Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Nunua pikipiki mkuu, hutojuta
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Ulihamia kipindi hicho hicho cha JK au hivi majuzi?
 
Dada angu Mane, hebu njoo inbox unipe mchongo, unapataje hiyo 200K au wewe trafiki nini au una michongo yako inahusisha rushwa rushwa hivi, i love you kitambo sana
Kweli kila mtu anawaza ajuavyo yeye...yaan nipewe laki 2 kwa mwezi??hapana...!ila kuna biashara kichaa sana...labda ujenge nyumba ukopee mkopo mzuri benk...mwee huyo laki 2 mm naipata kwa siku 1!nah!
 
Tatizo la kujenga nje ya mji hata ukisema upangishe hiyo nyumba huwezi pata mpangaji,we unafikiri nani akapange kilomita zaidi ya 35 kutoka town ni ngumu.

Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi.

Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni
Uko right nimenunua Kiwanja Pongwe tanga mil 1.8 sqm 600 ni km 18 toka city centre Kiwanja kimepimwa kabisa
 
Mkuu soko la nyumba kwa sasa limeshuka sana kwa mfano kinondoni kwa pinda kuna nyumba mpaka za laki sita achilia mbali tabata achilia mbali makumbusho uko kote ni karibu na posta not less than 10 min upo kazini au nyumbani na muda wa kupumzisha akili ifikirie vitu vingine upo.
Kerege nadhani ata kama utakua na mafuta ya kuchoma kila siku bado nadhani hautakua na muda wa kufaid maisha kwa maana ya ya kwamba jioni ukifika homu itakua arrnd saa nne na kutoka hom asubuh ni saa 12 sharp hapo hamna maisha ni utumwa.
Panga hata chumba kimoja kino au sinza then ijumaa unarudi kerege and jumatatu anatokea atleast uifaid nyumba yako kipindi cha wknd
8 km from bagamoyo road ata mpangaji labda kama kuna mradi ndo utapata wapangaji otherwise supply ya nyumba mijini kwa ss ni kubwa mtu hana sababu ya kupanga nje ya mji
Kwanini nyumba za kupangisha zimeshuka bei tofautu na kipindi cha kikwete? Leo maeneo ya sinza, kijitonyama, kinondoni, nyumba zimeshuka bei alaf madalali wamekuwa wachache
 
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
Well said
 
Sawa ardhi ni mali lakini malengo yake ya kukwepa kodi ya pango mjini hayajatimia kwa sasa. Kaenda kununua mbali mno haimsaidii. Labda kama angenunua huko kwa malengo ya kufuga lakini si makazi wakati shughuli zake mwenyewe ziko posta mpya. Hivyo mimi namshauri eneo hilo alifanye la mifugo ajipange atafuta karibu apange baadaye anaweza kuja kupauza kwa bei nzuri tu
Ameshasema kuna vibaka, mifugo itapona?
 
sawa lakini asijutie
mm nitamtafuta @ joshua_ok aiuzie maana kuna mdogo wangu mwaka 2010 alinunua pori ndani kilomita 5 kutoka Kibanda cha Mkaa Kimara kabla ya Mbezi Louis wanajiita Makao Mapya, leo kuna Makanisa na Mahoteli, kuna Shule za Bweni nk
Lengo asiweke kukwepa Kodi aweke km Rasilimali
MMikoani ndio hakufai kabisa maendeleo yatachelewa kwani km Dodoma viwanja ni milioni 15 Moshi na Arusha ndio hakuna kabisa ni vya urithi
kwa hiyo ajifunze Ardhi haichezewi
hapa nina safari ya kuhamia Kilosa hata miezi 6 Waziri Lukuvi kaachia maekari huko, najua sitapewa ila nitanunua na hicho cha KEREGE naingia PM yake
Safi kabisa
 
Back
Top Bottom