Najuta kuilinda na kuisaidia CCM ishinde, sasa navuna majuto

Najuta kuilinda na kuisaidia CCM ishinde, sasa navuna majuto

Ni sauti ya jamaa alietimuliwa kazi katika sera ambayo CCM walio serikalini wameivalia njuga, maana huonekani kiongozi mpenda maendeleo kama hujasimamisha na hatimae kuwafukuza kazi walio chini yako. Tanzania sasa inaingia katika wakati mwengine mgumu sana ni wakati wa majungu na kufukuwa makaburi.

Tayari wapenzi wengi wa CCM waliomo ndani ya vyombo vya serikali wameanza kuuma na kusaga meno, maana wengine wameshatimuliwa na wengi wapo njiani. Viongozi wakuu serikalini wanafukuza watu makazini na kuwasababishia majuto na mawazo, hio ndio CCM haitabiriki hata uipende vipi.
CCM oyee.

Kwa mlio makazini hasa wakurugenzi mmekalia kuti kavu, fukuza fukuza imeanza kama ni corona sasa imebadili jina ina kasi ya ajabu. Najuta kuichagua na kuzitoa kura zangu ili tushinde mbona wanatugeuka, alisikika mkuu mmoja wa operesheni ya ushindi wa CCM aliepigwa na chini.
Hata wapambe na madereva wa kina mdee na wabunge wenzake wanalalamika kuhusu maamuz ya utawala wa cdm Kwa kuwavua uheshimiwa mabos zao kulingana na vyuma vilivyokaza walikua na uhakika wa ada za watoto pamoja mahitaj mengineyo ila wanakamat hawajalibarik hilo.
 
Back
Top Bottom