Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Mimi sijaanza kupata hizo laki mbili kwa siku lakin inashangaza sana watu wanavyoshangaaa ? hiyo ni million sita tu kwa mwez,sema kazi za kuajiliwa zinalemaza sana.2010 wakati naanza ajira rafiki yangu alifungua hardware ndogo tu,leo ni bonge la millionea,analipa kodi serikalini mil 128 kwa mwaka.
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

View attachment 1259979
Assumption zako bado siyo sawa, kwani ukikaa sinza na unafanyakazi mjini hutumii mafuta tofauti yake ni ipi? Uhuru wa kuishi kwakona utumwa wa kulipa kodi ni tofauti sana, kwanza hakuna mwenye nyumba anayelipwa kwa mwezi, either mwaka, miezi sita au mitatu, huoni hiyo karaha imeondoka, mwanaume pambana jali chako
 
Tatizo watu Humu asilimia kubwa wanadhan kila MTU aliemo humu Ni rika LA Stori Vijiweni

Humu kuna watu wanabiashara kubwa sana.

Binafsi kuna watu wawili humu Ni Wafanyabiashara wakubwa sana na huwez dhania.

nilifahamiana nao humu humu kibiashara na mpk sasa tunafanya biashara mara kwa Mara.

Ofisi zao by minimum mauzo kwa Siku hayapungui milioni 20 tena halo nahisi hali inapokua mbaya.

Mana kuna kipindi ukifika ofsini utakuta MTU mmoja tu, kakaa anaandikiwa Oda ya milioni 15 - 30.

Sasa MTU kama uyo ukihoji faida ya LAKI MBILI kwenye mauzo ya milioni 50 kwa siku utaonekana kichaa.
Watu bado wana akili mgando wakidhani kama dunia kwao haiendi basi haitaenda kwa wengine wote.

Kuna watu wanatengeneza milions kwa siku, utawala wa magufuli huuhuu.

Nilioneshwa mtu mwenye turnover ya 30M a day sikuamini.
 
Bei gani
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

View attachment 1259979
 
Amina
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
 
Amina
Nina maoni haya: Kujenga na kuishi sehemu ya mbali na mji kama hiyo yako kwangu mimi ni jambo zuri sana. Na zaidi niseme sehemu za Kerege ni nzuri sana na kuna hewa safi na mtu unakuwa mbali na rabsha za mjini. Na kingine ni kuwa una uhuru wa kufanya mambo mengi kama bustani na ufugaji. Changamoto yake kubwa ni security. Maeneo kama hayo yanakuwa hatari hasa wakati wa usiku kwa sababu hakuna watu wengi. Kuishi maeneo kama hayo inatakiwa mtu uwe na uwezo mkubwa. Vitu kama gharama za usafiri visiwe issue, na uwe na ulinzi madhubuti (japo majambazi wakidhamiria wanakuwa huru zaidi kwa sababu ya kukosekana msaada wa haraka). Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alijenga karibu na shule ya Bunju B. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema amehamia porini. Leo hii hakuna anayemcheka na eneo limekuwa mji. Ushauri wangu: Hayo maeneo ni mazuri na siyo muda mrefu sana kutakuwa mji wenye watu wengi. Kama huna shida sana usiuze. Tafuta mbinu nyingine tu za kujikwamua na baadae utaona faida yake.
 
Sawa
Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.

Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.

Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.

Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.

Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.

Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.

Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.
 
acha usiwafuate waswahili wanaopenda Mjini.
Hapo Kerege patajakuwa Mjini kati kabisa, mwaka 1979 Sinza Makaburini ndio palikuwa mwisho wa Mji wa DSM linafuata pori hadi UDSM
Leo Kibaha ni Mjini kabisa ngoja hiyo njia 6 ya Highway km hukona mwendo kasi halishii Kimara
Ardhi ni mali huwezi linganisha Ardhi yenye ukubwa sawa kwa Miji ya Tanga, Dodoma au Mwanza
Tafuta wenyeji, Mkiti au Mjumbe wakutafutie wapangaji hiyo ni Rasilimali kubwa kuliko kupanga km Mhindi Mjini, Shika ardhi popote km Elimu kwani ni utajiri kuliko hao wezi wa leo tu
Kweri kabisa kuna mshikaji alinunua pande za uko uncle wake akamfanyizia mambo akamjengea nyumba moja mbovu choo cha nje jamaa nasikia kuuona mjengo akaupiga nyundo wote hadi Leo anajenga, imani yake kutakuwa mjini soon nyumba inaitwa nyumba ya nyundo hapo mitaa ya kelege.
 
NJE YA MADA:

MAPINGA, KEREGE, ZINGA, KIROMO, KITOPENI, UKUNI (MAENEO YALIYOPO BARABARA KUU YA DAR - BAGAMOYO)
NI MAENEO AMBAYO YANAONEKANA KEKI SANA KWA MTU KUMILIKI ARDHI,
NA
HIVYO WATU WENGI KUTOKA DAR ES SALAAM NA MAENEO MENGINE KUMIMINIKA BAGAMOYO KWA WINGI KWENDA KUNUNUA ARDHI (VIWANJA & MASHAMBA).

NOTION HIYO IMEIBUA WIMBI KUBWA LA MATAPELI (WANAOJIITA/KUJIFANYA MADALALI) NA KUPELEKEA WATU WENGI KUTAPELIWA NA MADALALI HUKO,
AMA KWA KUUZIWA MAENEO YASIYOWAHUSU AU KUWAUZIA MAENEO YENYE MIGOGORO,
YAANI UNAKUTA ENEO MOJA WAMEUZIWA WATU 6 TOFAUTI,
NA WOTE WANAZO NYARAKA-

SASA HAPO ZINAANZA KESI MAHAKAMANI SASA-
THE STRONGEST DO SURVIVE,
THE WEAKEST END UP TO PERISH.

UNAPOENDA KUNUNUA ARDHI BAGAMOYO,
KUWA MAKINI SANA-
SANA NA SANA, NA TENA ZAIDI YA SANA!!!
WEKA AKILI YAKO MBELE, KISHA PESA NYUMA,
NA SIO PESA YAKO MBELE, KISHA AKILI NYUMA.

(Kama umemaindi herufi kubwa, unaweza sema nikupe mwongozo).
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.

View attachment 1259979
Iyo nyumba au banda?
 
Back
Top Bottom