Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Umenena points,
Kama anauwezo wa kutumia 400000 kwa mwezi, inamaana hata uwezo wa kuimarisha ulinzi wake upo hasa kwa vibaka
Nashauri nunua mbwa ( Trained) hata wawili kukabiliana na vibaka, lakini pia kupitia bughudha ya vibaka kaa na serikali ya mtaa wakupitishie kibali ununua siraha.
Kuhusu galama za usafiri, nunua pikipik TV's Lita 2 kwenda na kurudi kwa umbali huo.
Pia usiuze Wala kupangisha zaidi buni mradi mdogo mdogo Kama kufuga kuku ili wakusupport kwenye running cost za pikipiki hasa mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekusikia MOTIVATIONAL SPEAKER.
 
Pole, ila uko sio mbali na Kariakoo.
Kwa macho siyo mbali, lakini round trip mpaka mjini ni roughly 42 kilometers... Kwa mafuta tu si chini ya Sh. 450,000 kwa mwezi... Bado usumbufu wa kutrack daily .... Social life na kule ninakotaka kuelekea naona... Nivunje huo mpaka au ukomo ... Naweza kupanga nikaenjoy more quality life, kiuchumi , kijamii na hata fursa za kiuchumi... Ofisi yangu ipo kati kati ya mjini.. Usafiri nitakuwa naenda kwa mguu... na nimeshafungua biashara nyingine ambayo nitaisimamia vizuri na ninaweza kuextend hata muda wa kuhudumia wateja wangu mpaka saa 4 usiku na kupita na kuangalia nini kinaendelea itakuwa rahisi... think out box.. Kwa kweli sasa hivi ni muda wa kurudi city center.... Nitafanya mambo mengi zaidi... Tujiurize kwa nini wageni tu ndio wanaishi maeneo mazuri mazuri ya miji yetu.
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
[/Q
tusha jua kua umejenga, what next??
 
Inabidi uwe wa kwanza kuingia barabarani kukwepa foleni. Pia weka mitambo ya ulinzi ikiwemo rapid security response.
 
Kuna Rafiki yangu mmoja mnyarwanda aliwahi kuniambia kama unataka kujenga nyumba basi isizidi Km 20 kutoka City Centre otherwise gharama za Maisha zitakuwa kubwa sana. Wakati naanza kujenga miaka hiyo nilizingatia ushauri wake nikapata eneo Km 17 from City Centre ndipo nikajenga. Faida naziona sasa maana hainigharimu sana kwenda na kurudi mjini kila siku.

Ushauri kwa mtoa mada

Hiyo nyumba ya Bagamoyo weka Electric Fence kisha funga Camera na pia tafuta kijana awe House Boy kama hayo mawili ya mwanzo yakishindikana. CCTV Camera bei ni rahisi sana. Mie nimefunga kwangu na nimeweka tangazo ila kuna madogo wa kitaani walikuja ingawa mbwa waliwakimbiza lakini niliwaona na nikaenda kuonyesha zile picha kwa majirani na bodaboda wote wa mtaani. Kuna mmoja anaitwa Baba Sele alihama kabisa kitaa maana watu walikuwa wanataka kuwachoma.

Hiyo nyumba kaa nayo itakusaidia umri wa kustaafu na sio kuiuza maana cha mtu kitu na mwenye nacho sio sawa na asiye nacho
Tangazo lilikuwa linasemaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh Kerege mbali sana!sisi tumehama Sinza tukahamia Madale mwisho!Dah siku za mwanzo kwa kweli nlkua napaona bush bush kweli lakini nimeanza kuzoea!Watu wanajenga sana pia viwanja vipo,panafikika kwa kupitia Wazo hill ukitokea Tegeta kibaoni vilevile unaweza fika Madale mwisho kwa njia ya Goba au Mbezi!Viwanja vipo japo vingi vishanunuliwa ila jaribuni kupitapita uku kabla ujajichimbia uko nje ya mji unless shughuli zako za kiuchumi ufanyie hukohuko!Changamoto iliobakia ni barabara ya Lami tu kuunganishwa kutokea Wazo hill kiwandani mpaka Madale mwisho huku!Figisuvza kisiasa ndio zinatuchelewesha inasemekana Watawala hawataki kisa ni jimbo la Mdee[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh Kerege mbali sana!sisi tumehama Sinza tukahamia Madale mwisho!Dah siku za mwanzo kwa kweli nlkua napaona bush bush kweli lakini nimeanza kuzoea!Watu wanajenga sana pia viwanja vipo,panafikika kwa kupitia Wazo hill ukitokea Tegeta kibaoni vilevile unaweza fika Madale mwisho kwa njia ya Goba au Mbezi!Viwanja vipo japo vingi vishanunuliwa ila jaribuni kupitapita uku kabla ujajichimbia uko nje ya mji unless shughuli zako za kiuchumi ufanyie hukohuko!Changamoto iliobakia ni barabara ya Lami tu kuunganishwa kutokea Wazo hill kiwandani mpaka Madale mwisho huku!Figisuvza kisiasa ndio zinatuchelewesha inasemekana Watawala hawataki kisa ni jimbo la Mdee[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
Niulizie kiwanja huko bei gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom