Kujenga nje ya mji kuna kanuni zake zitazokufanya ufurahie maisha hayo.
1. Hakikisha una eneo la kubwa kutosha ujasiriamali si unakaa nje ya mji then umejibana kama unakaa Tandale.
2. Fanya uzalishaji mdogo mdogo, hakikisha hela ya kula na mafuta inatokea eneo unaloishi mf. unafuga mifugo mbali mbali kama kuku, bata, mbuzi na hata kanga na njiwa.
Pia, lima lima kwa kutumia mbolea za mifugo unayozalisha mf. mboga mboga, mazao ya muda mfupi madawa kama mlonge na matunda na uyoga na pia kufuga kambale kwenye mifuko.
3. Tumia usafiri utaokuzalishia, wengine wanalalamikia gari inachoka lakini amini usiamini hutagharamikia mafuta na hata shida ndogondogo zitatuliwa na mapato yatokanayo na usafiri huo huo hasa ukitumia gari zenye siti nyingi kama noah, alphard, hiace, etc. Usitumie gari ndogo kama sienta, cube cubic au spacio hizo zinakufa haraka sababu zinaelemewa mno.
4. Ishi kwa kusoma timing ya foleni ya barabara unayotumia, mfano unaweza kutoka kazini saa kumi jioni lakini ukakuta barabara haipitikia kwa foleni ila ukitoka kumi na moja kamili tu unakuta ishafunguka.
5. Hakikisha unajenga nyumba kiuchumi, ili kadiri mji unavyokua unaweza kubalisha na kuweka appartments ( kuna Mzee anajuta katika hili, katawanya mjumba ambao hauna kazi kwa sasa wala faida kama angejenga kiuchumi katika lile eneo na kipindi hiki angeweka appartments)
Huwa nakaa na kuongea na waliomudu maisha ya aina hii, nimejikuta nayaelewa sana!