Najuta kuhamia kwangu Kerege

acha sound yaani ujenge mjengo kama huo ushindwe na mafuta ya gari, kuna tatizo mahala sasa kama umepaki ndinga mbili nje si uuze moja , by the way hutakiwi kuuza nyumba boya wewe, uza gari nunua bajaji ya biashara iwe inakuwahisha stendi kula daladala, ukirudi jioni inakurudisha home ikiwa imeshakula vichwa na hela inaingiza
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=)...
Huna sababu ya kuhama mkuu, kwako ni kwako na kuna heshima yake, kama kifedha haupo vizuri kopa kutoka Benk na tumia hiyo nyumba kama collateral , ukipata fedha ongeza urefu wa ukuta ongezea kama course 4 na juu weka razor wire.

Badilisha gari uchukue yenye engine ndogo kama IST iliyopo in good form inaweza kwenda hadi 18 km kwa lita, na maisha yaendelee.
Chukua nduguyo kutoka kijijini kwenu abakie ndani mchana kwa ajili ya usafi na ulinzi
 
Jitahidi kushauri bila kutukana ama kukashifu, unaweza kutumia lugha ya staha na ujumbe ukafika
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=)...
Serikali ikijenga Bandari ya Bagamoyo kama walivyosema , na kiwanda cha sukari cha Bakhresa kikianza uzalishaji hayo maeneo yote ya Mapinga, Zinga , Kerege nk yatainuka kwa kasi
 
Bas mm nna wazo nikizichanga nijenge kerege for life!...nilipewa kiwanja huko!bt mbona si uswahilini kule mzee??
Ndo nami nashangaa, Kerege ipi hiyo imekuwa uswazi? Tena kilometer 8 toka barabara ya lami..
 
Sure
 
Umbali mkubwa mno about 42 km one way!! Kibaby Walker changu unatumia lita nane kwa siku, sawa na elfu 21. Too expensive! Kama unatumia gari kubwa kidogo cc 2000 si shughuli pevu mzee! Nakushauri Nunua Noah uwe unakula vichwa asubuhi unavyoenda job na jioni muda wa kurudi, hutaumia tena kwenye mafuta.
 
Hapo unampa moyo tu kwanza anakazi ya kuamka sa 8 kila ck ilihali kwake atakua anaingia si chini ya sa 4. Huko hata akisema auze hawez pata mteja labda abahatike kupata mstaafu ambaye anahitaji kupata fresh air ambaye atakuwa akifanya tu shuguli zake kuzunguka maeneo anayoishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…