Najuta kuhamia kwangu Kerege

Unajidanganya, maisha ya kuamka saa 10 usiku ili saa moja asubuhi ndio ufike mjini kati huu ni uwendawazimu kwa Tanzania, kuna nchi nimeishi train za umeme ndio usafiri wa kwenda makazini na mtandao wa reli umepita kwenye makazi mengi, ukikaa mbali na mjini hakuna tatizo lakini si kwa Tanzania acha kudanganya wenzanko.

Watu wenye busara akiwa na million 50 ananunuwa nyumba karibu na town unang'arisha then unaenjoy maisha.
Unakaa sehemu hata kuhudhuria harusi huwezi unawaza stress za muda wa kurudi usiku, disco huwezi kwenda haya ni maisha gani sasa?
 
Ur very Correct my Broder
 
Nikwambie kitu mkuu, usiuze nyumba uza gari nunua pikipiki boxer au mahindra
 
Haya mawazo sio ya mtu mkomavu,

1. Nyumba ya m50 mjini unaongelea mji upi?

2. Harusi hata kama inafanyikia morogoro ikiisha hata saa 8 usiku kama una usafiri wako private hakuna tatizo lolote.

3. Ulivyoongelea Disco imenipelekea kutambua uchanga wako. Huenda tunabishana na watoto wetu huku.

You have to be man enough to own a house in Dar es Salaam.
 
Mbona hujamshauri kuhusu tatizo la vibaka ?
 
Disco kuna nini huko!?
 
Hiyo nayo inaitwa nyumba?
 
kuna dada kaacha kazi ya mshahara laki 3 masaki.
Ruti ya mapinga-masaki sio kazi ndogo.
Hela yote ya mshahara inaishia kwenye nauli.
 
Inawezekana wewe umekomaa vigimbi lakini siyo akili,

Nyumba ya million 50 ni Dar na kwa taarifa yako Mimi real estate ndio fani yangu.

Kutoka harusini saa 8 usiku kudrive km 50 huu nao ni zaidi ya uwendawazimu.

Kama umezaliwa kijijini Nyalugusu ni lazimà ushangae swala LA outing, kila MTU na hobby take mwingine disco mwingine live band mwingine matamasha.
 
Kwako ndo unaona ujanja umemaliza hapo ukitoka out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…