Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Ila mbona mikopo yenyewe ya tabu hivyo..
Hata kama ni shida tuvumilie jamani.

Nina rafiki yangu mmoja alitengenezewa group akiwa anaitwa tapeli na wameweka picha yake kilichoniuma ni kuwa amekopa elfu 50 ila walichompa ni elfu 32 baada ya makato inamaana yeye atatoa 29 maana wanamtumia kwenye simu. Alafu wanataka arudishe elfu 54
Bloangu si useme tu ni weweeeee

Anyway hatukatai wasitukopeshe,tunachotaka wawe regurated,wasajiliwe na BOT na riba zao pia ziwe regurated,sio kujiamulia tu
 
Namba ulizokuwa nazo kwenye simu wao tayari wanazo ... Watakukutengenezea hadi Group la Whatsapp na wataweka hadi picha zako na kiasi ulichokopa .. Yaaan Hadi unakopa tayari ulisha ruhusu wawe na namba zako zote na baadhi ya picha
Hqyari sana hawa watu...hatujuagi tu na haeajui cha kuchelewa bahati mbaya wala nini..umaskini na kukosa mishe timamu za kupata hela pale upatapo shida hupelekea kujilengesha kwa hawa..japo ni msaada ila utaratibu wa kukufanya ulipe ni very harrasing
 
Wiki iliyopita si ni li kopa pesa x ikawa natakiwa nirejeshe pesa nusu mara mbili ndani ya siku 14 yani kila baada ya siku Saba nirejeshe.

Sasa rejesho la kwanza lilikuwa jana ila cha moto nakipata! Aloo najuta, sio kwa meseji hizo ninazotumiwa!

Kwani nisipolipa watanifanya nini tofauti na kuwapigia wadhamini wangu?

Pia soma: Nape: Tumewaagiza TCRA wachunguze wale wanaodhalilisha watu waliowakopesha Mtandaoni
Jambo la kwanza kufanya futa app yao.

APP ni scam kwenye simu yako ndio wanatumia kufuatilia text messages zako, calls na picha kwenye gallery ya simu yako.
 
Jambo la kwanza kufanya futa app yao.

APP ni scam kwenye simu yako ndio wanatumia kufuatilia text messages zako, calls na picha kwenye gallery ya simu yako.
Nimeshafuta App Yao lengo ni kuepusha usumbufu huku nkiendelea kupambana Ili niweze kuwalipa pesa Yao taratibu
 
NAJUTA Mimi jamani najutaaa
Huna sababu ya kujuta.
1. Walipe
2. Waombe upunguze ulichonacho
3. Ilitakiwa kabla ya siku kufika uombe extension kuna kiwango unalipa
3. Kama nilivyosema hapo juu futa App na ondoa line uliyokopea kwenye smartphone. Ila kama unaona hakuna uwezekano wa kulipa. Hapa watakuwa na access na simu yako kuidukua.

Kwa sasa kama app ipo kwenye simu yako basi mnatumia wawili na wewe huna control nayo wala privacy. Almost kila kitu unachofanya kwenye simu wana uwezo wa kuona. Kama kutuma na kupokea miamala. Picha unazopiga na kuzituma kwa honey. Hao jamaa ni hatari mnoo ila usitishike.
 
Acha nao hao mimi wamenidai mpaka wamekoma...saivi wameniacha ...hawanitafuti tena ...washafanya kila kitu mpak group la WhatsApp waliniweka ila hawajanistua kwa chochote...we nuna na mambo yako mkuu
Ngoja niwakaushie ila nkipata pesa Yao nawalipa
 
