Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Nimekupata vizuri.
Kama ndivyo basi hatuna serikali ya wananchi kwenye hili taifa.

Watu wanapigwa kwa sababu ya shida zao...sirikali kimya.
Mbaya sana.
Na jamaa ni matapeli.
Unajua kwanini ni matapeli!?
Kipindi unapewa taarifa za mkopo unaambiwa riba asilimia 10 ila ukija ku click mkopo unakuta makato tofauti na riba tofauti.
App ambayo kidogo nawapongeza ni Credit mkopo.
Wale niliwahi kukopa elfu 7 nikaambiwa nirudishe elfu 9.
Kidooochooo afadhali.
 
Yanayokukuta ndo yanayonikuta,kiufupi nshaamua siwalipi kama vipi ubaya ubwela. Unajua ni kwann siwalipi? Iko hivi.... nilichukua elfu 70 lakini katika simu ikaingia kama 57k afu wananitaka nilipe 90k baada ya wiki. Tatizo ni kua baada ya siku tatu zikaanza meseji kibao toka kwao,kesho yake wakaanza kupiga simu nikapokea,alooo huyo dada anavyoongea sio kistaarabu hataki kusikiliza lolote kama ananikaripia vile.
Nikasema kumbe ndo zenu sasa tuone,sijalipa hata mia wanapiga simu kwa namba tofauti naziangalia tu. Wakawapigia wadhamini wangu na wao nikawapanga nikawaambia wawaulize kwann kabla hamjampa hela huyo mtu hamjapiga kuniulia kama niko tayari kumdhamini. Hawajawapigia tena.
 
Back
Top Bottom