Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

unnamed.jpg
 
Tatizo la kujenga nje ya mji hata ukisema upangishe hiyo nyumba huwezi pata mpangaji,we unafikiri nani akapange kilomita zaidi ya 35 kutoka town ni ngumu.

Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi.

Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni
 
Back
Top Bottom