Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

Mkuu jumba kama hili kibaka anaingiaje? Unashindwa weka germany shepherd hata wa 2 tu unaendelea na shughuli zako? Majibu utayaona
 
Kama unaenda kujenga sehemu ya mbali hivyo hakikisha unapata eneo kubwa kuanzia ekari moja ili ufanye na shughuli zingine za bustani na ufugaji zikupunguzie kidogo gharama za maisha. Mie habari za kwenda kujenga nje ya mji then unaishia kupata kiwanja sijui 25 kwa 30 hizo sizitaki kabisa bora nikomae mjini
 
Bei gani na anakuwa kama Fisi kivipi mkuu?
Ndo hapo utumie dawa sasa!! yaani weye ukija kwangu na wazo la kuiba utaona fisi mkubwa ajabu...anakubwekea kwanza utashangaa nii hii?
 
kama unahitaji kuishi nje ya mji kubali kuendana na uhalisia maisha ya mjini ukiyaishi nje ya mjini utatumia gharama kubwa kuishi
 
Yaani hapo kerege unaona mbali Mimi nipo kibaha kwa mfipa na kutoka hapo kwa mfipa mpaka kwangu 6km ,natoka kwangu Asubuhi na kipikipiki changu nakuja hadi morogoro road naiacha hapo sheli napanda daladala naenda town nikirudi naichukua narudi home kwenye hewa safi
 
Nina maoni haya: Kujenga na kuishi sehemu ya mbali na mji kama hiyo yako kwangu mimi ni jambo zuri sana. Na zaidi niseme sehemu za Kerege ni nzuri sana na kuna hewa safi na mtu unakuwa mbali na rabsha za mjini. Na kingine ni kuwa una uhuru wa kufanya mambo mengi kama bustani na ufugaji. Changamoto yake kubwa ni security. Maeneo kama hayo yanakuwa hatari hasa wakati wa usiku kwa sababu hakuna watu wengi. Kuishi maeneo kama hayo inatakiwa mtu uwe na uwezo mkubwa. Vitu kama gharama za usafiri visiwe issue, na uwe na ulinzi madhubuti (japo majambazi wakidhamiria wanakuwa huru zaidi kwa sababu ya kukosekana msaada wa haraka). Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alijenga karibu na shule ya Bunju B. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema amehamia porini. Leo hii hakuna anayemcheka na eneo limekuwa mji. Ushauri wangu: Hayo maeneo ni mazuri na siyo muda mrefu sana kutakuwa mji wenye watu wengi. Kama huna shida sana usiuze. Tafuta mbinu nyingine tu za kujikwamua na baadae utaona faida yake.

Kikubwa apangishe na hella ya kupangisha aitumie kuongezea kupanga mjini
 
Yaani hapo kerege unaona mbali Mimi nipo kibaha kwa mfipa na kutoka hapo kwa mfipa mpaka kwangu 6km ,natoka kwangu Asubuhi na kipikipiki changu nakuja hadi morogoro road naiacha hapo sheli napanda daladala naenda town nikirudi naichukua narudi home kwenye hewa safi
Duh, 6km toka home hadi moro road, then daladala hadi town. Nilikuws nadhani naishi shamba, nate natengua kauli rasmi.
 
Yaani hapo kerege unaona mbali Mimi nipo kibaha kwa mfipa na kutoka hapo kwa mfipa mpaka kwangu 6km ,natoka kwangu Asubuhi na kipikipiki changu nakuja hadi morogoro road naiacha hapo sheli napanda daladala naenda town nikirudi naichukua narudi home kwenye hewa safi
Doh[emoji16]
 
Back
Top Bottom