Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Aminia sana, huo ndo uanaume sasa siyo kila siku mastatus WhatsApp kama shanga halafu yote picha za mtu
 
Ni kweli ujiposti status WhatsApp lakini bado una ego hata, hiki ulicho kileta kinaonesha wewe ni mjivuni, ni kama ulikua unataka kutuambia kwamba unamiliki gari na pia wewe ni msomi ungekua sio mtu wa kujionyesha ungekausha hata usingeandika huu uzi
 
Mimi kujiweka status ndio siwezi
Na kufanya graduation sijawahi..
Sio kama wanaofanya nawaona washamba HAPANA sipendelei tu sherehe
 
Kiukweli mimi status naweka, mfano 2024 nilivyopata CPA aisee nimepost picha zaidi ya 10, basi tu najiskia vizuri na wala siyo kumringishia mtu, ni part ya celebration
 
ila hapa amejianika aiseeeeh
 
Status Mara nyingi inaeleza mood ya siku husika, mf birthday n.k kwahiyo kupitia status nirahisi Sana kumsoma mtu kweny swala zima la utulivu wa akili yake.
Kupost na kufuta baada ya muda mfupi maana yake uwezo wake wa kufkria na kung'amua jambo ni mdogo. Kupitia status utakua tabia nyingi Sana za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…