Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Hao hawatukanwi wanaambiwa ukweli!!!

Au labda siyajui matusi ya single mama,em weka sample single mama anatakiwa aambiweje isionekane tu kwao.
wanabezwa kitu ambacho chanzo Cha single mom ni sis wanaume tuwe wakweli......

Nimekulia familia ya wazazi wawili lakini mama alinisisitiza kuwa hakuna mwanamke au mwanaume asiyehitaji mwenza....

Hivyo ukiona hujisikii kumwoa huyu single mom mpite tuu lakini sio kubezwa na kuonekana ni wakosaji ktk hii dunia

Wengi humu ndani wamelelewa na single maza kibao na waliona mama zao wanavyowapambania tupunguze mihemko ya kijinga ili tuonekane gents!

Japo mimi sipo tiyar kumuoa single maza na siwezi.... maake nina mifano yao Mingi ...... Lakini tuwaheshimu ni ndugu zetu, dada zetu, binamu, na mama pia
 
Ukishaelewa maana ya mitandao ya kijamii. Hutaita mtu mwingine mshamba kwa sababu hajafanya kile unachofikiria wewe. Binafsi yangu hutakuta picha yangu status lakini sijawahi kuona shida watu wengine wanavyoshare moments zao kwenye status.

Jambo la kwanza uelewa mengine huitaji elimu ya degree kutofautisha JF na Whatsapp na uulize kwani kilichofanyika hapa kinatofauti gani na kile kinachoitwa ushamba.
A million doller question...
 
Ila jamiiforums huwa mnajifanya hampendi baadhi ya vitu afu mwishoo wa siku mnakuja kujiumbua wenyewe,
mfano TikTok afu wote mnaifahamu sound ya kaongo yeye Sasa sijui mmeifahamia wapi??
Kila mtu afanye kinachompa amani.....

Ukilogwa ni wewe, uonekane mshamba sisi haituhusu

Hutaki kuona status ya mtu..... una u-mute kiaina
 
Mimi napost hata nikila wali mbegu napost yan ile watu wanavyo comment na kushare mawazo Ndio nainjoi tunapiga story sna tunakumbukana..

Nikiwa nawana mtaani nachangia mada yoyote sikai kimya kwamba wataniona nina vimba nilicho nacho

Mtaani huku ukiwa mtu private sana unaonekana unajidai unamajivuno..

Mimi kwakweli napost atakaye nuna anune atakaye furahi anakoment tunapiga mastori
Na hivyo ndivyo maisha yasanapswa kuwa, fanya unachoona kinakupa furaha bila kuvunja sheria. Kama kunakitu kitakuwa hakipo sawa tuelekezane bila kuitana washamba...
 
Babu yangu alikufa miaka ya 1940 Kipindi hicho Baba yangu alikuwa bado mdogo yupo shule ya msingi.

Baba yangu alinisimulia kwamba walimzika babu yangu kwenye makaburi ya kanisa na wala hawakuwa na picha yeyote hata ya kumbukumbu waliyo itunza.

Na wakati babu yangu anafariki hakuacha picha yeyote na wala hakukuwa na picha yake yeyote.

Yani sisi tumekuja kuzaliwa tunabaki kupewa stori tu za babu, Lakini hata sura yake hatujawahi kuiona. Na hakuna picha yake hata moja iliyo tunzwa.

Sasa kama hupigi picha kuna zile,
Fun Moments ulizo ishi kuna siku unatamani uzipitie halafu hata picha ya kumbukumbu huna.

Unabaki kusimulia tu bila evidence yeyote. Hata wajukuu wanaweza kudhani una wadanganya.

Unatakiwa uwe na picha na videos zako nyingi. Kiasi kwamba hata ukikaa na wajukuu zako unapiga nao stori. Unawaambia mimi nilifika USA, Canada, Ulaya, Australia n.k unawapa picha na videos waone.

Take pictures have memories post everywhere, Document your life. Keep records.

