Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Una matatizo.
Niuzie mimi hiyo nyumba halafu njoo kwangu baada ya miaka mitano tu.
 
Hayo hayatuhusu kwa kweli, ekari 20 Kerege ni Zako na familia yako, hatuna sababu ya kujua!

Kama unataka kununua waswahili wamekaa barabara yote hiyo ya Bagamoyo nenda kawanunue! Sio lazima hapo kwake!
😂😂😂😂

Sio kwa povu hili
 
Hayo hayatuhusu kwa kweli, ekari 20 Kerege ni Zako na familia yako, hatuna sababu ya kujua!

Kama unataka kununua waswahili wamekaa barabara yote hiyo ya Bagamoyo nenda kawanunue! Sio lazima hapo kwake!
Hujajibu swali, au proposal, mtoa mada anataka kuuza wewe unaingilia nini.
Yatakuhusu tu baada ya miaka 5.
Kujifanya mjanja ni mama ya Ujinga.
 
Acheni kudanganyana,tatizo mnaangali ulipo leo ila hamjui kesho mtakuwa wapi,Kwa ushaur mdog tu ni kwamba Ukikaa kwako ni heshima kubwa sana,unakuwa huru,unapanga mambo binafsi bila bughdha yyte na mkumbuke maisha yanabadilika huwez jua kwamba kila siku utakuwa na uhakika wa kodi ya nyumba..Thanx
Nakazia hapa.
Walio wengi hudhani kwamba kwa sababu sasa hivi anapokea mshahara na kumudu kulipia kodi ya laki 4 au 5 basi miaka yote atakuwa na huo uwezo hawajui kwamba maisha hubadilika.
Ukitaka kujifunza hilo watafute watu waliofukuzwa kazi au kutumbuliwa au kupata maradhi watakupa experience
 
Hayo hayatuhusu kwa kweli, ekari 20 Kerege ni Zako na familia yako, hatuna sababu ya kujua!

Kama unataka kununua waswahili wamekaa barabara yote hiyo ya Bagamoyo nenda kawanunue! Sio lazima hapo kwake!
Du...mkuu
Una kiroho cha korosho kama hujijui!
Ungesema la maana kama ungewaunganisha muuzaji na mnunuzi badala ya kumwaga upupu!
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Tatizo umeshazoea kuishi mjini. Ni ngumu kupazoea kwa Sasa. Swala la wezi hata si za wapo pia.
Huo umbali unaouona Sasa, kwani wakati unajenga ulikua unaenda na ndege?.

Uza hiyo nyumba na gari ukanunue mjini. ili uwe unatembea tu kwenda kokote.
 
Lifestyle ya Wahindi ni next level. Nimeshangaa bilionea kuishi kwenye apartment
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Kutokana na sasa hela kuwa ngumu nimeweka ukuta mfupi, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba kupitia kwa madalali na Zoom haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Tafuta gari ya Diesel mkuu.
 
Back
Top Bottom