Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Katika watu wenyewe huruma na roho nzuri Kwa watoto ni wanaume Hilo halipingiki ila nakushangaa wewe utakua na shida
Nakwede naona unazidi kumtia wenge men mwenzetu, yaani ajione ana roho mbaya kwa malaika sio 🤣🤣🤣🤣
 
Achana na huyo mwanamke,tafuta mwanamke ambaye hajazaa uoe.Kila mtu ahukumiwe na maamuzi ya maisha yake-yeye alichezea maisha yake kwa kuzaa mapema basi akae bila kuolewa afaidi matunda ya maamuzi yake
100%
 
Kinachokutesa hapo ni roho mbaya...tafadhali ondoka,usijeua mtoto...yaan ondoka hapo haraka.
Hukujua kuwa singlemom maana yake anamtoto ambaye si damu yako?
Siyo Roho mbaya, Hakika ungejua ni kwa namna gani napambana kumpenda huyu mtoto usingesema hivyo. Nalazimisha nafsi yangu impende lakini imeshindikana.
 
Vijana wamekua wapumbavu sasa. Wanachuagua mke kiholela holela tu kama vile sio maisha yao. Ukiwasanua utasikia mapenzi hayashauriki na blah blah kibao. Wpte tunajua future ya mahusiano/ndoa ni fumbo, lakini iyo sio sababu ya kufanya gamble kwenye red flag. Wanawake wenye rekodi nzuri wapo kwanini ufanye gamble kwa mwanamke mwenye rekodi mbaya?
 
Fungua uzi kuhusu kutimuliwa na babako mzazi ukingali mwanafunzi kinda kabisa!
 
Angekuwa ni mwanamke ameolewa mwanaume mwenye mtoto akawa anapitia changamoto kama hizi ungetoa ushauri mwingine au ndo huu huu both sides?
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako huu Kiongozi. Najuta sana kufanya hili Kosa ukizingatia Mimi Sina mtoto nje. Sijui nilijichanganya vipi? But baado nna mda naamini nitarekebisha.
 
Daah🙏🙏🙏
 
Angekuwa ni mwanamke ameolewa mwanaume mwenye mtoto akawa anapitia changamoto kama hizi ungetoa ushauri mwingine au ndo huu huu both sides?
Sister kuhudumia ni kazi sana ukizingatia Mimi Sina mtoto nje!! Provider mkubwa hapa nyumbani ni Mimi imagine uhudumie mwanamke mwenye mtoto asiye wako ebu Jaribu kivaa viatu vyangu.
 
Mtoto wa umri gani?
 
Naomba nieleweke simchukii huyu mtoto na Wala Sina shida naye. Lakini nafsi yangu imegoma kabsa kumpenda huyu mtoto wake. Najilazimisha sana kumpenda huyu mtoto lakini Moyo wangu unegoma kabsa it has been almost 1 year ni mda Sasa niutue huu mzigo nafsi yangu ibaki huru.
 
Mtoto hana kosa ni bora hizo hasira uzielekeze kwa mtu mwingine na sio huyo mtoto
 
Mdoangu kalelewa na baba mwingine mara baada ya mama kukacha ndoa.

Huyo mdoangu hamtaki kabisa baba yangu ambae ni baba yetu wa ukweli.

Anafanya kila kitu kwa yule baba wa kambo.

Anamtii na kumheshimu pia kujitoa kwa kila kitu kwa yule mzee japo si babake.

Vijana mnao wa-diss single maza kisa mwanae atakugeuka hua nawashangaa sana.

Mtoto kukugeuka ni kutokana na namna utkavyo mlea.

Kwann asikugeuke Ukimlea kijeshi, kibaba wa kambokweli kweli, kiroho mbaya... mpaka anauliza mama huyu kweli babangu?
 
kwani kichanjio chako amechukua huyo single mother? kama unacho lala mbele!! oa kigori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…