Najuta kununua 2009 Mitsubishi Pajero 3500Di-D: Auto

Najuta kununua 2009 Mitsubishi Pajero 3500Di-D: Auto

Mwaka 2019 nilijichanganya kwenye 2009 Mitsubishi Pajero 3,500Di-DAuto, Petrol. Kitu inakunywa karibia 21 litres/100km (highway). Pesa mzozo bado nalipa deni la NMB. Gari haliuziki.

NB: kupenda sifa kumenitokea puani.
Mbona hiyo gari nzuri labda kipato chako ndo duni njoo tubadilishane na Nissan patrol 4500cc diesel......ndo utajua kwamba mjini kuna watu wanaishi kwa gharama kubwa.
 
Mtoa mada tuwekee picha angalau
Nadhani alijichanganya hapa

EFFCB6DF-CF11-4E04-A2B1-28742E99C008.png
 
Nilichukua brevis kwa bei ya kutupa 2m mbona niliuza laki nane gari full tank njombe mbeya haitoboi
Mnanunua gari zikiwa vimeo mnakuja kuzibatiza majina ya ajabu ajabu,

Yaani 70 litres ushindwe kutoboa kilometa zisizozidi 250???

Hiyo gari ikiwa full tank unatoboa Dar Makambako vizuri kabisa kama ni nzima.
 
Mwaka 2019 nilijichanganya kwenye 2009 Mitsubishi Pajero 3,500Di-DAuto, Petrol. Kitu inakunywa karibia 21 litres/100km (highway). Pesa mzozo bado nalipa deni la NMB. Gari haliuziki.

NB: kupenda sifa kumenitokea puani.
Kwa rate hiyo ya fuel consumption, unamiliki gari ambalo linatumia mafuta sawa na fuso la cubic MITA 4.5 likiwa full loaded na mchanga au kokoto au mawe. Pole sana mdau
 
Back
Top Bottom