WanaJF
Habari zenu, heri ya Ramadan na Kwaresma, matumaini yangu wote wazima, waliyo na changamoto Mungu akawape njia.
Ni kijana barubaru wa miaka 28 mwenye nguvu na Afya.
Wakuu kama kichwa Cha habari hapo juu kinavyo jieleza, nilioa huyu single mother mwaka mmoja uliyo pita baada ya kujiridhisha tabia zake zinafaa kuwa mke na mm bila hiyana nikachukua nikaweka ndani, nikatia pamba maskioni kuzuia kelele za "KUOGOPA SINGLE MOTHER" kumbe nilikua najidanganya nafasi yangu.
Wakuu kila kukicha nikimtazama huyu mtoto wake Roho yangu inauma kwa uchungu wa majuto ya kuoa huyu single mother ni kama nilirogwa hivi kuoa huyu mwanamke, kivipi yaani natunza mbegu za mwanaume mwingine naye yupo tu anakula Bata at the end mtoto aje kunikana mimi siyo baba yake, kwanini hata sikuchukua mdogo wangu nikae naye , kuliko kuhudumia damu ambayo siyo yangu. Wakuu najuta sana.
Niwe Mkweli nafsi yangu inajuta sana. Nahitaji msaada wa kisaikolojia nijinasue kutoka hapa nilipo kwama, imefika hatua hata kukaa nyumban siwezi kabsa.
Pia naomba wale waliyo wai pitia hii situation walijinasuaje? Mnisaidie.