Hawa jamaa wanadukua taarifa binafsi mfano sms unazotuma , wzup message pia, wanaingia ktk gallery ya picha zako.Basi wakianza kudai siku ya tano usipowalipa siku ya sita saa 12 asubuhi washaanza ikifika saa 7 mchana hujalipa wanaingia gallery wanachukua picha yako wanaandika na maneno ya kishenzi wanakutumia ,wanawatumia pia ulioandika wadhamini na baadhi watu uliwa save ktk contact zako ambao una mawasiliano nao mara kwa mara.Pia wakati wanakupigia bila we kujua wanaunganisha kwa kuwapigia jamaa ulio wa save ktk contact zako huku wanakudhihaki lipa deni jamaa zako wakati huo wameunganishwa wanaskia ! ni udukuzi wa waziwazi huwezi kujua mpaka jamaa yako akupigie simu akueleze mbona nimeskia hivi ?? ni kweli ??
Hawa jamaa ni wadukuzi wa hali ya juu.
Kuna wakati mwingine wanaingia wzup yako wanatafuta kama una message zozote zinazohusiana na mapenzi basi wanazi highlight kwa rangi kama vile kijani then wanakutumia ktk wzup yako ! manake wanakwambia wanajua siri zako ! hivo uwalipe ili wakufichie siri ! Hii ni blackmail ya hali ya juu.Hata wanapokutishia tutawambia ndugu zako wakulipie au tuta kuundia kundi la wzup wakuchangie ni Balck mail ya hali ya juu !
Wakati mwingine wanapokupigia kwa kuwa wanakuwa wengi ktk hizo ofisi zao unawaskia kabisa wanasema huyu lazima alipe leo mbona ana pesa kwenye simu ?? na wengine anawatumia ?? manake wanadukua mpaka mawasiliano yako na kiasi gani unakuwa nacho ktk simu hawa jamaa ni hatari sana !
Wanaangilia ktk contact list yako aidha kama mwanamume wanatafuta wakike walio ktk contact list yako ndo wanawatumia message zao na picha na kama we ni KE wanatafuta wa kiume ambao wanahisi ni wapenzi wako.Au wakijua huyu ni boss wako basi wanae.Yaani wana study contact list yako utadhani ya kwao na wana monitor mawasiliano yako na wakipata tu loop hole wana take advantage.Mfano wakijua huyu ndo mpenzi wako kutokana na mawasiliano ya simu basi watakuandama kumpelekea message zao za kishenzi kuwa we tapeli na mwizi wa mitandaoni.
Kwa hiyo kuweni makini sana.Wana uwezo wa kusoma message unazopokea na kutuma kwa wakati kiufupi wanajua kila kitu unachokuwa unafanya wanapokuwa wanakufuatilia ulipe deni lao.Wanaingia ktk picha galleryy wanatafuta picha ambazo hazifai kuonyesha hadharani wanakutumia kuwa usipolipa watazinclude ktk wzup group watalounda kwa ajili yako.
Mi nashangaa vyombo vya serikali vimekaa kimyaaaa !!
Hata vyombo vya habari kama TV na magazeti vimekaa kimyaa !
Magazeti ya uchunguzi hii ni habari ambayo kama mtaiandika kwa kina jamii itafunguka na serikali itachukua hatua ktk hili janga.Chukueni hatua wakati ni sasa !
NB:Naweza kuandika kitabu kuhusiana na hawa jamaa kwa leo inatosha
 
Hii ipoje kisheria, kumdhalilisha mtu kimtandao si ni kosa la jinai? Kukopa na kuchelewesha deni ni kosa la madai
Je mkipambana mahakamani nani ataumia? Akijitokeza mtu mmoja akawanyoosha hata hiyo mikopo wataacha kukopesha
Hawana uwezo wa kupeleka wakopaji mahakamani. Kuna taratibu nyingi za kifedha na ukopeshaji wanakiuka.
 
Hawana kauli za kistaarabu.
Mwanzo walinitisha wakisema ooooh tutapost picha zako nikasema hawanijui.
Nikafuta taarifa zangu muhimu zote.
Kesho yake wananitafuta kiupole,aisee sikuwasikiliza na laini nikavunja.
Walinitusi sana wale mbwaa.
Wenye ukauzu kama wewe ndo mnafaa kwa hao watu, ila kwa jinsi nilivyo bahili siwezi kopa elf 50, unipe 38 halafu nilipe elf 60🤣hiyo ni biashara kichaa ndo maana wanadhulumiwa wanaishia kutumia mbinu za kudhalilishana ili walipwe
 
Back
Top Bottom