Najuta kumpa ndugu yangu PS (playstation), kawa kama Teja

Najuta kumpa ndugu yangu PS (playstation), kawa kama Teja

S
Mkuu minions wa Shetani ni wengi,sio Freemasons tu.Ninaloweza kusema for certain ni kwamba Shetani ndiye mastermind wa ulevi.Kamtumia nani kuleta tabia ya ulevi sina hakika,maana watengeneza pombe ni wengi na wapo spread across the whole underground society spectrum.
Sawa mkuu.😂
 
Kwanza nimepata wazo,

Ngoja nifanye mpango nirud kwenye magame maana Hizi mbususu Sasa zitakuja kunitoa roho.

Mwenye game za mpira aje pm tufanye biashara
nimepunguza kucheza game nimeongeza kasi kwenye pombe yaani ikifika weekend me kurudi home saa 9 usiku kawaida.
 
TUNAFIKA ULIPO KWA DAR 0710701361 [emoji338]
FIFA 23 LA PS4 LIPO[emoji91][emoji91][emoji91]
PES 23 LA PS4 LIPO[emoji91][emoji91][emoji91]
PES 23 LA PS3 LIPO[emoji91][emoji91][emoji91]
Pia tunaweka games nyingine kali kwenye PSP, PS2, PS3, PS4 pamoja na PC.
KWA PS4 NI 15000 KWA GAME KWA MASHINE ZILIZOCHIPIWA TU.
KWA PS3 NI 5000 KWA GAME, GAMES KUANZIA TANO KUNA OFA.
KWA PS2 NI 2000 KWA GAME KUANZIA TANO KUNA OFA PIA.
KWA GAMES ZA PC NI 5000 TU.
KWA GAMES ZA PSP KUWEKEWA KWENYE SIMU NI 1500 TU.
PIA TUNAFANYA WINDOWS INSTALLATION KWA BEI POA KABISA NA KUWEKA MOVIES NA SERIES KALI.
TUNAFIKA POPOTE ULIPO HASA KWA DAR.
Kwa mawasiliano zaidi 0710701361.
Instagram www.instagram.com/skygames_arena
Nahitaji pes 2023 kwenye pc
Vipi upande wa specification za pc inacheza vizur kwa pc ya uwezo gani mkuu
 
Nakumbuka kipindi nipo chuo tulikuwa tunapiga mpaka saa tisa usiku ndio naenda kulala. Usifanye mchezo na addiction yake kuna jamaa alifuatwa na demu wake akamjibu anampotezea muda haoni yupo kwenye ligi.

Daah nakumbuka ile kauli ilimuuma sana demu sababu ilikuwa mbele yetu baada ya game kuisha jamaa akawa na kazi ya kubembeleza.
[emoji23]
 
Dah huyo kachelewa kuijua ps, mimi nlikuwa teja wa ps kipind niko la saba hadi form 2 nikaacha kabisa nkawa chizi kubeti sikukaa sanA nikaacha sasa yeye form 4 unaiba hela ili ucheze ps dooh..? Yuko mkoani kwani..?
Fom 4 wa sikuhz ana miaka 15 mbali sana 17
 
umeshazoea sasa huenda, kuna game ukianza kucheza hadi kazini unaweza usiende[emoji23] Call of duty zile mission zake unaweza kujiona ushakuwa navy au us Marines wa USA.

assassin's creed etc.
Oya COD walitulia sana japo sijawah limaliza pia Gost Recon hili nmemaliza mission zote lile wildland. Pia kuna Metal Gear Solid nalo sio pw japo la zamani kidogo
 
Tunafanana,
Mi mwnyw Ni pombe na Mbususu
Jana yenyewe nmerud home Saa 8
Sasa mkuu kurudi usiku mnene hivyo mama mtu home inakuwaje?

wanamindigi sana hawa watu.

Daah maana yani mkuu mpaka zilinigharimu nikaachana na manzi yangu tena nilimpenda. Mbaya yy alikuwa hapendi pombe.
 
Nahitaji pes 2023 kwenye pc
Vipi upande wa specification za pc inacheza vizur kwa pc ya uwezo gani mkuu
Game za sasa hakikisha pc haipungui uwezo ufuatao.

i3,5 or 7 gen ya 4+
ram 8gb
gpu kubwa kubwa walau kuanzia gtx 1050

hapo unakuwa na angalau uhakika wa kucheza game zote. or bora kuwa na ps4 tu maana now unaipata mpka laki 6 yenye hali nzuri mkononi mwa mtu.
 
Oya COD walitulia sana japo sijawah limaliza pia Gost Recon hili nmemaliza mission zote lile wildland. Pia kuna Metal Gear Solid nalo sio pw japo la zamani kidogo
Game zote hizo kila mwaka wanatoa mpya. so hata metal gear solid pia nadhani imefika 5.
 
Kawa kama zombi

Niliwahi kununua playstation Kwa mwanafunzi flan hivi wa chuoni alikuwa anadaiwa ada na hana pesa, aliniuzia hio mashine Kwa laki 3 na nusu, lengo langu lilikuwa niiuze hata kwa laki 5 maana hii mashine inauzwa takribani laki 8 madukani, kazi zilinitinga nikawa nimeiweka tu sebleni.

Sasa Kuna ndugu yangu huyu kamaliza form 4 mwaka jana anaenda kuanza chuo mwezi huu alikuja kunisalimia mwezi wa 7 hivi, aliiona hio ps na akaanza kuitumia, ilibidi akae siku 4 lakini game lilimnogea alikaa wiki, anavyoondoka aliniomba sana nimpe mashine, nikampa ila nikamwambia aitunze atairudisha akienda chuo.

Mwezi uliopita nimepigiwa simu na mama yake analalamika nimemuharibu mtoto wake, muda mwingi anacheza ps, kulala saa Saba usiku, kapoteza umakini na kawa kama Teja.

Ilibidi mama yake amnyang'anye hio ps kaifungia sehemu anayoijua yeye kaniambia siku nikiihitaji atanisafirishia.

Baada ya kufungiwa hio ps dogo akaanza kwenda kucheza kwa rafiki zake wenye ps, muda ambao marafiki zake hawapo kaanza kwenda kwenye frem za mtaani wanazochezesha ps kwa hela.

Sasa huku kwenye frem wanazochezesha ps huwa wanalipia pesa kwahiyo dogo kaanza kuiba Hela nyumbani Ili aende kucheza, kukiwa hakuna pesa anaweza kuuza vitu vidogo vidogo, baba yake alipogundua alimtembezea kipigo cha haja lakini bado hasikii.
Akikua ataacha
 
Kama matokeo mazuri waachie tu watoe ushamba.

Hizi ps huwa Kuna kipindi kinafika zinazoeleka.

Kwa Sasa itumie iwe kama kifaa cha adhabu, unaweza kuwapa kazi flani wasipoifanya unaifungia ps, makosa madogo madogo unaifungia hata siku 1 ama 2, makosa mazito dozi inaongezwa
Mnaharibu watoto nyie
 
Alafu naona watoto wa kiume ndio mko na addiction sana na hizi vitu. Hawa wa huku bado ni wadogo wadogo wapo shule likizo huwa wanakuja huku napoishi ukisema ufiche wanashinda wanalia siku nzma hawawezi hata kula kwa hiyo nawaacha tu.
Kuna muda nazima umeme makusud wanashinda kama wagonjwa huwa nashangaa sana. Wazazi wao wanajuta kuwanunulia hayo magemu sijui nini kifanyike kuwanusuru.
Unaogopa mtu kulia?
 
Back
Top Bottom