuni, ni kama ulikua unataka kutuambia kwamba unamiliki gari na pia wewe ni msomi ungekua sio mtu wa kujionyesha ungekausha hata usingeandika huu uzi
 
Mimi kujiweka status ndio siwezi
Na kufanya graduation sijawahi..
Sio kama wanaofanya nawaona washamba HAPANA sipendelei tu sherehe
 
Kiukweli mimi status naweka, mfano 2024 nilivyopata CPA aisee nimepost picha zaidi ya 10, basi tu najiskia vizuri na wala siyo kumringishia mtu, ni part ya celebration
 
Mkuu wewe kama mimi tuu
Kuna wanangu niliomaliza nao Telecom pale Cive walikua watu wa ku show off status ila mii wala

Nulipo piga electrical south africa wala hakuna ndugu aliyekua anajua an ni mtu wa kimya kimya..

Juzi nimeenda dubai lakini cha ajabu sijapiga picha hata kidogo. Mpaka mdogo angu anashangaa huyu blaza vipi ila naona normol tuu..

Maisha ya mtandaoni kujianika mi ndo siwezi kabisa aiseee
Hii ni nature niliyonayo toka advance nilipo piga A ya phy na chem wala sikua mtu wa show off zaidi zaidi waliokuwa and anapost matokeo yangu ni wale ndgu wa karibu tuu..
ila hapa amejianika aiseeeeh
 
Status Mara nyingi inaeleza mood ya siku husika, mf birthday n.k kwahiyo kupitia status nirahisi Sana kumsoma mtu kweny swala zima la utulivu wa akili yake.
Kupost na kufuta baada ya muda mfupi maana yake uwezo wake wa kufkria na kung'amua jambo ni mdogo. Kupitia status utakua tabia nyingi Sana za watu.
 
Back
Top Bottom