Sasa unaficha ficha hiyo sura, Hupigi Picha, Halafu siku ya msiba wako, Ndio ile watu wana hangaika kutafuta picha zako hawapati.

Halafu ukishazikwa ndio umesahaulika mazima. Hata wajukuu wakija kuhitaji picha za babu yao. Hazipo.
 
Mkuu wewe kama mimi tuu
Kuna wanangu niliomaliza nao Telecom pale Cive walikua watu wa ku show off status ila mii wala

Nulipo piga electrical south africa wala hakuna ndugu aliyekua anajua an ni mtu wa kimya kimya..

Juzi nimeenda dubai lakini cha ajabu sijapiga picha hata kidogo. Mpaka mdogo angu anashangaa huyu blaza vipi ila naona normol tuu..

Maisha ya mtandaoni kujianika mi ndo siwezi kabisa aiseee
Hii ni nature niliyonayo toka advance nilipo piga A ya phy na chem wala sikua mtu wa show off zaidi zaidi waliokuwa and anapost matokeo yangu ni wale ndgu wa karibu tuu..
You just did.
 
Baadhi ya mambo ambayo yakizidi sana huwa nayaona ushamba na ulimbukeni. Haya mambo mimi yamenipita mbali kabisa.

1. Kujipost WhatsApp status
Hata kama nitafanya jambo gani, hata kama nimepata nini cha mafanikio huwezi kukikuta status. Mwaka jana nimegraduate taaluma mbili tofauti lakini huwezi kukuta status. Acha status hata graduation sikuhudhuria(Japo sio ushamba)
Sijui nimenunua gari kali najisikia aibu sana kujipost. Hata picha tu ya gari sina, na zile zilizotumiwa na Mjapani nilishazifuta.

Kuna mdogo wangu alikuwa anapenda kupiga picha na gari anajipost. Nikamkataza.

Yule baby alikuwa anapenda kujiselfie na mimi halafu anajipost. Nikamkata kistaarabu tu baby don't do that. Hata kesho nikifanya harusi nadhani hakutakuwa na status.

Naona wenzangu wanapost matokeo ya watoto wao yaliyotoka jana. Mimi A tupu za wakwangu siwezi kuzipost, naona ulimbukeni. Ahadi ya zawadi niliyompa akipata A zote nitampatia, nitamtia moyo aongeze bidii na kumpeleka vacation ya kisima.

2. Kutumia elimu na kazi yangu kujiona bora
Nina mavyeti mengi tu lakini sio bora kuliko wengine. Sio bora kuliko mlinzi na mfagizi pale ofisini. Wakati wengine wakipita bila hata kumsalimia mlinzi na kusaini daftari getini. Mimi lazima nimjulie hali nijitambulishe. Hata akisema basi nenda tu, namwambia hapana nitasaini hapa na kule kwa Mkurugenzi nitasaini. Maana ndio utaratibu.

Tukiwa shamba mimi sio bora kuliko kibarua. Kwa hiyo msosi wa shamba utakula wote.
You just did.
 
Mkuu wewe kama mimi tuu
Kuna wanangu niliomaliza nao Telecom pale Cive walikua watu wa ku show off status ila mii wala

Nulipo piga electrical south africa wala hakuna ndugu aliyekua anajua an ni mtu wa kimya kimya..

Juzi nimeenda dubai lakini cha ajabu sijapiga picha hata kidogo. Mpaka mdogo angu anashangaa huyu blaza vipi ila naona normol tuu..

Maisha ya mtandaoni kujianika mi ndo siwezi kabisa aiseee
Hii ni nature niliyonayo toka advance nilipo piga A ya phy na chem wala sikua mtu wa show off zaidi zaidi waliokuwa and anapost matokeo yangu ni wale ndgu wa karibu tuu..
Ila we dogo akili zako unazijua mwenyewe, ndo kwanza upo chuo mwaka wa 2,
 
Back
Top Bottom