Mkuu jumba kama hili kibaka anaingiaje? Unashindwa weka germany shepherd hata wa 2 tu unaendelea na shughuli zako? Majibu utayaonaWakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).
Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.
Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Joshua_ok[emoji15]Waswahili tumejaa mahangaiko
Njoo nikupe dawa ya wezi ya kinigeria zipo kibao zinazo changanya wezi!! hata mbwa unamchanja anakuwa km fisi!!Niliweka wakawapa sumu
Bei gani na anakuwa kama Fisi kivipi mkuu?Njoo nikupe dawa ya wezi ya kinigeria zipo kibao zinazo changanya wezi!! hata mbwa unamchanja anakuwa km fisi!!
Ndo hapo utumie dawa sasa!! yaani weye ukija kwangu na wazo la kuiba utaona fisi mkubwa ajabu...anakubwekea kwanza utashangaa nii hii?Bei gani na anakuwa kama Fisi kivipi mkuu?
Utaratibu wa kuipata.Ndo hapo utumie dawa sasa!! yaani weye ukija kwangu na wazo la kuiba utaona fisi mkubwa ajabu...anakubwekea kwanza utashangaa nii hii?
Nina maoni haya: Kujenga na kuishi sehemu ya mbali na mji kama hiyo yako kwangu mimi ni jambo zuri sana. Na zaidi niseme sehemu za Kerege ni nzuri sana na kuna hewa safi na mtu unakuwa mbali na rabsha za mjini. Na kingine ni kuwa una uhuru wa kufanya mambo mengi kama bustani na ufugaji. Changamoto yake kubwa ni security. Maeneo kama hayo yanakuwa hatari hasa wakati wa usiku kwa sababu hakuna watu wengi. Kuishi maeneo kama hayo inatakiwa mtu uwe na uwezo mkubwa. Vitu kama gharama za usafiri visiwe issue, na uwe na ulinzi madhubuti (japo majambazi wakidhamiria wanakuwa huru zaidi kwa sababu ya kukosekana msaada wa haraka). Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alijenga karibu na shule ya Bunju B. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema amehamia porini. Leo hii hakuna anayemcheka na eneo limekuwa mji. Ushauri wangu: Hayo maeneo ni mazuri na siyo muda mrefu sana kutakuwa mji wenye watu wengi. Kama huna shida sana usiuze. Tafuta mbinu nyingine tu za kujikwamua na baadae utaona faida yake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Njoo nikupe dawa ya wezi ya kinigeria zipo kibao zinazo changanya wezi!! hata mbwa unamchanja anakuwa km fisi!!
Duh, 6km toka home hadi moro road, then daladala hadi town. Nilikuws nadhani naishi shamba, nate natengua kauli rasmi.Yaani hapo kerege unaona mbali Mimi nipo kibaha kwa mfipa na kutoka hapo kwa mfipa mpaka kwangu 6km ,natoka kwangu Asubuhi na kipikipiki changu nakuja hadi morogoro road naiacha hapo sheli napanda daladala naenda town nikirudi naichukua narudi home kwenye hewa safi
Doh[emoji16]Yaani hapo kerege unaona mbali Mimi nipo kibaha kwa mfipa na kutoka hapo kwa mfipa mpaka kwangu 6km ,natoka kwangu Asubuhi na kipikipiki changu nakuja hadi morogoro road naiacha hapo sheli napanda daladala naenda town nikirudi naichukua narudi home kwenye hewa safi