Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Sasa itasaidia nini wakishanitengenezea Hilo group la what's app??
Haina maana kwako kama wewe ni muokota makopo na mnywa visungura. Ila kama ni mtu mwenye heshima zake, una familia, una ndugu, una marafiki na watafutaji wenzako mnategemeana kwenye suala la uaminifu ujue hapo unapoteza credibility.

Kwa namna yeyote ile mimi siwezi jihusisha na mtu anakopa mikopo uchwara ya mtandaoni na anashindwa kulipa, anakubali kutangazwa kama mwizi. Kama hana aibu kwa wale jamaa sembuse kwa hela yangu mwenyewe ambaye sitomtangaza wala kumsumbua.

Mimi circle yangu kupelea hela ni suala la kawaida hivyo ni simu moja unaomba hela wala husemi unarudisha lini wala unaenda fanyia nini. Sasa leo hii nitangazwe tapeli wa mikopo umiza si nitaonekana mwendawazimu.
 
Usilipe achana nao zaidi ya kutuma message kwa namba za jamaa zako na vitisho viingi hawana cha zaidi.Nika ma Joka la kibisa.Hao ni matapeli wanafanya biashara haramu.Ndo maana ukiwauliza ofisi iko wapi hawakuonyeshi ! Hapo ndo ujue hao ni magumashi biashara wanayofanya sio ! We waulize ofisi iko ile uende.Wakikuonyesha njoo hapa unitag ! Watakutumia maneno meeengi ya vitisho lakini hakuna lolote !
 
Wanaorudisha ni wengi kuliko wanaotapeli na riba zao kubwa. Sasa hivi hapa Tz hakuna biashara yenye hela kama ukopeshaji. Wanaofikia level za microfinace wanapiga hela sana.
Ooh okay sawa, naona ina utapeli mwingi.....katika biashara ambayo siwezi hata kuithubutu ni hii yani huo mtaji wa kukopesha bora nkale kitimoto na bia, hapana asee.
 
Lipa kwanza halafu kopa tena.

Hapa lengo la kukopa tena ni Ili wao wakutafute wewe na siyo wewe uwatafute, maana ukirejesha halafu wakawa hawakudai, hawatakutafuta kamwe.

Wakikupigia waeleze kwamba mkopo uliopita walikudhalilisha, kwa hiyo utawapeleka mahakamani kudai fidia ya udhalilishaji maana walitoa siri zako za kifedha.

Waambie unawapa siku moja watume sms kuwa contacts zako zote ya kuomba radhi kuwa wewe siyo tapeli.

Wakishatuma sms za kukusafisha (utapata majibu toka kwa ndugu), basi Kaa kimya na usiwalipe huo mkopo wa pili.

Hapa utakuwa umewaingiza kwenye mfumo wako; kwanza, hawataweza tena kuwaaminisha watu kwamba wanakudai maana wameshajichanganya kwa kuomba radhi, pili, utakuwa umejilipa fidia ya udhalilishaji.

Baada ya hapo, hata wakipiga simu waambie hatudaiani.

Maana kama hawana ustaarabu kwako ni kwanini wewe uwe mnyonge kwao?
Hii haiwezekani
 
Ila mbona mikopo yenyewe ya tabu hivyo..
Hata kama ni shida tuvumilie jamani.

Nina rafiki yangu mmoja alitengenezewa group akiwa anaitwa tapeli na wameweka picha yake kilichoniuma ni kuwa amekopa elfu 50 ila walichompa ni elfu 32 baada ya makato inamaana yeye atatoa 29 maana wanamtumia kwenye simu. Alafu wanataka arudishe elfu 54
Dah kweli nchi ngumu sana unakopa 50 elfu tu inakutoa kamasi mbichi je ingekuwa milioni moja si utauza nyumba.
 
Back
Top Bottom