Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Mkuu wewe kama mimi tuu
Kuna wanangu niliomaliza nao Telecom pale Cive walikua watu wa ku show off status ila mii wala

Nulipo piga electrical south africa wala hakuna ndugu aliyekua anajua an ni mtu wa kimya kimya..

Juzi nimeenda dubai lakini cha ajabu sijapiga picha hata kidogo. Mpaka mdogo angu anashangaa huyu blaza vipi ila naona normol tuu..

Maisha ya mtandaoni kujianika mi ndo siwezi kabisa aiseee
Hii ni nature niliyonayo toka advance nilipo piga A ya phy na chem wala sikua mtu wa show off zaidi zaidi waliokuwa and anapost matokeo yangu ni wale ndgu wa karibu tuu..
Wewe MTU wa show off sana...ndo maana umetaja kila kitu chako hapa!!
 
Kila mtu anafanya kile kinachomfanya afurahi, huwezi kuita hobby za wenzako "ushamba" , ni kitu watu wanapenda kushare furaha na huzuni zao na jamii inayowazunguka na wala sio ushamba kama ulivyoiita mtoa hoja.

Labda ungesema tu hauna interest na kujitupia mtandaoni ila don't term others as washamba kisa wewe hufanyi.
Tatizo la mtu mweusi ni kutaka kuwapangia wengine cha kufanya. Mleta mada ndiye mshamba mkubwa.
 
Una wasema wanaoonesha mafanikio yao mitandaoni mimi nilichogundua ni kwamba na wewe unapenda ila huna guts… kwani hapa sasa hivi umetoka kufanyaje? Umetuambia yote kuhusu wewe kama wenzio na wewe umefanya hivyo hivyo umebadili tu mtandao wa KIJAMII
 
Baadhi ya mambo ambayo yakizidi sana huwa nayaona ushamba na ulimbukeni. Haya mambo mimi yamenipita mbali kabisa.

1. Kujipost WhatsApp status
Hata kama nitafanya jambo gani, hata kama nimepata nini cha mafanikio huwezi kukikuta status. Mwaka jana nimegraduate taaluma mbili tofauti lakini huwezi kukuta status. Acha status hata graduation sikuhudhuria(Japo sio ushamba)
Sijui nimenunua gari kali najisikia aibu sana kujipost. Hata picha tu ya gari sina, na zile zilizotumiwa na Mjapani nilishazifuta.

Kuna mdogo wangu alikuwa anapenda kupiga picha na gari anajipost. Nikamkataza.

Yule baby alikuwa anapenda kujiselfie na mimi halafu anajipost. Nikamkata kistaarabu tu baby don't do that. Hata kesho nikifanya harusi nadhani hakutakuwa na status.

Naona wenzangu wanapost matokeo ya watoto wao yaliyotoka jana. Mimi A tupu za wakwangu siwezi kuzipost, naona ulimbukeni. Ahadi ya zawadi niliyompa akipata A zote nitampatia, nitamtia moyo aongeze bidii na kumpeleka vacation ya kisima.

2. Kutumia elimu na kazi yangu kujiona bora
Nina mavyeti mengi tu lakini sio bora kuliko wengine. Sio bora kuliko mlinzi na mfagizi pale ofisini. Wakati wengine wakipita bila hata kumsalimia mlinzi na kusaini daftari getini. Mimi lazima nimjulie hali nijitambulishe. Hata akisema basi nenda tu, namwambia hapana nitasaini hapa na kule kwa Mkurugenzi nitasaini. Maana ndio utaratibu.

Tukiwa shamba mimi sio bora kuliko kibarua. Kwa hiyo msosi wa shamba utakula wote.
Kasome japo human psychology hata intro tu utajua hauko sahihi hata kidogo
 
Ukishaelewa maana ya mitandao ya kijamii. Hutaita mtu mwingine mshamba kwa sababu hajafanya kile unachofikiria wewe. Binafsi yangu hutakuta picha yangu status lakini sijawahi kuona shida watu wengine wanavyoshare moments zao kwenye status.

Jambo la kwanza uelewa mengine huitaji elimu ya degree kutofautisha JF na Whatsapp na uulize kwani kilichofanyika hapa kinatofauti gani na kile kinachoitwa ushamba.
Jamaa yeye ndo kaonesha ushamba, wanataka kuwa recognised kwa kutopost badala watulie wenyewe,
Kama hulipi bills za mtu na chochote anachofanya hakina madhara hakuna haja ya kuona wenzio ni washamba
 

Attachments

  • IMG-20241230-WA0002.jpg
    IMG-20241230-WA0002.jpg
    52.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom