Najuta kuhamia kwangu Kerege

Safi sana mkuu, naelewa sana mkuu. Sikumbuki lini nilinunua hoho, ngogwe, mchicha, mapapai na kuku wa kienyeji. Weekend kama hivi unatumia mda wako kwenye bustani unaenjoy maisha.
 
Mshukuru mungu sana kwanza kwa kujenga halafu mjini hakuna mbali ...hebu sikia hii
Mwaka 1997 marehemu mama yangu alihama sinza kajenga kitunda kulikuwa hakuna gari hata moja tulikuwa tunapanda malori ya mchanga.kipindi hicho kiwanja chetu karibu heka tulinunua laki 3.mama yangu alikuwa anasema amenunua basi tu kwa sababu hela haina kazi
Ila baadaye alijutia sana kwa maana huyo mzee aliyetuzia alitaka laki 5 atupe heka nzima pesa mama alikuwa nayo leo hii kitunda kuna lami kumeendelea hakuna kiwanja cha 1m wala 2m labd uende mbondole mbele mji hauchelewi kukuwa..kuwa mpole kuuza nyumba zama hizi ni kucheza kamari
 
Cha msingi kuongeza kipato lima mboga mboga,fuga kuku wa mayai hasa wakienyeji, ardhi ya huko hata matunda ina kubali asubuhi unakuja na mzigo wako hutokosa wateja tena wafanyakazi wenzako ,mwanzoni utaona aibu ila baadaye utapata hela sana...ikwezekana fuga na ngombe wa maziwa utapata pesa ya kutosha maisha ya taenda tu!!!
 
Umeongea point mno mkuu, Mimi nilinunua shamba sehem flan kijijin huko,

Shamba lilikuwa linauzwa 1.2m kubwa mno yan, lakin watu wakaanza kusema oooh umepunjwa mara shamba lenyewe baya miti mingi, yan watu wakataka kunipoteza kabisa.

Nikaenda kuchukua ushauri kwa mamkubwa alichoniambia ni hiki,

"mwanangu ardhi huwa haipunji" nikajipa moyo, basi nikaweka vibarua shamba likasafishwa aiseee nilipiga mahind msimu huo yan pesa ilirudi na faida nyingi tu.

Had sasahivi hilo shamba wanalima tu huko ndugu na kwa sasa thaman yake ni kubwa mno.

Mwaka jana alijitokeza jamaa mmoja kigogo akataka anipe 7m nilikataa na siwez kuuza.
Lai yangu kwa mtoa uz n kwamba we vumilia tu wala usiingie tamaa ukauza eti uhamie mjini ufanane na wahindi utapotea jipe miaka hata mitano mbele utaona mji unavokusogelea.
 
wewe mjanja
unajua kuna Mikoa Mashamba huwa HAWAUZI na Nchi jirani zetu huwezi pata eneo
sasa jamaa yupo DSM wanamcheka Je Wahindi walionunua Kilosa, Kimamba Gairo mbona wanalala maghorofani Canada
 
Ardhi ni rasilimali adimu sana ,mimi na kiwanja buyuni block 28 nilinunua 1.8m watu wangu wa karibu waliniambia nimepigwa sijuii vile viwanja vimepimwa vina hata.mwak jana jamaa alifika 15m nikakata mwaka 2014 jamaa alifika 10 kikagoma ardhi inapanda sana kila mwaka.huyo akivumilia hadi 2025 na amini hatouza tena
 

Daah nimekumbuka ile mansion ya Mzee Mengi kule Machame,mt.kilimanjaro unauona hapo pembeni yako full ubaridi na zile mvua mvua za kule daah kutoka getini mpk unaingia ndani bonge la distance.

Yaani ukicheki mazingira tu husika unapizi kwanza kwa furaha,90% tunaishi kwny vibanda kama tunavyosemaga wenyewe(nimejenga kibanda changu huko kivule,karibuni).

Dar ni pa kijinga sana,weather/foleni/mpangilio wa makazi ni hovyo hovyo ni vile basi tu no way out lazima tuishi.
 
Endelea kujidanganya. Zama za Ardhi kupanda thamani ziliisha mwishoni mwa 2016. Kama hukuuza nyumba/ardhi enzi hizo andika maumivu. Madalali wanaisoma namba. Pita Masaki/Oysterbay/Upanga uone apartments zilivyo wazi/Matangazo ya "FOR LEASE" mpaka yanapauka. Kuhamia Dodoma nako kumefanya Dar iwe kama imepigwa Bomu
 
Sasa unawezaje kwenda kukaa KM 50+ nje ya mji wewe ni mstaafu au? Bunju tu hapo ni 40 km hadi mjini, halafu ukute una gari ya 1500 na unalalamika kwenda na kurudi wiki tu au kwa mwezi unajikuta unatembea 3500km kama vile unaenda congo vijana wajanja wote wanaenda Kinyerezi mkuu
 
Chief Namiliki Nissan Fuga Full Stress. Kuna wakat ikizingua lazima kudamka saa 9 nimpigie bodaboda aniwahishe stendi ya daladala za Bagamoyo-Nyuki niunge tena mpaka Makumbusho-Posta. Yaani safari kama unaenda Guanzghou kununua malonya
 
Chief Namiliki Nissan Fuga Full Stress. Kuna wakat ikizingua lazima kudamka saa 9 nimpigie bodaboda aniwahishe stendi ya daladala za Bagamoyo-Nyuki niunge tena mpaka Makumbusho-Posta. Yaani safari kama unaenda Guanzghou kununua malonya
Mkuu hapo ulifeli mimi katika vigezo vyangu vyote napima Km toka kazini na ninapokaa nashukuru Mungu nimepata kiwanja sehemu toka kazini hadi nitakapo hamia ni 23-25km kwaio hapo najua wese la 55,000 kwa wiki linanisogeza vizuri kabisa, kuna kiwanja mimi kipo mapinga ni 3km toka barabarani wala hata sijashughulila nako nje ya mji wanakaaga wastaafu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…