Najuta kuhamia kwangu Kerege

Wakati naanza kazi niliapa kuwa sitajenga Zaidi ya KM 20 toka ilipo Ikulu na kama ni mkoani sitajenga Zaidi ya KM 10 toka makao makuu ya mkoa husika
 
Hujaelewa kumbe... Anaweza kuwa na kiwanja huko lakini sio kukaa huko
 
1. Kwasababu hujui thamani ya muda, ndio maana unaona sawa kukaa masaa 3 kila siku.

2. Hujui thamani ya pesa, hiyo hela unayoiweka kwenye kiwanja usubiri ukiuze miaka 30 mbeleni ungeizungusha kutengeneza cashflow ambayo utajenga nyumba mjini hapahapa.

Binafsi nina nyumba mbele ya tegeta sijahamia bado kwasababu ni mbali na shughuli zangu. Nafikiria kuiuza.
 
Labda sikueleweka..ishu hapa sio jirani akiniona nimeshika chuma la eicher atasemaje .ishu ni yale mazoea mzee baba!hapa hakuna cha elimu ya kujitmbua wala nn...!kuna kaulemavu kapo sana ukizoea kutembelea gari!wenyewe wanakajua!
Me nimekuelewa usijali mkuu
 
Cha muhimu hapo, huko kerege sio pabaya fanya namna uanzishe mradi utakao fidia gharama za usafiri. Mantiki ya watu kukaa mbali na mji ni ili waweze kufanya mambo yasiyofaa kufanyika mjini.

Huwezi kukaa kerege eti una ka plot 20 kwa 20m. Hapo piga ufugaji wa kuku, samaki pia watu wanafuga huko, kitimoto kama imani yako inaruhusu. Uza gari kama ni saloon nunua pick up ikusaidie kupiga ufugaji.

Pia hapo mtaani kwako kama bado hapajachangamka toka barabarani baada ya kuwa fit kiuchumi fungua hapo kibiashara kidogo mfano fyatua tofali, fungua hardware uchwara, fungua duka la pembejeo za kilimo na vyakula vya mifugo piga hela. Kuajiriwa peke yake haitoshi.

Ni hayo tu Mkuu.
 
Kusema ukweli wangu Mimi binafsi hata Bunju siwezi kujenga kwa ajili ya kuishi labda nijenge Guest house, ndio sembuse kerege?

Tutumie akili zetu vizuri, kuna maeneo ukinunuwa ni maandalizi ya maisha ya ustaafu utakakapokuwa huna safari za kutoka kila siku, unataka eneo kubwa kwa ajiri ya ufugaji na makazi ya uzeeni.

Kwenda kununuwa kiwanja chs 20 kwa 20 Kerege ni matumizi mabovu ya akili.
 
Asiwadanganye mtu kuishi kwako raha bwana hata kama ni porini kwako hapawezi kuwa mbali bwana ni kujiongeza tu.

Kwakuongezea tu, USIUZE NYUMBA utachanganyikiwa. Kama umeishiwa uza gari. Kula msoto kidogo akili ikae sawa utapata way out tu. Ungekuwa na NOAH ungekuwa unakula vichwa asbh na jioni wakati wa kwenda na kutoka kazini mafuta yangejinunua yenyewe tu.

Cha muhimu fikirisha kichwa sijaona kama unachangamoto wewe, usilaze kichwa.
 
asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).
Hongera kwa kujenga, nyumba ni asset kwako ni kwako tu, lakini pia hongera kuwa na gari, chukulia kuwa hayo ni matumizi kama kununua nguo na vinginevyo,
 
Kuwa mvumilivu, BRT Phase 4 inakuja soon utakuwa unaserereka tuu mjini Dk 0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…