Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

sawa lakini asijutie
mm nitamtafuta @ joshua_ok aiuzie maana kuna mdogo wangu mwaka 2010 alinunua pori ndani kilomita 5 kutoka Kibanda cha Mkaa Kimara kabla ya Mbezi Louis wanajiita Makao Mapya, leo kuna Makanisa na Mahoteli, kuna Shule za Bweni nk
Lengo asiweke kukwepa Kodi aweke km Rasilimali
MMikoani ndio hakufai kabisa maendeleo yatachelewa kwani km Dodoma viwanja ni milioni 15 Moshi na Arusha ndio hakuna kabisa ni vya urithi
kwa hiyo ajifunze Ardhi haichezewi
hapa nina safari ya kuhamia Kilosa hata miezi 6 Waziri Lukuvi kaachia maekari huko, najua sitapewa ila nitanunua na hicho cha KEREGE naingia PM yake
Positive mind
 
Huu uzi nimeingia kiutani utani ila nimepata kitu kikubwa sanaa
Nilikua naelekea kula za uso soon...
Ngoja nirudishe majeshi nyumaa
pesa zenyewe kuzipata shida halaf nicheze mchezo wa kubeti nibetuliwe....
Sema m naona kila upande una point...
Cha msing hapa ni kulala kwenye ka duka kangu...
asanteni wachangiajii.....
 
Mkuu usichulie poa, huko mikoani na vijijini ndio hela ilipo.. Dar watu wamekaba kila fursa, unahitaji mtaji wa kutosha kuingia kwenye mbilingembilinge za Dar..

Kahama,Geita, Katoro,Nzega hiyo miji mzunguko wa hela ni mkubwa na kama unacheza karata zako vizuri uwezo wa kuingiza 200K kwa siku upo... Hiyo 200K mbona hata Dar au Mwanza ukicheza draft yako vizuri unaipata??
[/QUOTE


Ww samurai unataka uwatishe watu kw porojo zako eh😅😅!mie nimeandika tu...!..hakuna kitu km hicho bwana wee..!
 
Nina maoni haya: Kujenga na kuishi sehemu ya mbali na mji kama hiyo yako kwangu mimi ni jambo zuri sana. Na zaidi niseme sehemu za Kerege ni nzuri sana na kuna hewa safi na mtu unakuwa mbali na rabsha za mjini. Na kingine ni kuwa una uhuru wa kufanya mambo mengi kama bustani na ufugaji. Changamoto yake kubwa ni security. Maeneo kama hayo yanakuwa hatari hasa wakati wa usiku kwa sababu hakuna watu wengi. Kuishi maeneo kama hayo inatakiwa mtu uwe na uwezo mkubwa. Vitu kama gharama za usafiri visiwe issue, na uwe na ulinzi madhubuti (japo majambazi wakidhamiria wanakuwa huru zaidi kwa sababu ya kukosekana msaada wa haraka). Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alijenga karibu na shule ya Bunju B. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema amehamia porini. Leo hii hakuna anayemcheka na eneo limekuwa mji. Ushauri wangu: Hayo maeneo ni mazuri na siyo muda mrefu sana kutakuwa mji wenye watu wengi. Kama huna shida sana usiuze. Tafuta mbinu nyingine tu za kujikwamua na baadae utaona faida yake.
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Oo
 
I tend to differ lakini unaweza kuwa na maana kama unamaanisha unependa vitu. Yaani vitu vinakuendesha wewe badala ya kuviendesha. Jaribu kubadili mfumo wa kufikiri. Imenisaidia sana


Maisha nnayoishi sasa nna zaidi ya mwaka sijui kitanda ni nn..nalalia godoro la wanafunzi lile dogo la mwisho...maisha yanasonga sana tu...niliwah hisi siwez ishi bila hvyo vitu..lakini kumbe nilikua najidanganya...!am very ok..sema nikirudi mjini ndo naishi hvyo kupoza ubongo😅!nakuelewa sana!.asante pia
 
Wahindi si wapuuz kujibanza kwenye nyumba za msajili
Wanaakili sana, wao nyumba ina maji na umeme 24/7, bafu na vyoo viko connected na sewage system hawawazi vyoo kujaa.
Usalama wa uhakika, barabara nzuri na hawasafiri mwendo mrefu kwenda kufanya shughuli zao.
 
I live almost 30km from city centre, dadeq bajeti ya mafuta kwa mwezi ni kodi tosha. Ukijumlisha foleni ya Morogoro road ndio usiseme, thank goodness barabara inapanuliwa so huenda in the near future mambo yakabadilika.

Naelewa unachopitia...
 
nilidhani unasema Milioni 13 kumbe milioni 1
Dodoma huku unapata eka moja porini kilomita 18 kutoka mjini kwa 1,3M, kiwanja kinafika 20m maeneo ya kujenga, ambayo joshua_ok anafananisha na KEREGE
mm nitafutieni kiwanja aua shamba iwe Kibaha, Chanika au Bunju najua barabara zipo
Magari yatatumia gesi itakuwa rahisi tu
 
Siwatishi naelezea uhalisia wa hayo maeneo ukiwa mpambanaji kweli na ukalicheza draft lako vizuri.. 200K/day haiwezi kupatikana bila kuituma hela ikuletee na kuisimamia ikuletee hiyo 200K. Kuna vitu huwezi kuongea humu tuishie hapa...
 
Pamoja na kuishi nje ya mji, umbali kutoka kazini na home, siwezi hata siku moja kufananisha na upangaji, headache za kupanga sio kabisa.

Huku mtu kama unapenda vikazi vidogo hutanunua mbogamboga, utakamata kuku na kumkata shingo mwenyewe, utakula mapapai yako mwenyewe na ile hewa fresh utaipata kila siku.
 
Siwatishi naelezea uhalisia wa hayo maeneo ukiwa mpambanaji kweli na ukalicheza draft lako vizuri.. 200K/day haiwezi kupatikana bila kuituma hela ikuletee na kuisimamia ikuletee hiyo 200K. Kuna vitu huwezi kuongea humu tuishie hapa...


😅😅..mie nimechakaa balaa...kwakweli bora ukae kimya! Tuna kauvivu kakutoka nje uone unataka tafuniwa tu..hela haiwez mfata mtu wa aina hii kamwe..!never!
 
Back
Top Bottom